linalo husika na masuala ya wanawake UN Women, linasema kuozeshwa mtoto wakike
chini ya umri wa miaka 18, huu ni
ukatili, Taarifa iliochapishwa kwenye wavuti
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake,Mwishoni
mwaka mwaka wa 2022, UN Women inasema
dharura duniani, majanga, mizozo, na vita vinazidi kuongeza ukatili dhidi ya
wanawake na wasichana na kuchochea visababishi na hatari zaidi.
HALI YA UKATILI DHIDI YA
WATOTO IKOJE SASA:
Ofisi ya Ustawi wa Jamii Mkoa
wa Morogoro imeonesha kwamba hali ya ukatili dhidi ya Watoto unarudisha nyumba
maendeleo na mipango ya Mkoa huo, kulingana na kwamba jamii ya walio wengi
wanaendelea kukumbatia utamaduni na desturi za kizamani kwa baadhi ya
halmashauri za Wilaya.
Katika taarifa hiyo kutoka
Ofisi ya ustawi wa jamii Mkoa wa Morogoro, Bi, Jesca Kagunila ambae ni Afisa Ustawi
wa Jamii amebaina halmashauri ambazo zimekuwa na matukio mengi zaidi kwa
kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka 2022.
Hata hivyo ukatili mwingine
ulio ongoza zaidi ni ukatili wa mimba za utotoni, na halmashauri ilio ongoza
kuwa na matukio mengi yalio ripotiwa ni halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ambayo
inajumla ya matukio 1870 ya ndoa za utotoni kwa kipindi ya mwaka 2022.
HALI
YA UKATILI KWA WATOTO MOROGORO ILIKUAJE KABLA?
NINI CHANZO HASA CHA UKATILI HUU KWA WATOTO?
Aziza Juma ni mkaazi
wa kata ya changalawe katika halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, amesema
changamoto za wazazi nichanzo kikubwa cha watoto kufanyiwa ukatili mbali mbali
ukiwemo ukatili wa Kingono yaani kubakwa
na kulawitiwa, kutokana na kukosekana kwa utulivu wa familia.
“Nimewahi kukutana na mtoto mmoja wa
kike, mwenye umri wa miaka 12 alie kuwa amevimba usoni baada ya
kuzungumza nae akanieleza juu ya kisa kilicho mtokea hadi kupata makovu hayo na
uvimbe, aliniambia kwamba baba wakufikia alikuwa akimpiga mama yangu mzazi hadi
kupoteza fahamu.
Nilipo muomba ache kumpiga akanigeukia
kuanza kunipiga mimi, baadae akaniambia kama unataka nisikupige tushiriki tendo
la ndoa, nilipo kataa na kupiga kelele sana watu wengine wakasikia ndipo kuja
ndani wakati huo yeye akawa ameshakimbia” alisema Aziza Juma.
Chapisho lililo chapishwa na Shirika
la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake linasema, Mabadiliko ya
tabianchi yanachochea aina zote za ukatili dhidi ya wanawake na wasichana na
tayari kuna mwenendo ulio dhahiri ambao unazidi kupanuka kadri janga la
tabianchi linavyozidi kuwa baya, kasi ya maendeleo ya teknolojia nayo yanaongeza
ukatili wa wanawake na wasichana kupitia mtandaoni na kuibua vitisho vipya
dhidi ya haki za makundi hayo.
Bi,
Kagunila anasema, ukatili dhidi ya watoto hujitokeza katika njia
tofauti tofauti inaweza kuwa kimwili, kingono au kifikra, Inaweza kufanyika
mbele za watu, faraghani au mtandaoni na kutekelezwa na ndugu au mtu mwingine
yoyote bila kujali unafanyika vipi, wapi na umetekelezwa na nani au ni kwa sababu
gani? Ukatili dhidi ya watoto una madhara makubwa ya muda mfupi au muda mrefu ambao
huzuia ushiriki wao kikamilifu kwenye jamii zao.
“Watumishi wa Serikali
wanapaswa kujitafakari sana katika nafasi zao, kwa sababu ukiangalia matukio
mengi unakuta yanafanyika hapa Manispaa ambako ndipo makao makuu ya taasisi
zote za Serikali, kwa ngazi ya Mkoa kwa nini yasizibitiwe? Kiongozi unapo ona
njia hii haieleweki kwa jamii kuleta matokeo chanya unayo yataka ni lazima
utafute mbinu nyingine ya kukabiliana na changamo hizo”.
“Kwanini wakati mwingine
viongozi tusivae sura za kiuchunguzi, ilikubaini mambo yanayo tendeka kwenye
eneo lako la kazi ? mfano kila robo unakuwa na takwimu zinazo onesha watoto
wamelawitiwa, wamebakwa na bahati nzuri nikwamba watoa taarifa maranyingi
husema pia mazingira ambayo tukio/matukio hayo yamefanyika, viongozi niwakati
wakujitafakari zaidi juu ya nafasi zao walizo nazo ilikuleta mabadiliko chanya
katika taifa na kuwalinda watoto” amesema Josia Amosi, Sio jinalake halisi.
Ukatili dhidi ya Watoto kwa
kipindi cha mwezi Oktoba- Disemba, 2022 takwimu zinaonesha kwamba Manispaa ya
Morogoro imeongoza kwa aina mbili za ukatili kwa watoto, kama ambavyo chati
inaonesha hapa.
KIPI KIFANYIKE SASA?
Kila mmoja kwenye jamii
anapaswa kuwa mlinzi wa familia na jamii yake, kila anapo muona mtoto fikra
moyoni imuijie ikimwambia huyu nimwanangu, hivyo hakuna mazazi mwenye utimamu
anaweza kuruhusu na kumuacha mwanae atendewe ukatili yakupasa kukemea ukatili
na unyanyasaji wa kijinsia, amesema
Josia Amosi, Sio jinalake halisi.
Aziza Juma anaishauri Jamii ipaze sauti sasa ilikuokoa watoto wanaokumbwa na ukatili, hii ina maana maeneo
ya hifadhi, majumbani, Shuleni, njiani namaeneo mengine ambako mtoto aweza
kufanyiwa ukatili, namba za simu za kutoa taarifa wakati wowote za paswa kuwa
kila pahara, ushauri nasaha na aina zozote za usaidizi ambao manusura wa
ukatili wanahitaji.
Kila mwaka, kampeni ya siku 16 ya
kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake husaka hatua za pamoja za kimataifa
kutokomeza aina zote za ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Ni muda muafaka
sasa wa kuungana katika kutokomeza hali ya ukatili kwa watoto.
Na, John Kabambala-Morogoro.