By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
Tanzania Kids Time
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Mazingira
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Wasiliana Nasi
Reading: SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NI SULUHU KWA WATOTO WAKIKE
Share
Notification Show More
Latest News
Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
TANZANIA WILL HOST CIGOFA4 TO FIND CONCRETE SOLUTIONS FOR YOUTH LAND QUESTIONS
Editor's Pick
Aa
Aa
Tanzania Kids Time
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi
  • Contact
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Tanzania Kids Time > Blog > Afya > SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NI SULUHU KWA WATOTO WAKIKE
AfyaElimu

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NI SULUHU KWA WATOTO WAKIKE

Tanzania Kids Time
Last updated: 2024/01/29 at 2:30 PM
By Tanzania Kids Time 11 Min Read
Share
SHARE

 

Picha na Kheel
Center/Flickr

Hebu nikurejeshe nyuma kidogo kuhusu historia fupi ya kuanzishwa kwa Siku hii ya Wanawake Duniani, Mnamo Machi 25, 1911 Kiwanda cha nguo
cha Kampuni ya Triangle Waist cha
New York Marekani, kiliungu kwa moto ambao uiligharimu maisha ya wafanyakazi 146 vifo hivyo vilitokea chini ya
dakika 20 tu, na wengi wakiwa ni  wahamiaji vijana.

Baada ya Vita kuu ya pili ya dunia,
Machi 8 ilianza kusherehekewa katika nchi kadhaa, Mnamo 1975, Umoja wa Mataifa
ulianza kuiadhimisha siku hii kama Siku ya Kimataifa ya Wanawake, Miaka miwili
baadaye, Desemba 1977, Baraza Kuu lilipitisha azimio la kutangaza Siku ya Umoja
wa Mataifa ya Haki za Wanawake na Amani ya Kimataifa kuadhimishwa siku yoyote
ya mwaka na Nchi Wanachama, kwa mujibu wa mila zao za kihistoria na kitaifa.

Tangu wakati huo, Umoja wa Mataifa na
mashirika yao wamefanya kazi bila kuchoka ili kupata usawa wa kijinsia duniani
kote na matokeo makubwa yamepatikana: mwaka 1995 Azimio la Beijing na Jukwaa la
Utekelezaji, ramani ya kihistoria iliyotiwa saini na serikali 189, ilizingatia
maeneo 12 muhimu ya wasiwasi, na kujumuishwa kwenye Lengo namba 5 la malengo
endelevu ya kudumu ya Umoja wa Mataifa “Ili Kufikia usawa wa kijinsia na kuwawezesha
wanawake na wasichana wote”
katika Ajenda ya 2030 ya Maendeleo
Endelevu.

Waliokufa kwa janga hilo la moto, wengi walikuwa
wasichana wenye umri kati ya miaka 14,15,16
na 17
, idadi yao ilikuwa 146 vifo
hivyo vilitokea chini ya dakika 20,hao
ni walioshindwa kujinasua kutoka kwenye moshi na moto huo, hili likiwa ni moja
ya majanga mabaya zaidi tangu kuanza kwa Mapinduzi ya Viwanda nchini Marekani,
kwa mujibu wa Smithsonian
Magazine
, bofya link hii ilikusoama zaidi. https://www.smithsonianmag.com/smart-news/american-garment-workers-who-helped-inspire-international-womens-day-180962364/#gXHV6kiTelvQEssi.99   .

Miongoni mwa wasichana waliofariki
katika ajari hiyo ya moto ni Kate Leone
alikuwa na umri wa miaka 14 wakati
moto huo ulipotokea. Mzaliwa wa Marekani, alikuwa ameishi Marekani kwa maisha
yake yote, Alizikwa kwenye makaburi ya Calvary mnamo Machi 28, 1911, 
bofya link hii ilikusoama  https://trianglefire.ilr.cornell.edu/victims/72.html

Na,
Rosaria Maltese
alikuwa na umri wa miaka 14 wakati moto huo ulipotokea. Mzaliwa wa Italia, alikuwa ameishi
Amerika kwa miaka 4. Alizikwa kwenye makaburi ya Calvary mnamo Machi 28, 1911,
hawa wote walikuwa wanafizikia, 
bofya link hii ilikusoama https://trianglefire.ilr.cornell.edu/victims/82.html
.

NCHINI TANZANIA HALI IKOJE?

Siku hii ya Wanawake Duniani wanawake na wasichana ulimwenguni pote hutumia siku hii kuzungumzia changamoto na vikwazo wanavyo kumbana navyo, katika maeneo ya kazi, shuleni na hata nyumbani ambapo nchini Tanzania wasichana wankabiriwa na ndoa za utotoni ambacho nikikwazo kikubwa katika maendeleo ya msichana mwenyewe,familia na taifa kwa ujumla wake katika nyanja ya afya na uchumi.

