UTANGULIZI:
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba
(TMDA) ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yenye jukumu la kudhibiti ubora, usalama na
ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.
Taifa
linapaswa kulindwa na miongoni mwa vitumuhimu ni matumizi ya madawa na vifaa
tiba na vitendanishi vinavyo tumika kwa watoto, watoto watakapo pewa au kutumia bidhaa hii ya dawa pasipo
kuthibitishwa na mamlaka husika matokeo yake kizazi hicho kunahatari ya
kuteketea, hivyo basi ndiomaana, mwaka 2018, TMDA ilifanya ukaguzi wa viwanda
vya kusindika vyakula vya nyongeza na maziwa ya watoto wachanga vilivyopo nje
ya nchi ili kujilidhisha kabla ya kuruhusiwa kuingiza sokoni.
KULINDA AFYA ZA WATOTO:
TMDA hupokea maombi ya usajili wa
vifaa tiba nchini vikiwemo vinavyotumika kwa watoto kutoka kwa wadau mbalimbali
walioko ndani na nje ya nchi, Baada ya kupokea maombi hufanya tathmini ya
taarifa za ubora, usalama na ufanisi wa Vifaa tiba vilivyowasilishwa na pale
inaporidhika na tathmini husika ya vifaa hivyo husajiliwa.
wa sampuli katika maabara.
Maabara ya TMDA hupima sampuli za
vifaa tiba kwa lengo la kuhakiki ubora, usalama na ufanisi wake kabla na
baada ya kuruhusiwa kuingia katika soko, Pale inapobainika kwamba kifaa tiba
hakikidhi viwango vya usalama, ubora na ufanisi hakipewi usajili na kama kipo
sokoni matumizi yake husitishwa na kuondolewa.
uingizaji na usafirishaji nje ya nchi.
TMDA hudhibiti uingizaji nchini
wa vifaa tiba na Dawa kwa kuwataka waagizaji kuomba kibali cha kuingiza
vifaa tiba nchini na kufanya ukaguzi kwenye vituo vya forodha
kuhakiki kama waagizaji wamezingatia taratibu za uingizaji vifaa tiba.
katika soko na vituo vya forodha.
TMDA hufanya ukaguzi katika vituo
vya forodha, maeneo ya biashara ikiwa ni pamoja na maduka, maghala na vituo vya
kutolea huduma za afya kwa nia ya kuhakiki usalama, ubora na ufanisi wa vifaa
tiba na Dawa, Pale inapobainika kwamba kuna ukiukwaji wa sheria, kanuni na
taratibu, Mamlaka huchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa onyo,
kusitisha kwa muda matumizi ya kifaa tiba hadi marekebisho yafanyike au kufuta
usajili wa kifaa tiba kufikisha mtuhumiwa mahakamani pale inapolazimu.
Maeneo ambayo huleta changamoto
kubwa kwa jamii ni maduka ya dawa
muhimu, baadhi yao huuza dawa na vifaa tiba vilivyo isha muda wake kwa baadhi
yao, kwa nini hutokea hali hii? Je, ni njiagani hutumika kuhifadhi dawa na
vifaa tiba kwenye maduka ya dawa? Nimetembelea moja kati ya maduka ya kuuza dawa
muhimu Marhaba farmasi iliopo Mkoani Morogoro, na nimefanya mahojiano na Kelvin Magonda huyu ni mfamasia
sikiliza mahojiano hayo….https://appfasta.com/tkt/cms/
CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI TMDA KULINDA AFYA ZA WATOTO
Mkuu wa Mawasiliano kutoka TMDA Bi, Gaudensia Simwanza
amebainisha changamoto mojawapo kwa
jamii ni ununuzi holela na kutumia dawa bila kufanyiwa uchunguzi au kuelekezwa
na daktari, kutumia vijiuasumu kutibu magonjwa yanayotokana na virusi (viral
infections) kutumia dozi isiyosahihi au kushindwa kumaliza dozi, kutumia dawa
zinazoingiliana
kiutendaji kwa pamoja, kwa mfano tetracycline
na Magnesium kutumia dawa na pombe. Jambo linguine
kubwa ununuzi wa dawa au kifaa tiba kilicho maliza muda wake wa matumizi, na
kushindwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika kama vile TMDA.
ELIMU GANI HUTOLEWA NA TMDA KWA JAMII?
Elimu inayo tolewa na TMDA ni kuhusu
matumizi sahihi ya bidhaa kupitia shule za sekondari na msingi, makundi
mbalimbali ya wananchi na vikundi vya wajasiriamali, Lengo la elimu hiyo ni
kuimarisha udhibiti wa sekta hiyo ili kuhakilisha kuwa huduma za usambazaji na
uuzaji wa dawa, vifaa tiba na
vitendanishi inatolewa bila kuathiri usalama wa chakula na kusababisha madhara
ya kiafya kwa walaji.
uelewa kwawatumiaji wa bidhaa zinazodhibitiwa na TMDA na wananchi kwa
ujumla katika matumizi sahihi ya bidhaa na kuongeza utii wa Sheria bila
shuruti.
athari zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi.
ubora, usalama, na ufanisi wa dawa, Vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa nyingine
za afya kwa wote.
bora za udhibiti katika kulinda afya ya jamii na mazingira kwa kutumia
wafanyakazi wenye ujuzi na ari ya kazi.
Ili kuepuka au kupunguza kutokea
usugu wa bakteria unashauriwa kutumia dawa kwa usahihi, Usinunue vijiuasumu
kiholela, Usinunue vijiuasumu bila cheti cha Daktari, Hakikisha unafahamu
matumizi sahihi ya dawa ulizopewa kabla ya kurudi nyumbani toka kituo cha afya
au duka la dawa na Tumia dozi sahihi kwa kipindi.
waagizaji na wauzaji wa vifaa tiba kufuata taratibu na kujihakikishia ubora,
usalama na ufanisi wa vifaa tiba wanavyonuia kuviuza kwenye soko la Tanzania
kabla ya kukaguliwa na kuhakikiwa na Mamlaka, hii itarahisisha udhibiti wa
vifaa tiba nchini na kuongeza imani ya watumiaji na wananchi kwa bidhaa
zinazouzwa.
taarifa TMDA au kituo chochote cha afya inapobaini ukiukwaji wa taratibu za
utengenezaji, usambazaji, uuzaji na matumizi yasiyo sahihi ya vifaa tiba ili
mwisho wa yote lengo la Serikali la kulinda afya ya wananchi wakiwemo watoto liwezekutimia.
Na, John Kabambala-Morogoro.