Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo
la umoja wa mataifa FAO, linaonesha takribani asilimia 70 ya wakazi wa nchi za
Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania wanategemea kilimo
kama njia ya kujipatia kipato sambamba na chakula na uhakika wa lishe bora.
Ingawa hali hiyo imekuwepo myakanenda
myaka rudi, sasa ni tofauti kwa miaka ya hivi karibuni mabadiliko ya tabianchi
yamekuwa ni mwiba mchungu ndani ya sekta hiyo ya kilimo na kuibua changamoto
nyingine katika jamii hasa familia zenye kipato cha chini, ukosefu wamvua za
kutosha katika misimu sahihi ya kilimo, husababisha upungufu wa chakula na baa
la njaa katika familia nyingi na wahanga wakubwa wa janga hili ni watoto,
wanaolazimishwa kufanyiwa vitendo vya ukatili ili wapate chakula kila siku.
TATIZO NI KUFANYIWA UKATILI WATOTO.
Matukio ya kubakwa, mimba na ndoa za
utotoni, kulawitiwa, kuchomwa moto mikono watoto, kuunguzwa mikono na maji ya
moto hata kuchapwa kupita kiasi, yanaendelea kuripotiwa siku hadi siku katika familia
nyingi, vyombo vya ulinzi na usalama, mashirika ya kutetea haki za binadamu na
hata viongozi wa dini macho na fikra za waliowengi hudhani tatizo ni kupolomoka
kwa maadili kwenye jamii husika.
Jambo hili linapaswa kuangaliwa kwa upana
wake kila mmoja kwa ngazi ya familia,jamii na taifa kwa ujumla wake juu ya
vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, ikiwa chakula hakuna nyumbani, hakuna
uhakika wa kupata kazi inayoweza kuingiza kipato kunauwezekano mkubwa wa
familia hiyo kuwa na migogoro isiyo isha na kupelekea kusambalatika kwa familia
hiyo na watakao athirika zaidi ni watoto maana watakosa mahitaji muhimu yakilasiku
kama vile chakula na malazi.
Jedwari hili linaonesha uhalisia wa matukio
hayo hasa mimba za utotoni katika Mkoa wa Morogoro, mwezi Julai-Septemba 2022.
CHA UKATILI KWA WATOTO NI NINI:
Kwa mujibu wa takwimu hizo kutoka ofisi ya afisa
ustawi wa jamii Mkoa wa Morogoro za mwezi Julai hadi Septemba mwaka 2022
zinaonesha kwamba, Miongoni mwa sababu zinazo sababisha ongezeko la matukio
haya ni umasikini wa kipato cha kutosha pamoja na ukosefu na uhakika wa chakula
katika familia, hivyo watoto wanapokosa uhakika wa kupata chakula nyumbani ni
rahisi kushawishiwa kwa vipande vidogo vya fedha na kufanyiwa ukatili hasa
watoto jinsi ya kike kufanya ngono pasipo ridhaa yao.
msimamizi wa mradi wa kilimo hifadhi unaotekelezwa Mkoani Kigoma na shirika la
chakula na kilimo la umoja wa mataifa FAO nchini Tanzania ,anasema FAO kupitia
mradi wake wa Ushirikiano wa Pamoja Kigoma (KJP) wameamua kuhuisha kikosi kazi
cha taifa kinacho shughulikia kilimo hifadhi ili kupambana na mabadiliko ya
tabianchi hasa kwa kuwaelimisha wakulima, mabadiliko hayo yanaathari kubwa
kupungua kwa chakula kwenye familia nyingi nchini Tanzania.
“Mambo tunyo yaangalia katika kikosi kazi
hiki cha taifa moja ni, kuidhinisha yale yaliyomo kwenye ripoti ya kitaifa
kuhusu maeneo ambako Kilimo Hifadhi kinatekelezwa, Pili kukubaliana kwa pamoja
maeneo ya msingi yatakayojumuishwa kwenye mifumo ya kitaifa na kikanda
kuhusiana na Kilimo Hifadhi.