Katika kuyawasilisha hayo kwa niaba ya Watoto Nancy Kasembo ni Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamuhuri ya Muungano Tanzania, alipozungumza nami kuelekea siku ya maadhimisho ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika March 8 ya kila Mwaka, juu ya umri upi ni sahihi kuoa/kuolewa, “Sisi kama viongozi wa baraza la watoto
Tanzania, Wizara ya Katiba na Sheria haijatushirikisha moja kwa moja kutoa
maoni yetu juu ya umri upi ni sahihi wa kuoa/kuolewa, isipokuwa tunatoa maoni
yetu kupitia vikao vyetu ambavyo tuna kaa na Wizara ya Maendele ya Jamii Jinsia
Wanawake na Makundi maalumu”
 .

MATATIZO YANAYO WAKUMBA WATOTO WAKIKE NI YAPI?

Kupata
mimba kabla ya wakati, hatari ya kukumbwa na matatizo kipindi cha ujauzito na wakati
wa kujifungua, Vifo vya ghafla, Utapiamlo, Wasiwasi na mafadhaiko, viwango duni
vya elimu ya msingi na ujuzi wa kusoma na kuandika, Ndoa
za utotoni huendeleza umaskini, kuingia katika maisha ya matarajio duni, hatari
kubwa ya vurugu katika familia, unyanyasaji, na vifo vya mapema.

SIKU HII NI SULUHU YA VIKWAZO KWA WANAWAKE NA WASICHANA?

Mchakato wa kuitafuta haki ya kutoozeshwa
chini ya umri wa miaka kumi na nane (18) kwa watoto wakike, safari hii
ilianzishwa na mwana harakati wa kutetea haki za watoto wakike nchini Tanzania
mnamo mwaka 2016 Rebeca Gyumi, Na hapa nimemtafuta Wakili kutoka katika Taasisi
ya Msichana Initiative
Lucy Gidamisi
yeye anaanza kwa kuelezea mchakato huu na hatua zilipo fikia hadi sasa
…..Lucy Gidamis….. https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1678136765–less-file-Lucy-Gidamisi-Wakil.mp3 

Nimezungumza
na
Dr. Rose Reuben Mkurugenzi
mtendaji wa Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), nilimuuliza
ni jambo lipi ambalo mnatamani kulizungumza juu ya kuwa tetea watoto wakike ili
Sheria ya ndoa iweze kubadilika katika kipindi hiki cha maadhimisho ya Wanawake
Duniani?
….Dr. Rose Reuben..  https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1678214319–less-file-Ros.mp3

Na huu
ucheleweshwaji unasababishwa na nini
……Dr.
Rose Reuben…
https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1678138822–less-file-Dr.Rose-Reuben-.mp3 

Ndoa
za utotoni ni tatizo nchini Tanzania linalo sababisha wasichana kutotimiza
ndoto zao kielimu, Ndoa hizi mara nyingi husababishwa na hali duni za kimaisha,
mila na desturi potofu na ukosefu wa elimu juu ya madhara ya ndoa za utotoni.

Nancy
Kasembo

mwenyekiti wa baraza la watoto la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, anaiona
siku ya Maadhimisho ya Wanawake Duniani kuwa ni mkombozi kwa watoto wakike,
ambayo huazimishwa tarehe 8 /03 ya kila mwaka…. Nancy Kasembo… 
https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1678137406–less-file-Nancy-Kasembo-.mp3  

Nancy
nilimuuliza je, Wizara ya Katiba na Sheria nchini, imekwisha washirikisha moja
kwa moja juu ya kutoa maoni ya umri upi ni sahihi kuoa/kuolewa kwa
motto?………
Nancy Kasembo… https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1678137506–less-file-Nancy-Kasembo-.mp3  

 Wizara ya Katiba
na Sheria iliwasilisha Bungeni Mapendekezo ya Marekebisho ya Sheria kwa kuweka
masharti ya kuusawazisha umeri wa kuoa/kuolewa na kuwa miaka 18. Hata hivyo
umri wa Chini wa kuolewa Ulipendekezwa kuwa miaka 15 endapo masuala yafutayo
yatazingatiwa, jambo hili limefanya nimtafute mataalamu ili kutoa ufafanuzi juu
ya kipengele namba tano cha mambo yanayopaswa kuzingatiwa, kinacho sema “
Dktr.Amethibitisha
Mtoto anauwezo wa kuingia kwenye ndoa?”

 Daktari
anathibitishaje kuwa mtoto anauwezo wa kuingia kwenye ndoa?
 
Swali hili nimemuuliza Theopista Jacob yeye Dktr. Bingwa wa masuala ya watoto kutoka chama cha
Madaktari Bingwa wa Watoto Tanzania (PAT)
……. Dktr. Theopista Jacob… https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1678137609–less-file-Theosita-Jaco.mp3   

Kwa mujibu wa ripoti iliotolewa na
Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN WOMEN) iliopewa jina la “
MAENDELEO JUU YA
MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU
”
ya  mwaka
2022,inaonesha kwamba haki ya elimu kwa wasichana ni muhimu kwa kila mtu katika
nyanja ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na ukuaji wa uchumi na ustawi, kila mwaka
wa ziada wa masomo unaweza kuongeza mapato ya msichana akiwa mtu mzima kwa hadi
asilimia 20.

