ya hali ya hewa na ongezeko la joto yameongeza ueneeaji wa baadhi ya magonjwa
yanayotokana na maji na vidudu vya magonjwa, na kupunguza uzalishaji wa chakula
kwa baadhi ya watu walio katika mazingira magumu duniani kote, Kuna uwezekano
mkubwa kwamba hasara za kiafya zinazosababishwa na dhoruba na mafuriko
zitaongezeka karne hii ikiwa hakuna hatua za kukabiliana nazo.
Na katika
jambo hili waathirika wengi wa janga hili ni watoto ambao seri zao bado
hazijakomaa kuhimili misuko suko ya mawimbi makubwa ya joto, mvua kubwa,
mafuriko na magonjwa yasio zoeleka kuwapata watoto, karne hii yanawapata.
Hatua za
kukabiliana na hali ya hewa ili kulinda afya na kukabiliana na mafuriko ni
pamoja na upangaji bora wa matumizi ya ardhi, uhamasishaji wa jamii, kupunguza
hatari ya kupata huduma muhimu kama vile maji, nishati na chakula, na hatua za
kusaidia kaya zilizo hatarini, hali ya tahadhari ya mapema kwa jamii hasa walio
na makazi kwenye mikondo ya maji na vimbunga waweze kuchukua hatua za kuhama
katika maeneo hayo ili kuepusha athari za kiafya na vifo.
TATIZO
Tatizo ni
ongezeko la joto, ukame, mafuriko baridi kali na magonjwa yasio ya kawida kwa
watoto, ripoti ya Unicef iliotolewa mwishoni mwa mwaka 2022, inaonesha kwamba mwaka
2020, karibu watoto milioni 740 sawa na
mtoto 1 kati ya 3 ulimwenguni waliishi siku 83.54 zenye joto
zaidi lenye nyuzi joto 35°C, na
ripoti hiyo ya Unicef inaonesha
kwamba, Ifikapo 2050 itafikia hali ya juu ya utoaji wa hewa chafu kwa takriban
digrii 2.4 za ongezeko la joto, takwimu
hii inatarajiwa kuongezeka hadi takriban milioni 816
sawa na watoto 2 kati ya 5 watakuwa wenye hatari zaidi.
Jedwari hapa chini linaonesha zaidi.
Sababu kuu ya
ongezeko la tatizo hili duniani ni gesi chafu itokanayo na viwanda, ongezeko la idadi
ya watu hutajwa pia kama
sababu mojawapo, shughuli za maendeleo ya binadamu zinazo sababisha kuharibu
mazingira na ukataji miti hovyo, vyombo vya moto kama vile Ndege, magari, pikipiki na vifaa
vitumiavyo umeme majumbani, jambo lingine ni ukataji miti kwenye misitu pasipo
kurejeshea miti mingine, hivyo moja kwamoja binadamu hutengeneza jangwa lisilo
la asilia.
Tofauti ya
hali ya hewa inahusishwa na usambazaji wa kijiografia, Magonjwa yanayoenezwa na
ambayo yanajulikana kusababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa ni pamoja na
malaria, dengue, homa ya bonde la ufa, homa ya manjano, mzunguko wa mafuriko na
ukame huongeza magonjwa yanayosababishwa na maji kama vile typhoid na
kipindupindu.
Leonard Kitindi msimamizi miradi
kutoka shirika la CONASU anasema mabadiliko ya hali yahewa ni
janga la kitaifa na kidunia, na jambo hili huathiri maeneo yote na viumbe
vyote, kwa upande wa binadamu waathirika wakubwa zaidi ni watoto ambao kingazamili
yao hazijakomaa kuhimili mawimbi mabdiliko ya hali yahewa.
“sisi
kama CONASU baada ya kugundua chanzo cha tatizo hili, tumeanza kuelimisha jamii
juu ya utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji, kwa kupanda miti,kurejeshea
maeneo ambayo yalisha katwa na kubuni njia nyingine za fursa za kibiashara
zilizopo kwenye maeneo ya jamii, ilikujipatia kipato nasio kukata miti kama
njia ya kujipatiakipato, mfano tuna mradi wa kurejesha miti aina ya mikoko kule
Bagamoyo Mkoani Pwani” amesema Leonard Kitind.
Kwa mijibu
washirika la afya ulimwenguni WHO, katika
kipindi cha miaka 10 nchini Tanzania tayari
kumeripotiwa matukio ya ugonjwa wa malaria hasa katika maeneo ya nyanda za juu
ambayo kijadi yalikuwa hayana mbu na malaria kama Tanga, Kilimanjaro, Iringa,
Kagera na Mbeya, miongoni mwa mengine, ambako hayakuwa yameenea hapo awali.
Malaria na
kipindupindu ni miongoni mwa masuala muhimu ya afya ya umma hasa kwa watoto
chini ya umri wa miaka mitano na miongoni mwa wanawake wajawazito, uwezekano wa
kuugua malaria mara nne zaidi kuliko wastani wa wakawaida jambo hili
linashuhudiwa kuwa ni moja ya visababishi vya mabadiliko ya hali yahewa.