Tatu kujenga uelewa miongoni mwa wajumbe
wa Kikosi Kazi Cha Kitaifa kuhusu kilimo hifadhi na kusaka mbinu za kupanua
usambazaji wa mbinu hizo za kilimo na nne, kuandaa mpango kazi na bajeti kwa
ajili ya majukumu ya kikosi kazi hiki, ili kufikisha elimu hii kwa wakulima kwa
ajili ya kulima kwa faida na kupata chakula cha kutosha kitakachoweza
kumfikisha mkulima katika msimu mwingine wa kilimo pasipo upungufu wowote
kwenye kila kaya.
Katika kufikia malengo hayo tutakuwa na
majukumu mahsusi ikiwemo kuandaa orodha ya Washiriki Wakuu Wa Kilimo Hifadhi
Katika sekta binafsi na ya umma walio mstari wa mbele kusongesha teknolojia za
kilimo hifadhi hapa Tanzania” alisema Moorine Lwakatare.
Joseph Makoye nimkulima kutoka katika kijiji cha dakawa Wilayani Mvomero
anasema juu ya mabadiliko ya hali ya hewa amegeukia kilimo cha bustani ya nyaya
kulingana na kilimo cha mazao ya mahindi kushindwa kuvumilia ukame.
“Niliandaa shamba hili hapa nilipo kwa
ajili ya kupanda mahindi mwezi wa kumi na moja kama ambavyo ilivyo kawaida ya
mvua za vuri, lakini mvua haikunyesha kwa wakati ikaja kunyesha mzi wa kumi na
mbili nayo sio ya kulidhisha nikapanda hatimae mahindi yamekauka, nikaamua
kupanda nyanya ambazo naweza kumwagilia na ninakuwa na uhakika kiasi furani cha
kuvuna hata kidogo kuliko mahindi.
Pakiwa na maji kidogo ya kumwagilia kwenye
la mahindi wakati wa jua kali unapo mwagilia mahindi yanaweza kudumaa na
kushindwa kubeba kwa sababu unyevu utakua mdogo tofauti na mazao ya mbogamboga
na nyanya, najua baada ya miezi miwili na nusu naweza kuanza kuvuna nya kidogo
kidogo nakwenda kuuza ili nipate pesa ya kunua chakula cha familia ” amesema Joseph
Makoye.
shirika la Sustanable Agriculture Tanzania (SAT) Mkoa wa Morogoro anasema
kilimo wanacho wafundisha wakulima wengi nikulima kilimo hai ambacho hakitumii
kemikali nyingi, bali watumie mbolea ya asili na kulima kitaalamu ili kupata uhakika
wa chakula na mazao mengi zaidi hata akiba ya biashara kulingana na mabdiliko
ya tabianchi pamoja na kulinda afya ya binadamu.
“Wakulima
wadogowadogo tunawafundisha zaidi kilimo cha mazao ya muda mfupi kamavile mboga mboga ambayo huchukua siku kumi na nne
hadi siku tisini, yanakuwa tiyari kuvunwa na kuuzwa” amesema Dr.Kizito Mwajombe.
UTATUZI WA JAMBO HILI NI UPI:
Moorine Lwakatare Wakulima
sasa wanapaswa kukubaliana na mabadiliko ya tabianchi na mbinu zinazopendekezwa
kutumia katika kilimo kama ambavyo shirika la chakula na kilimo la umoja wa
mataifa FAO lilivyo anza kuhamasisha kilimo hifadhi, ilikuendelea kupata mazao
ya kutosha na kuondoa njaa katika familia, kwani janga hili linawasukuma watoto
wadogo kufanyiwa vitendo vya ukatili kwa ahadi ya kupewa fedha na chakula.
Wakulima tunao tegemea mvua tuanpaswa
kuzingatia mbinu za wataalamu, hasa kilimo hifadhi ambacho hakisumbui udogo
mara kwa mara, kulima kwa mzunguko na kuweka matandazo katika mazao ili kutunza
unyevu unyevu, Joseph Makoye anasema.
Serikali kupitia Wizara ya kilimo na
mashirika yanayo jishughulisha na kilimo kamavile FAO, WFP, SAT nawengine, wanapaswa
kushirikiana ili kuipeleka elimu ya kilimo hai na kilimo hifadhi kwa kila
mkulima kwaajili ya kupambana na baa la njaa kwenye kaya, Dr.Kizito Mwajombe.
Na, John Kabambala-Morogoro.