By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
Tanzania Kids Time
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Mazingira
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Wasiliana Nasi
Reading: ATHARI ZA ADHABU ZA VIBOKO SHULENI
Share
Notification Show More
Latest News
Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
TANZANIA WILL HOST CIGOFA4 TO FIND CONCRETE SOLUTIONS FOR YOUTH LAND QUESTIONS
Editor's Pick
Aa
Aa
Tanzania Kids Time
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi
  • Contact
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Tanzania Kids Time > Blog > Elimu > ATHARI ZA ADHABU ZA VIBOKO SHULENI
Elimu

ATHARI ZA ADHABU ZA VIBOKO SHULENI

Tanzania Kids Time
Last updated: 2024/01/29 at 2:30 PM
By Tanzania Kids Time 9 Min Read
Share
SHARE

 

VISA JUU YA ADHABU YA VIBOKO KWA WANAFUNZI SHULENI.

Na, John Kabambala-Morogoro. Mwezi September hautasahaulika
kamwe kwenye familia ya
 Eradius, uchungu, simanzi, vilio, masikitiko
na huzuni vilitawala katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera vikitokea katika
Shule ya Msingi Kibeta, halikuwahi kutokea kabala tukio kama hili na hapakuwa
na mwenye uzoefu na kifo kitokanacho na
adhabu ya viboko Shuleni, sio tu
kwenye familia hiyo! Ila hata kwa jamii na walio kuwa wanafunzi wenzake.

Kwa muda mrefu kumekuwa na
matukio mbali mbali ya athari ya viboko kwa wanafunzi mashuleni kama vile
kuvunjwa mikono, kuachwa na makovu hadi vifo, miongoni kati ya matukio yalio
sikitisha zaidi ni lile la kifo cha mwanafunzi
Sperius Eradius wa Shule ya Msingi Kibeta, Manispaa ya Bukoba Mkoani
Kagera, tukio hili lililotokea Mwezi September Mwaka
2018, kifo kilichotokana na adhabu ya viboko aliyopata kutoka kwa
mwalimu tena akiwa shuleni.

Vivyo hivyo tukio jingine
linalo husishwa na adhabu ya viboko ni la
Mwanaidi
Ally
,  mwanafunzi wakike aliekuwa
akisoma kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari
Saba saba iliopo Mkoani Mtwara,
Mwanafunzi huyo alikuwa na umri wa miaka kumi nasita (
16), kifo cha mwanafunzi huyo kilitokea mwezi Desemba Mwaka 2022, ambapo uhai na ndoto zake
zikazima ghafla kama mwanga wa umeme unavyo katika ghafla bila taarifa, hayo ni
baadhi ya matukio ya vifo kwa wanafunzi yalio husisha adhabu ya viboko.

 MWONGOZO NA KANUNI  ZA ADHABU YA VIBOKO SHULENI INASEMAJE?

Mwongozo wa kutoa adhabu
mashuleni chini ya kifungu cha 61 (1) (v) cha Sheria ya Elimu sura ya
353 marejeo ya mwaka 2002 ambao unampa
mamlaka Waziri wa Elimu kutunga kanuni za Masuala mbalimbali zitakazokidhi
utekelezaji wa masuala ya Sheria hiyo.

Miongoni mwa kanuni
zilizotungwa ni pamoja na
The Education
(Corporal Punishment) Regulation G. N. 294 ya mwaka 2002.
Kanuni hizi
zinatoa mwongozo, ni wakati gani adhabu ya viboko inatakiwa kutolewa na kwa
kiwango gani.

“Kanuni ya 3 (1) inasema adhabu ya viboko itatolewa iwapo patatokea utovu
mkubwa wa nidhamu au kosa kubwa litakalofanywa ndani au nje ya shule ambalo
litaishushia shule heshima. Kanuni ndogo ya (2) inasema adhabu ya Viboko
itatolewa kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi na isizidi viboko
vinne (4) kwa tukio lolote
.
”

 

Sheria
imempa mwalimu mkuu wa shule husika mamlaka ya kutoa adhabu ya viboko au
kukasimisha mamlaka yake kwa umakini mkubwa kwa mwalimu yeyote kutoa
adhabu hiyo, Mwalimu anayechaguliwa kutoa adhabu atakua na mamlaka ya kutoa
adhabu pale tu atakapopata idhini ya mwalimu mkuu katika tukio husika.

Kanuni
ya (5) inataka kila adhabu ya Viboko inayotolewa kwa mwanafunzi kumbukumbu ya
kutolewa kwa adhabu hiyo sharti iwekwe kwenye kitabu yaani (
Kumbu kumbu),
ikitaja jina la mwanafunzi, kosa alilolifanya, idadi ya viboko na jina la
mwalimu aliyetoa adhabu na kumbukumbu hizo lazima zisainiwe na Mkuu wa shule.

LENGO LA  STORI HII NI NINI?