Kwa upande
wa Daktari bingwa wa watoto Theopista
Masenge kutoka chama cha madaktari bingwa wa watoto Tanzania (PAT) amesema athari ya mabadiliko ya hali
ya hewa kwa watoto nikubwa kuliko jamii inavyo ichukulia, mfano kwa sasa kunamagonjwa
mbalimbali ambayo huwapata watoto kwa kujirudia rudia na mengine hayakuzoeleka
katika jamii.
Hali ya
joto,baridi kali,mafuriko yasababishwayo na mvua kubwa, ukame na upungufu wa
maji safi na salama yanapozidi huongezeza magonjwa yasio eleweka kwa watoto,
mfano kwa mujibu wa ripoti ya masuala ya afya ilio tolewa hivi karibuni ya
mabadiliko ya hali ya hewa ya asili inaonesha kwamba “Zaidi ya nusu ya magonjwa
yanayojulikana ya binadamu yanaweza kuchochewa na mabadiliko ya hali ya hewa”.
Dr. Theopista Masenge.
iliyozinduliwa jijini New York Marekani mwishoni mwa mwaka 2022 na shirika
la UNICEF ,inaonesha kwamba watoto milioni 559 kwa sasa wanakabiliwa na joto Kali ulimwenguni kote.
Hali hiyo inategemewa kuwa mbaya
zaidi ifikapo mwaka 2050, watoto wote duniani ambao wanakadiriwa kuwa bilioni 2.02 watakuwa wameathiriwa na mawimbi
tofauti ya joto kali bila kujali wapo kusini au kaskazini mwa dunia, na vile
vile bila kujali ongezeko la joto litakuwa katika kiwango cha wastani wa nyuzi
joto 1.7 katika kipimo cha Selsiyasi au kiwango cha juu cha nyuzi joto 2.4
katika kipimo cha Selsiyasi.
Ripoti hiyo inaionesha Tanznia kuwa nimiongoni mwa nchi zilizo
kwisha onja janga hilo la mabadiliko ya hali ya hewa hasa kuongezeka kwa joto
na kuwaathiri watoto, ambapo kwa kipindi cha mwaka 2020 zaidi ya watoto milioni
tano sawa na asilimia kumi nasaba waliathirika na joto kali, na inakadiriwa
kuongezeka zaidi ifikapo mwaka 2050 kama jedwri linavyo onyesha hapa.
Tanzania |
MWAKA |
WATOTO WALIO ATHIRIKA KWA MAWIMBI YA JOTO. |
ASILIMIA |
MUDA WA MAWIMBI YA JOTO |
ASILIMIA |
2020 |
5.2 million |
17% |
– |
– |
|
|
WATOTO WATAKAO ATHIRIKA KWA MAWIMBI YA JOTO. |
|
MUDA WA MAWIMBI YA JOTO WATOTO WATAKAO PITIA. |
|
|
2050 |
35.4 million |
100% |
26.3 million |
74% |
Asha Juma mkazi wa Bigwa
Manispaa ya Morogoro yeye anazaidi ya miaka 50 anasema kila mwaka unapo isha,
hali inabadilika na mabadiliko haya yanawasumbua zaidi watoto wadogo, “kilasiku unakuta mtoto na mama yake wapo
hospitali asubuhi mchana na jioni, ukiingia ndani ya nyumba ambayo inawatoto
utakutana na mabox tofauti tofauti ya dawa za watoto, kwa sababu leo ana
ugonjwa huu na kesho ana ugonjwa huu kila ugonjwa una aina ya dawa yake, hivyo
haya mabadiliko ya hali ya hewa yanaathiri zaidi hiki kizazi tofauti na enzi
zetu”
KIPI KIFANYIKE
KUREJESHA HALI YA AWALI:
Ripoti ya UNICEF imeshauri kwamba:-
kila nchi lazima ibadilishe huduma muhimu za kijamii WASH, afya, elimu, lishe,
ulinzi wa kijamii ili kuwalinda watoto na vijana, ikiwa nipamoja na utungaji wa
sera maalumu na miongozo juu ya athari zitokanazo na mabadiliko ya hali ya
hewa.
Bi, Asha Juma anashuri, Serikali
na wanasiasa wanapaswa kuchukua hatua za maksudi na sio kungojea tena, maana
hakuna dunia nyingine isipo kua nihii pekeyake, udhibiti wa uchafuzi wa hewa kwenye
viwanda, uchomaji misitu nk.
“Hili
siojambo tena la kuingalia na kusubiria Serikali kuweka amri bali, ni kila
mmoja wetu kuchukua hatua maana mabadiliko ya hali ya hewa hayachagui
pakuharibu, tupande miti, tupunguze matumizi ya kukata kuchoma mioto kwenye
misitu yetu ya asili na tuvilinde vyanzo vyetu vya maji” Leonard Kitindi.
Dr. Theopista Masenge yeye anashauri kila
mwananchi apande miti kuzunguka maeneo yake yakuishi, mashamba yake lakini pia
kuna ulazima wa kupima afya mara kwa mara familia nzima na hasa watoto,
ilikubaini endapo kuna ugonjwa wowote na kuchukua hatua mapema.
Na, John
Kabambala-Morogoro.