wakati uwiano kati ya urefu na umri vinakuwa chini kwa vigezo vya ukuaji
vilivyowekwa na shirika la afya duniani. kwa jina jingine udumavu unaweza
kuelezewa kuwa ni udhaifu wa ukuaji wa mwili na maendeleo ya ukuaji wa mtoto
unaotokea kwa mtoto kutokana na lishe duni, kuugua mara kwa mara na kukosa
msisimuo wa kisaikolojia na kijamii.
Kwa mujibu wa ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi
na Mtoto na Viashiria Vya Malaria Tanzania wa Mwaka 2022, na Viashiria vya Hali ya Lishe inaonesha
kwamba kiwango cha Udumavu kwa watoto chini ya umri wa miaka 5, Tanzania inaendelea kushuka japo haijafikia lengo la asilimia 28 kama ambavyo ilidhaniwa kufikia mwaka 2021, Chati ifuatayo inaonesha zaidi hapa chini.
Kwa mujibu wa baraza la afya Duniani kupitia Muongozo wake wa Malengo
ya Lishe ifikapo mwaka 2025, ulio andandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)
Serikali ya Tanzania,Shirika la Save the Children na Panita, unaonesha malengo
waliojiwekea ifikapo mwaka 2025 Tanzania
iweimepunguza idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano waliodumaa kwa asilimia 40, kupunguza kiwango cha tatizo la upungufu wa damu miongoni mwa wanawake walio katika umri wa uzazi
kwa asilimia 50, kupunguza
kiwango cha tatizo la watoto kuzaliwa wakiwa na uzito pungufu kwa asilimia 30.
Aidha kuongeza kiwango cha unyonyeshaji watoto maziwa ya
mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo kwa angalao asilimia 50 pamoja kupunguza tatizo la
ukondefu kwa watoto na kulidhibiti libakie chini ya asilimia 5.
HALI YA UDUMAVU ILIVYO SASA NGAZI YA KITAIFA:
Ripoti hiyo ya Viashiria vya Hali ya Lishe imebainisha kwamba, Uzito Pungufu kwa watoto
chini ya miaka 5 umepungua, Ukondefu umepungua, Uzito pungufu sana umeendelea kubaki
katika asilimia ileile kama ilivyo kuwa kwenye utafiti wa mwaka 2015/16, kama
chati inavyo onyesha hapa chini.
Aidha Mikoa inayo ongoza kwa Udumavu Watoto
chini ya miaka 5 imetajwa kuwa Mkoa wa kwanza ni Iringa una asilimia 56.9%, wapili ni Mkoa wa Njombe una asilimia
50.4% na watatu ni Mkoa wa Rukwa una
asilimia 49.8%.
SABABU ZA UDUMAVU KWA
WATOTO NI NINI?
Kwa mujibu wa Afisa lishe Manispaa ya Morogoro bi, Jacqueline Mashurano amesema hali ya udumavu kwa watoto imepungua kwa kiasi kikubwa, kwani suala la
lishe linagusa mambo mengi katika familia ikiwemo, uchumi, uelewa wa wazazi na
jamii kwa ujumla, jambo linalo sababisha kuona mabadiliko kidogo kidogo kwenye
eneo hili la Lishe kama chati inavyo onesha hapa chini.
Ulaji duni wa chakula kwa muda mrefu,
Magonjwa ya mara kwa mara, Utapiamlo wakati wa ujauzito na Upungufu wa nishati,
Tatizo hili la lishe husababishwa na kina mama kutopata mlo kamili
wakati wa ujauzito.
Tunaamini siku 1000 za kwanza
wakati wa ujauzito ndicho kipindi ambacho uumbaji unafanyika, hivyo katika
kipindi hicho mama akikosa kupata mlo kamili hupelekea mtoto kudumaa akiwa
tumboni mwa mama yake.
Lishe duni na kuugua mara kwa mara katika
kipindi cha siku 1000 za mwanzo za maisha ya mtoto, Taratibu duni za ulishaji watoto wachanga na
wadogo, ikiwemo watoto kutonyonyeshwa maziwa ya mama pekee katika miezi sita ya
mwanzo baada ya kuzaliwa, na kupewa chakula cha nyongeza kisichokidhi mahitaji
yao kilishe pale wanapotimiza umri wa miezi sita.
Hii
inamaanisha kupewa kiasi kidogo cha chakula, kupewa chakula kisichokuwa na
ubora, na kutopewa chakula chenye mchanganyiko wa makundi mbalimbali ya
vyakula, Afya na lishe duni ya wanawake
kabla ya ujauzito, wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua. Wanawake kuwa na
kimo kifupi, kutopangilia uzazi na hivyo kuzaa karibu karibu; na tatizo la
wasichana kupata mimba wakiwa katika umri mdogo.
Madhara ya yatokanayo na Lishe
duni ni yapi?
Mtoto kudumaa kimwili, hali ya mtoto
ambayo hupelekea mwonekano wake wa kimwili kuwa tofauti na umri wake, unaweza
kukuta mtoto anamiaka mingi lakini umbo lake linakua dogo au anakua mfupi,
kitaalam urefu unatakiwa kwenda sambamba na umri. Mtoto kuwa na uwezo hafifu wa
uwelewa na utambuzi wa mambo, hali hii hupelekea kuwa na wimbi la watoto
mashuleni wasiofundishika.
Letisia
Mwangaja mzaliwa wa Mbeya kwa sasa anaishi
kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro anasema
amesimulia hali ya lishe ilivyo sababisha mdogowake kuwa na tumbo kubwa kuliko
kawaida; “Nyumbani kwetu Mbeya mdogo wangu alikuwa na tumbo kubwa miguu na mikono
myembamba, baada ya kumpeleka kituo cha afya daktari akasema anatatizo la lishe,
kwa kumlisha chakula zaidi ya umri wake.
Ukiangalia nikweli kwa sababu mama
yetu alikuwa akimuachia chakula kilicho baki jana, anamwambia utakula yeye
anaenda shambani wakati huo mimi ninaenda shuleni kurudi nyumbani mama hadi saa
kumi jioni ndio anafika anapika mtoto anashindia kipolo” amesema Letisia Mwangaja.
SULUHISHO
LAKE NI LIPI?
Bi. Jacqueline
Mashurano
amesema wanaa mikakati ya kufikia asilimia 25 ifikapo mwaka 2025, katika kutatua
changamoto ya Udumavu kwa kutoa Elimu kuhusu utumiaji wa vyakula kwa watoto,
huku akibainisha kuwa Mkoa wa Morogoro una vyakula vingi vya aina tofauti
tatizo ni Elimu ya namna ya kupangilia kutumia vyakula hivyo eneo ambalo linatakiwa
kuwekewa mkazo zaidi kwa kushirikiana na afisa Kilimo,afisa Mazingira na afisa
Afya.
Jambo hili linatakiwa kuanza hata kabla wanawake
hawajawa wajawazito, ni muhimu kusimamia hali ya lishe ya wanawake katika umri wakuzaa
ili watakapo kuwa wajawazito wawezeshe kukuwa vyema kwa kiumbe kinacho kuja.
Siku1000 niza Msingi Sana katika
kuzuia utapiamlo unao pelekea Udumavu kwa watoto, Siku1000 zinajumuisha siku 270
za ujauzito, siku 730 za mtoto
katika miaka miwili ya mwanzo, Udumavu unaotokea
na kutorekebishwa katika siku1000 za
kwanza hauta weza kurekebishwa tena, amesema Letisia
Mwangaja.
Na, John Kabambala-Morogoro.