iliyowakutanisha Wahariri na wawakilishi wa vyombo vya Habari nchini Tanzania iliyoandaliwa na Shirikia la Gesci kutoka Nchini Kenya kwa kushirikiana na
Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation kutoka Zanzibar ilifanyika Jumamosi ya
tarehe 11 March 2023 katika Hoteli ya Double View iliyopo Kata ya Sinza Halmashauri
ya Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuitamburisha Ripoti ya
ALiVE kwa wanahabari, pamoja na kuutamburisha Mradi wa ADAPT.
Samson John
Sitta Mratibu wa Mradi wa ALiVE nchini Tanzania katika mahojiano baada ya
Warsha, ameiambia Tanzania Kids Time kwamba pamoja na lengo la Warsha hiyo ya
Siku moja kuwa ni kuitamburisha Ripoti ya Tathmini ya upimaji Stadi za maisha
na maadili kwa vijana (13 – 17) Afrika mashariki (ALiVE), lakini pia ilikua ni
kutoa taarifa ya utafiti kutoka katika Mradi mwingine wa ADAPT na kuwaeleza
wanahabari namna gani ripoti hizo zitatumika kufanya uchechemuzi katika Sera za
Nchi ili kuleta maboresho ya mitaala ya Elimu.
“Lengo la kukutana hapa
ilikua ni kuwapitisha wanahabari katika Ripoti yetu ya upimaji wa Stadi za maisha
kwa vijana wa umri wa miaka 13 – 17 Afrika mashariki, pamoja na hilo tulikua
tunawasilisha taarifa nyingine ya mradi mwingine wa ADAPT ambao ni Mradi Dada
wa ALiVE unaohakikisha baada ya utafiti na Ripoti kutoka ni kwa namna gani
matokeo yake yanaweza kutumika katika kufanya uchechemuzi katika Sera” Alisema Samson John Sitta, hii hapa ni sauti ya Samson John Sitta. https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1678775449–less-file-SAMSON-JOHN-SITT.mp3
Uzinduzi wa
Ripoti ya ALiVE ulifanyika jijini Dar es salaam mnamo Januari 26, 2023.
Mwandishi wa
Habari Hughes Dugilo kutoka Dar es salaam alikua miongoni mwa wanahabari
walioshiriki katika Warsha ya iliyoandaliwa na Shirika la Gesci, alishukuru na
kupongeza kwa jinsi miradi hiyo miwili inavyoshirikiana kutoa matokeo ya mahili
za Stadi za maisha na maadili kwa vijana wa Afrika ya mashariki na kuhakikisha
hatua zinachukuliwa kwa watunga Sera kisha Serikali kuchukua hatua ya kufanya
mabadiliko, lakini pia alieleza namna alivyo na wajibu katika kuhabarisha Jamii
kuhusu Stadi za maisha na maadili.
Mwandishi wa
Habari Hughes Dugilo alisema, “kwanza nipongeze miradi ya ALiVE na ADAPT,
leo tumeongeza ufahamu zaidi kuhusu Stadi za Maisha na Maadili, tukizungumzia
Stadi za maisha tunagusa maeneo mengi, masuala ya kujitambua, kujitegemea na
mimi kama Mwandishi wa Habari nina wajibu mkubwa sana baada ya Warsha hii,
kwanza kutekeleza majukumu yangu katika kuihabarisha Jamii kwa ujumla kuhusu
Stadi za maisha kwa vijana. Adhima ni kuona vijana wazitambua stadi za maisha,
wazisimamie na waziishi ili baadae waje kuwa watu wa kulisaidia Taifa letu” Sauti ya Hughes Dugilo.
JINSI MRADI WA ALiVE ULIVYOTOA RIPOTI
BARA NA VISIWANI.
Mradi wa
ALiVE ambao uko chini ya Taasisi Milele Zanzibar Foundation, ulifanya tathmini
yake ya upimaji Stadi za maisha na maadili kwa vijana Afrika mashariki kwanzia
Mwaka wa 2020 hadi 2022 upande wa Zanzibar na Tanzania Bara ili kuangalia
Mahili za Stadi za Maisha na Maadili waliyonayo vijana katika Halmashauri za
Wilaya 45 (Wilaya 11 kutokaTanzania visiwani na 34 za Tanzania Bara).
Mradi wa
upimaji Stadi za Maisha na Maadili kwa vijana wa umri wa miaka 13-17 uliofanywa
na Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation kutoka Zanzibar ulijikita kutafiti
Stadi za Maisha Tatu ambazo ni kujitambua, ushirikiano, utatuzi wa matatizo
pamoja na kutafiti Tunu (Maadili) ya Heshima, ambapo upande wa Zanzibar jumla
ya vijana wa kike na wakiume 2,447 wamehojiwa katika Kaya 1,942.
