By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
Tanzania Kids Time
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Mazingira
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Wasiliana Nasi
Reading: MIKUNDE CHANZO CHA LISHE BORA KWA MTOTO
Share
Notification Show More
Latest News
Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
TANZANIA WILL HOST CIGOFA4 TO FIND CONCRETE SOLUTIONS FOR YOUTH LAND QUESTIONS
Editor's Pick
Aa
Aa
Tanzania Kids Time
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi
  • Contact
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Tanzania Kids Time > Blog > Afya > MIKUNDE CHANZO CHA LISHE BORA KWA MTOTO
AfyaElimu

MIKUNDE CHANZO CHA LISHE BORA KWA MTOTO

Tanzania Kids Time
Last updated: 2024/01/29 at 2:30 PM
By Tanzania Kids Time 9 Min Read
Share
SHARE

 

Tanzania,
mazao jamii ya mikunde yanashika nafasi ya pili kwa ulaji, ikiwa nyuma ya mazao
ya nafaka. Mara nyingi mazao haya ya mikunde yamekuwa yakiliwa kama mboga
pamoja na nafaka, baadhi ya mikunde kama kunde na maharagwe, majani na matawi
yake yamekuwa pia yakiliwa kama mbogamboga.

 Shirika la Chakula
na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) linatafsiri kuwa mikunde ni jamii ya
mimea ya kunde ambayo imekaushwa, inajumuisha aina zote za mbaazi, dengu,
kunde, choroko, njugu mawe na maharagwe.

Mikunde, karanga na
mbegu za mafuta ni vyanzo vya protini ambavyo ni vya bei nafuu, na vyanzo
vizuri vya madini ya chuma, zinc, fosforasi, magneziamu, vitamini B, foleti na
nyuzi nyuzi.

“Kote duniani na katika bara la Afrika, kumekuwa
na ongezeko la uzalishaji wa mazao haya ya mikunde. Kwa mfano, kwa takwimu za
FAO 2014, Tanzania inaongoza Afrika kwa uzalishaji wa maharage (tani milioni
1.2), inaongoza kwa uzalishaji wa dengu (tani 150,000),
ni moja kati ya nchi tatu zinazoongoza kuzalisha zao la mbaazi na ni
moja kati ya nchi tano zinazoongoza kuzalisha zao la kunde (tani 191,000).

Pamoja na nchi yetu kujitosheleza kwa chakula,
bado Tanzania inakabiliwa na utapiamlo ambapo theluthi ya Watoto wamedumaa,
theluthi ya wanawake wana upungufu wa damu na theluthi moja ya wanawake wana
uzito uliozidi. Njombe, pamoja na kuwa ni moja kati ya mikoa inayoongoza kwa
uzalishaji mkubwa wa chakula nchini, inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya
Watoto wenye udumavu asilimia 50.4 kulingana na taarifa za Demografia ya Wizara
ya Afya (TDHS 2022)”
Hayo ya
lizungumzwa na Mkuu wa Wilaya ya Makete Juma Sweda, siku ya kilele cha maadhimisho ya Mikunde Duniani kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Athony Mtaka ambapo kitaifa yalifanyika Mkoani Njombe.

  Akiongea kwa niaba
ya Mwakilishi Mkazi wa FAO Tanzania Dr. Nyabenyi Tipo, Afisa lishe kutoka
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO)
 Bi Stella
Kimambo, 
 alisema Mazao jamii ya Mikunde yanafaida kubwa katika
miili ya Bidamu, lakini pia hurutubisha udongo, na mazo hayo nimojawapo ya
chanzo cha kupata protini, vitamin na uimalishaji wa kinga za mwili.

TATIZO NI NINI:

Familia nyingi zimekuwa
zikiyachukulia mazao ya mikunde kama chakula cha watu masikini na hivyo
kupunguza ulaji wake, mlo wa kawaida hauoneshi uwepo wa mikunde, Watu wengi
hula maharagwe lakini mbaazi, choroko na dengu hupatikana kwa nadra katika milo
ya kawaida, pamoja na kuwa na virutubisho vingi na kuuzwa kwa bei nafuu
ukilinganisha na maharagwe.