Ripoti hiyo iliolenga kuonesha usawa wa
kijinsia katika Malengo ya Maendeleo Endelevu, ambapo wasichana kutoka kwenye
kaya maskini zaidi na katika maeneo ya vijijini mwelekeo haujawa sawa, miongoni
mwa maeneo hayo ni Nchini Tanzania
hali bado inaonesha kuwa chini, kama ambavyo chati inaonesha hapa.

Sampuli ya nchi 29 zilizo na Takwimu za
hivi karibuni kwa wasichana wanaomaliza shule ya sekondari kwa jinsia, kwa wasichana
maskini wanaotoka vijijini na wasichana matajiri wanaotoka mijini ni asilimia
11.5 hadi 72.2, hivyo katika siku za maadhimisho ya Wanawake Duniani ya kila
mwaka ni lazima dunia ifahamu kwamba kundi la watoto wakike wanahitaji
kuondolewa vikwazo na kutimiziwa haki zao za msingi ikiwemo ya kupata elimu,
ripoti hiyo imesema.

KWA NINI WIZARA YA KATIBA NA SHERIA IMENDA KUKUSANYA MAONI MIKOA
HII?:

Mikoa iliowekewa rangi ya njano ndio mikoa kunako kusanywa maoni juu ya
umri upi ni sahihi wa kuoa/kuolewa,na iliowekewa rangi nyekundu ndio yenye
namba kubwa juu yandoa za utotoni.
Shinyanga (asilimia 59),Tabora
(asilimia 58)
,Mara(asilimia
55),Dodoma
(asilimia 51) ,Lindi (asilimia 48),Mbeya (asilimia 45),Morogoro (asilimia 42),Rukwa(asilimia 40),Ruvuma
(asilimia 39),Mwanza (asilimia 37),Kagera (asilimia 36),Mtwara (asilimia 35), Manyara (asilimia34),
Pwani (asilimia 33),Tanga (asilimia
29)
, Arusha (asilimia 27),Kilimanjaro (asilimia 27),Kigoma (asilimia
26), Dar es Salaam (asilimia
19)
,na Iringa (asilimia 8).

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI INALETA SULUHU KWA WATOTO WAKIKE:

Katibu na muwakilishi wa baraza la
watoto la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutokea Zanzibar,
Abubakar  Koke anasema siku hii nimuhimu sana kwa
taifa la Tanzania, hii ndio siku maalumu ya kupaza sauti na kuidai haki ya
mtoto wakike ambae ndio mama wakesho, “
Ndoa
za utotoni zina madhara kiafya na kiuchumi serikali kupitia Wizara ya Katiba na
Sheria ikusanye maoni zaidi kutoka kwa watoto wenyewe nasio kama ilivyo sasa na
pia ifike hadi kwenye Mikoa ilio na idadi kubwa ya matukio ya Ndoa za utotoni”.

Nancy Kasembo
anasema sisi watoto kupitia baraza la watoto la Jmuhuri ya Muungano wa Tanzania
tunamatumaini kwamba kupitia siku ya wanawake duniani, viongozi wa majukwa yan
wanawake,mashirika ya kutetea haki za watoto wakike, Serikali na wadau mbali
mbali watapaza sauti juu ya kuhakikisha kwamba vifungu vya sharia ya ndoa
vinavyo ruhusu mtoto wakike kuolewa chini ya umri wa miaka 18, vinaondolewa.

Tunatamani kuona Serikali ikitenda haki
ya kufanyia maboresho ya vifungu vya Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971, na itekeleze
maamuzi ya mahaka kama ambavyo iliatoa hukumu dhidi ya kesi ya Rebeca Gyumi , Dr. Rose Reuben.

Kwa sababu kauli mbiu ya mwaka huu
inasema “Ubunifu na teknolojia ya usawa wa kijinsia” Taasisi ya
Msichana Initiative tunaihamasisha jamii kutumia majukwaa ya mtandaoni ya
kijamii kupaza sauti za watoto wakike, kama ambavyo sisi tunatumia mitandao
yetu ya kijamii njiamojawapo ya kuzungumza na watoa maamuzi juu ya maboresho ya
Sheria ya Ndoa.

Na, John Kabambala.

You Might Also Like

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi

Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili

Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania

KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.

UWEZO TANZANIA YARATIBU KIKAO CHA MIKAKATI YA KUWASHIRIKISHA WAZAZI UELIMISHAJI VIJANA STADI ZA MAISHA.

Tanzania Kids Time March 6, 2023
Share this Article
Facebook Twitter Email Print
Previous Article MIKUNDE CHANZO CHA LISHE BORA KWA MTOTO
Next Article RIPOTI YA ALiVE YAWASILISHWA KWA WAHARIRI NA WAWAKILISHI WA VYOMBO VYA HABARI
Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

Facebook Like
Twitter Follow
Youtube Subscribe
Telegram Follow
- Advertisement -
Ad image

Latest News

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
//

Tanzania Kids Time: A platform spotlighting children’s and women’s issues in Tanzania, focusing on education, health, and environmental conservation.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

© 2023 Tanzania Kids Time. Powered by Digital Media Innovation Program. All Rights Reserved.

Join Us!

Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..

Zero spam, Unsubscribe at any time.

Removed from reading list

Undo
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?