Upande wa
Tanzania Bara Mradi wa ALiVE umewafikia vijana 14,645 katika Kaya 11,802.
KWA NINI MRADI WA ADAPT KUTOKA
SHIRIKA LA GESCI UNAHUSIKA.
Kwa mujibu
wa Ramadhani Matimbwa Mratibu wa Mradi wa ADAPT Kutoka Shirika la GESCI la
nchini Kenya, Mradi wa ADAPT ambao kirefu chake ni (Adapting of Assesment into
Policy and Learning) mradi ambao umejikita kufuatilia hatua kwa hatua namna
matokeo ya tafiti yanavyoweza kutumika vyema katika kufanya uchechemuzi kwa
watunga Sera na kuleta mabadiliko chanya ya tafiti hizo.
“ADAPT Pia inajaribu
kuchechemua tafiti za ALiVE namna tunavyojenga uwezo wetu sisi ni kwa kujadili
hizi tafiti mbalimbali, tunawaita watu kwa pamoja tunawaeleza kile
tunachokiamini ili kwa pamoja tukielewana mnaweza kujenga jambo Fulani lakini
pia tunavyokutana na wahariri na wanahabari kwetu inatusaidia kufikisha taarifa
hizi kwa Jamii na Serikali kwa sababu ADAPT lengio lake kubwa ni kufanya
mabadiliko, sasa mabadiliko yale huwa yaanzia kwenye mijadala” Alisema Ramadhani Matimbwa, na hii hapa ni sauti yake. https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1678776231–less-file-RAMADHANI-MATIMBW.mp3
Soma zaidi
kuhusu GESCI inayotekeleza Mradi wa ADAPT: Home
– The Global e-Schools and Communities Initiative (GESCI)
MFANO WA YALIYOMO KATIKA RIPOTI YA
ALiVE TANZANIA VISIWANI.
Kutoka
katika ukurasa wa Tano wa Ripoti ya ALiVE Zanzibar kipengele cha Stadi ya
Maisha ya “UTATUZI WA MATATIZO” Ripoti imebainisha 23% ya vijana wanapata
wakati mgumu kutambua tatizo au asili yake kimtazamo na kwa hivyo hawawezi
kutambua suluhisho lake.
Asilimia 48%
ya vijana wanauwezo wa kutambua uwepo wa tatizo kutoka kwa mtu kimtazamo na
kuchukua hatua ili kutambua uwezekano wa kupata suluhisho, 15% ya vijana
wanauwezo wa kutambua uwepo wa tatizo kutoka kwa mtu kimtazamo, kutambua njia
kuu za kutatua tatizo na kuweza kusuluhisha.
Lakini pia
Ripoti imesema 14% ya vijana wanauwezo wa kutambua uwepo wa tatizo kutoka
kwenye mitazamo mingi, kuwa na njia nyingi za suluhisho na kuchagua njia ipi
inaweza kutumika kutatau tatizo.
SHIRIKA LA RELI LILIVYOFANIKISHA
KUPATIKANA KWA MIRADI YA ALiVE NA ADAPT
Mtandao wa
Elimu Afrika Mashariki unaofahamika kwa jina la RELI, (Regional Education
Learning Initiative in East Africa) unafanya kazi katika Nchi Tatu za Afrika ya
Mashariki ambazo ni Kenya, Uganda na Tanzania ambao hadi sasa una zaidi ya
wanachama 70 ambao ni mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali kwa lengo la
kuhakikisha ujifunzaji jumuishi kwa watoto wote katika Afrika Mashariki.
Mradi wa
ALiVE unaotekelezwa na Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation umetoka katika
Kongani ya Stadi za Maisha na maadili ikiwa ni moja ya Kongani Nne zilizopo
katika Mtandao wa RELI.
Mradi wa
ADAPT unaotekelezwa na Shirika la Gesci kutoka nchini Kenya nao pia unatoka
katika Kongani ya Stadi za Maisha na Maadili kwa lengo la kuleta mabadiliko
kupitia ufuatiliaji wa matokeo ya tafiti mbalimbali na kuona kwa namna gani
watunga sera wanaweza kuleta mabadiliko.
Ifahamu kwa
undani RELI: RELI – Regional Education
Learning Initiative in East Africa (reliafrica.org)
Na Hamad Rashid