Tanzania ni mzalishaji
muhimu wa mikunde katika ukanda wa Afrika Mashariki, Mwaka 2021, Tanzania
inakadiriwa kuwa ilizalisha tani milioni 1.8 ya mikunde na zao hili ni miongoni
mwa bidhaa muhimu zinazouzwa kwa wingi nje ya nchi.

Mwaka huo huo, Tanzania
iliuza nje ya nchi mikunde yenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 269, kutoka
Dola za kimarekani milioni 193 mwaka 2020, Karibu
asilimia 85% ya mauzo ya mazao haya yamekuwa yakiuzwa
nchini  India.

 Pamoja na umuhimu
wake kwa upande wa lishe, mwenendo wa ulaji wa mikunde nchini umekuwa ukipungua
siku hadi siku, na kusababisha matatizo ya utapiamlo kwa watoto na watu wazima.

CHANZO CHA TATIZO:

Sababu zinazosababisha
tatizo hili ni hulka kwa baadhi ya kaya, kama vile tabia za ulaji wa chakula,
mabadiliko ya mapenzi ya mlaji, na kushindwa kwa wauzaji kuwianisha sifa za
mikunde na mapenzi ya mlaji, idadi ya wanakaya, na upatikanaji wa rasilimali na
mengineyo, jambo ambalo linaweza kupelekea ulaji mdogo kwenye familia. 

Kwa sababu hiyo jamii
inapaswa kuona umuhimu zaidi katika ulaji wa vyakula vyenye wingi wa protini
ili kupunguza utapiamlo, na magonjwa yasiyoambukizwa hasa kwa watoto walio
chini ya umri wa miaka mitano (5).

 Afisa kilimo na
mratibu wa masuala ya lishe kutoka Wizara ya Kilimo Tanzania Margreth
Natai
 amesema mazao jamii ya mikunde yapo mengi, yanayo paswa kutumika
kila siku katika mzunguko wa milo ya kila familia, ili kuwa na lishe bora,
ikiwa nipamoja na kuondoa udumavu kwa watoto, kuongeza damu kwa mama wajawazito
na hata wasichana walio katika umri wa kuzaa.

 Kwa upande wa
mtandao wa mazao jamii ya mikunde Tanzania (TPN) kupitia kwa mratibu wa
mtandao huo Ndg. Zirack Andrew, amesema mtandao huo unahamsisha
wakulima na jamii nzima kwa ujumla kulima mazao jamii ya mikunde na jinsi ya
kuyatumia, kwani yanabidhaa nyingi zaidi ambazo mkulima atanufaika nazo
kiuchumi mbali na faida ya kupata chakula bora.

 Kwa mujibu wa
ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria Vya Malaria Tanzania
wa Mwaka 2022  na Viashiria vya Hali ya Lishe inaonesha kwamba
kiwango cha Udumavu kwa watoto chini ya umri wa miaka 5, Tanzania ilikua na
asilimia 34% mwaka 2015/16, na asilimia 30% kwa kipindi cha mwaka 2022, ikiwa
imepungua kwa asilimia 4 tu kwa kipindi cha miaka 5.

Afisa lishe mtafiti
mwandamizi Vumilia Lyatuu kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe
Tanzania (TFNC) amesema Taasisi hiyo inahamasisha wanachi kula kula
vyakula ambavyo vinazingatia makundi mbalimbali ya vyakula, na hasa hutoa elimu
ya namna ya mapishi bora yasiyo sababisha virutubishi vinavyo takiwa mlaji
kuvipata vipotee wakati wakupika, mazao jamii ya mikunde ni miongoni mwa bidhaa
muhimu katika afya na lishe ikiwa ni pamoja na kuimalisha kinga ya mwili.

