SURUA NI
NINI?: Surua ni ugonjwa hatari sana unaoambukiza unaosababishwa na virusi, kabla
ya kuanzishwa kwa chanjo ya surua mwaka wa 1963, magonjwa makubwa ya mlipuko
yalitokea takriban kila baada ya miaka 2-3 na Surua ilisababisha wastani wa
vifo milioni 2.6 kila mwaka.
Zaidi ya
watu 140,000 walikufa kutokana na surua mwaka 2018 – wengi wao wakiwa watoto
walio chini ya umri wa miaka 5, licha ya kuwepo kwa chanjo salama na yenye
ufanisi.
SASA HALI
IKOJE KUHUSU CHANJO YA SURUA?
mahojiano maalumu na mtaalamu wa chanjo kutoka Manispaa ya Morogoro Dr.Philipo Bwisso amesema,
Surua husababishwa na virusi kwa kawaida hupitishwa kupitia mguso wa moja kwa
moja na kupitia hewa, Virusi huambukiza kwa njia ya upumuaji, kisha huenea
mwilini, Surua ni ugonjwa wa binadamu na haujulikani kutokea kwa wanyama.
DALILI ZA UGONJWA WA SURUA NI ZIPI?
Nimezungumza
na Dr.Philipo Bwisso mtaalamu na Mratibu wa Chanjo
kutoka Manispaa ya Morogoro amesema, miongoni mwa dalili za ugonjwa wa surua ni
kama vile homa kali, ambayo huanza siku 10 hadi 12 baada ya kuambukizwa na
virusi, na huchukua siku 4 hadi 7, kikohozi, baada ya siku kadhaa hupata upele,
na huendelea kwa siku 5 hadi 6, na kisha huisha. Vifo vingi vinavyohusiana na
surua husababishwa na matatizo yanayohusiana na ugonjwa huo, matatizo makubwa
hutokea zaidi kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5, au watu wazima zaidi
ya umri wa miaka 30.
KUNA MATATIZO
YEYOTE HUMPATA MGONJWA WA SURUA?
Matatizo
makubwa zaidi ni upofu, maambukizi ambayo husababisha uvimbe wa ubongo, kuhara na
upungufu wa maji mwilini, magonjwa ya kuambukiza kama vile pneumonia, Surua ina
uwezekano mkubwa wa kuwapata watoto wadogo wenye lishe duni, hasa wale walio na
upungufu wa vitamini A, au ambao kinga zao zimedhoofika kutokana na VVU/UKIMWI
au magonjwa mengine.
NANI YUKO HATARINI?
Dr. Philipo Bwisso anabainisha zaidi kuwa ni Watoto wadogo ambao hawajachanjwa wako
katika hatari kubwa zaidi ya surua na matatizo yake, ikiwa ni pamoja na kifo,
Wanawake wajawazito ambao hawajachanjwa pia wako katika hatari, Mtu yeyote
asiye na kinga (ambaye hajachanjwa au hajapata chanjo lakini hakupata kinga)
anaweza kuambukizwa.
Surua
inaendelea kutokea hasa katika nchi nyingi za Afrika na Asia, ambapo idadi
kubwa (zaidi ya 95%) ya vifo vya surua hutokea katika nchi zenye kipato cha
chini kwa kila mtu na miundombinu dhaifu ya afya.
Sophia Mgeta ni mkaazi wa
kijiji cha Dumila katika halimasahauri ya Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro na
ni baba wa watoto wawili, amenieleza namna alivyo anza kuona dalili za ugonjwa
wa Surua kwa mtoto wake, “Tulianza kuona mtoto wetu mkubwa anapata homa kasha upele
ulio samba mwili mzima jambo ambalo lilinisababisha nimpeleke kwenye kituo cha
afya cha Roma kilichopo hapa Dumila.
Baada ya
kfika huko daktari alivyo mpima na kumpatia huduma akatuuliza huyu mtoto wenu
aliwahi kupewa chanjo ya Surua ? Tukamjibu hakuwahi kuchomwa sindano ya Surua,
alitwambia kuwa mtoto ameugua ugonjwa wa Surua kwa sababu hajawahi kupata
chanjo ya Surua, hivyo nimuhi sana na nilazima mtoto apewe chanjo ya Surua
hatua kwa hatua”Alisema Sophia Mgeta
SURUA
INAAMBUKIZAJE?
Chapisho la
WHO limebainisha kwamba, Surua ni mojawapo ya magonjwa yanayoambukiza zaidi
duniani. Huenezwa kwa kukohoa na kupiga chafya, kugusana kwa karibu kibinafsi
au kugusana moja kwa moja na ute ulioambukizwa wa pua au koo.
Virusi
hubaki hai na huambukiza hewani au kwenye nyuso zilizoambukizwa kwa hadi saa 2.
Inaweza kuambukizwa na mtu aliyeambukizwa kutoka siku 4 kabla ya kuanza kwa
upele hadi siku 4 baada ya kutokea kwa upele.
Milipuko ya
surua inaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko ambayo husababisha vifo vingi,
haswa kwa watoto wachanga, wenye utapiamlo, katika nchi ambazo ugonjwa wa surua
umeondolewa kwa kiasi kikubwa, visa vinavyoagizwa kutoka nchi nyingine
vinasalia kuwa chanzo muhimu cha maambukizi.
KUPITIA CHANJO YA
SURUA KUNA MATAKEO YEYOTE?
Kwa mujibu
wa chapisho hilo lililo chapishwa Mwezi March, 2023, na Shirika la Afya Duniani
(WHO) kanda ya Afrika inaonesha kwamba, linasema Chanjo ya Surua imekuwa na matokeo
chanya katika kupunguza vifo vya surua, kama chati inavyo onesha hapa.
MATIBABU YAKE NI
YAPI? Milipuko ya
ugonjwa surua inaweza kupunguzwa kupitia huduma ya ambayo inahakikisha lishe
bora, unywaji wa maji ya kutosha na matibabu ya upungufu wa maji mwilini unaopendekezwa
na WHO, Suluhisho hili linachukua nafasi ya maji na vipengele vingine muhimu
vinavyopotea kwa njia ya kuhara au kutapika.
Watoto wote
waliogunduliwa na surua wanapaswa kupokea dozi mbili za virutubisho vya
vitamini A, wakipewa muda wa saa 24 tofauti, matibabu haya hurejesha viwango
vya chini vya vitamini A wakati wa surua ambayo hutokea hata kwa watoto walio
na lishe bora na inaweza kusaidia kuzuia uharibifu wa macho na upofu,
Virutubisho vya vitamini A pia vimeonyeshwa kupunguza idadi ya vifo vya surua.
NJIA GANI YAWEZA
KUTUMIKA ILI KUZUIA UGONJWA WA SURUA?
Dr. Philipo Bwisso anasema wazazi au walezi wa watoto hawapaswi kabisa kuacha kuwapeleka
watoto kiliniki ilikupatiwa chanjo ya Surua, tena kwa dozi kamili ikiwa
nipamoja na kukamilisha chanjo zingine zinazotolewa kwa ajili ya kumkinga mtoto
dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Sita sahau
jinsi ambavyo mtoto wetu alivyo tusumbua wakati wote nikulia tu, Nawashauri
ndugu, jamaa, marafiki na wazazi walio na watoto au ambao wanatarajia kupata
watato nimuhimu kuzingatia chanjo kzote zinazowahusu watoto, tuwapeleke kwenye
vituo vya afya ilikulinda afya zao,alisema Sophia
Mgeta
Na, John
Kabambala-Morogoro.