Mkurugenzi wa shirika la
People’s Care Initiatives Tanzania ( PCIT) Amina Mgeni wao
wanahamasisha program ya chakula shuleni, lengo likiwa ni kuendelea kuongeza
idadi ya wanafunzi shuleni kutunza afya zao na kuongeza ufaulu katika masomo,
“katika mazao jamii ya mikunde ni miongoni mwa mazao tunayo hamasisha
watoto wapikiwe shuleni hasa kupitia mradi wa AGRICONNECT “.

Mmoja wa wanafunzi
kutoka kwenye shule ya msingi Itipingi ambayo ni miongoni kati
ya shule kumi (10) zinazo nufaika na mradi AGRICONNECT unaofadhiliwa
na Umoja wa Ulaya (EU), 
na program ya chakula shuleni Janeth
Silvath
 amesema ladha ya chakula wanacho pikiwa kilicho changanywa kwa
mazao jamii ya mikunde ni nzuri na kila lishe ya kutosha  “Utoaji wa Chakula shuleni ni jambo muhimu
sana na nina naomba wazazi na kamati ya shule zingine waanzishe program ya kula
chakula shuleni kama hii”.
 

SULUHISHO LA TATIZO HILI:

Stella Kimambo-Afisa lishe kutoka FAO.

“FAO kwa kushirikiana
na Wizara ya Kilimo pamoja na Taasisi za serikali, Mtandao wa Mazao Jamii ya
Mikunde Tanzania na wadau wa maendeleo katika wiki ya mikunde Tanzania tuweza
kuendeleza yafuatayo 1, kuwajengea uwezo wapishi kutoka katika shule
zinazotekeleza mradi wa AGRICONNECT  Mkoa wa Njombe, pia
Baba na mama lishe katika Suala la Mapishi mbalimbali ya mazao jamii ya
mikunde,2) Wanafunzi wa Shule za Msingi zinazotekeleza programu ya Utoaji
Chakula Shuleni Mkoa wa Njombe, kushirikishwa zaidi kwa wanafunzi kufanya
chemsha Bongo, kuchora picha mbalimbali kwa kutumia mazao jamii ya mikunde
”
amesema Stella Kimambo .

Hata Wizara ya Kilimo Inapendekeza kwamba; 

-Wizara kutoa kipaumbele kwa mazao ya mikunde kwa
kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora na
viuatilifu
ili kuongeza uzalishaji na tija

-Wizara kufanya mapitio ya Mkakati wa Mikunde wa mwaka 2016 -2020 ili kuingiza masuala mapya
yanayojitokeza na ili kuendana na hali ya sasa.

-Wizara kuendelea kuhamasisha jamii umuhimu wa kuzalisha mazao ya mikunde na
kuhamasisha matumizi yake

-Wizara kuendelea kusimamia na kutoa taarifa za masoko (ya ndani na nje) kwa mazao ya mikunde ili kuwasaidia
wakulima kufanya biashara zenye tija.

Maadhimisho haya yafanyike kila mwaka ili kuhamasisha jamii kuzalisha na kutumia mazao haya
muhimu kiafya, kiuchumi na kimazingira.

Na, John
Kabambala-Njombe.

You Might Also Like

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi

Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili

Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania

KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.

UWEZO TANZANIA YARATIBU KIKAO CHA MIKAKATI YA KUWASHIRIKISHA WAZAZI UELIMISHAJI VIJANA STADI ZA MAISHA.

Tanzania Kids Time March 1, 2023
Share this Article
Facebook Twitter Email Print
Previous Article MABADILIKO YA HALI YA HEWA SABABU YA MAGONJWA NA VIFO KWA WATOTO
Next Article SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NI SULUHU KWA WATOTO WAKIKE
Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

Facebook Like
Twitter Follow
Youtube Subscribe
Telegram Follow
- Advertisement -
Ad image

Latest News

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
//

Tanzania Kids Time: A platform spotlighting children’s and women’s issues in Tanzania, focusing on education, health, and environmental conservation.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

© 2023 Tanzania Kids Time. Powered by Digital Media Innovation Program. All Rights Reserved.

Join Us!

Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..

Zero spam, Unsubscribe at any time.

Removed from reading list

Undo
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?