 

Ni, kuikumbusha Serikali kupitia Wizara ya Elimu
kusimamia ipasavyo mwongozo wa Adhabu Shuleni, kupitia kanuni ya 3 (1) na
Kanuni ndogo ya (2) ya adhabu,  kwani ukweli
usiofichika ni kwamba, mwongozo wa adhabu hii tajwa hapo juu hutekelezwa
kinyume cha kanuni zilizowekwa aidha kwa kutokujua au kwa kujua ila kwa
kupuuzia.

KWA NINI ADHABU YA VIBOKO SHULENI IENDELEE?

Kwa utamaduni ulio jengeka nchini Tanzania kataka
malezi ya mtoto nilazima viboko vipewe kipaumbele, suala hili hufanyika kwenye
jamii mbalimbali kwa lengo la kumbadilisha mtu mwenye tabia zisizo faa Shule, kwenye
familia, jamii,  baadhi ya Walimu
wanaunga mkono kuwa adhabu ya viboko iendelee kutolewa Shuleni kwa sababu zipi?
Mwalimu Paschal Martine kutoka Shule
ya Sekondari Kisemwa iliopo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini Mkoa wa
Morogoro aliniambia…Sauti…
https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1682245483–less-file-Paschal-Martin.mp3 

ADHABU YA VIBOKO SHULENI 
SIO TIBA KWA WENYE TABIA MBAYA:

Rosemary
Budala
Mwalimu wa Shule ya Msingi Mvuha iliopo katiaka
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini, yeye anakataa juu ya kuendeleza
adhabu ya viboko kwa wanafunzi Shuleni kama tiba ya wanafunzi wenye tabia mbaya,
sikiliza hapa mahojiano yake …Sauti…
https://appfasta.com/tkt/cms/attachments/1682245586–less-file-Rosemary-Budal.mp3 

HAKI ELIMU INAMTAZAMO UPI JUU YA ADHABU YA VIBOKO SHULENI?

Taasisi ya Haki Elimu nimoja kati ya wadau wakubwa
kwenye sekta ya Elimu nchini, na tutakubarina kwamba wameweza kuleta mabadiliko
makubwa kwenye sekta hiyo, kupitia miradi na kampeni zake juu ya maboresho ya
sera na miongozo ya Elimu Msingi na Sekondari nchini, ufuatiliaji wa Taasisi
katika Sekta ya Elimu imekuwa ikizichungulia na kuzichambua
 nyaraka kwa yasio tekelezwa wakati yameelezwa
ndani yake.

Kupitia mazungumzo kati yangu na Mshauri Mwelekezi
kutoka Taasisi ya Haki Elimu, Dkt.Wilberforce
Meena
juu ya adhabu zinazotolewa kwa Wanafunzi Shuleni, ameniambia kwamba,
“ Sio lazima mwanafunzi achapwe viboko ili ajutie kosa lake, ziko njia nyingi
muhimu Mwalimu anaweza kuzitumia ili mwa nafunzi ajutie kosa lake kupitia
adhabu hiyo atakayo pewa kuifanya.

Mfano,
Shule nyingi nchini zinamaeneo ya wazi tena hadi mashamba kwa baadhi ya Shule,
mwanafunzi apewe adhabu hata ya kuhudumia bustani ya miti,maua,kuku kwa muda
furani akiwa yeye peke yake, au apewe mazoezi mengi kuliko kawaida, nasio
kuchapwa viboko kwa kiango kilicho pitiliza wakati mwingine hata bila ruhusa ya
Mkuu wa Shule, kama ambavyo
Mwongozo wa kutoa adhabu mashuleni chini ya kifungu cha 61 (1) (v) cha
Sheria ya Elimu sura ya 353 marejeo
ya mwaka 2002
inavyo sema”.

MTANDAO WA ELIMU
TANZANIA UNASEMA (TENMET):

Juhudi zaidi ziongezwe katika
kuhamasisha utetezi wa vitendo vyote vya kikatili vinavyofanywa kwa mtoto na
kuviweka hadharani ili sheria ipate kuchukua mkondo wake, Serikali na mashirika
mbalimbali yatoe elimu kwa walimu na wazazi kuhusu kanuni ya viboko mashuleni
na utoaji wa adhabu mbadala kwa watoto.

Hata hivyo mwongozo wa utoaji wa adhabu
ya viboko shuleni usambazwe shule zote na kila mwalimu apate nakala, ili Walimu
waendelee kukumbuka mara kwa mara kuwa wana wajibu wa kumlinda mwanafunzi anapokuwa
shuleni na nje ya shule, kwani Mtoto ana haki ya kulindwa, kuendelezwa, kuishi,
kushirikishwa na kutobaguliwa, tunatoa wito kwa wadau wote wa watoto
tushirikiane kwa pamoja ili kuhakikisha mtoto anapata haki zake na anafahamu
wajibu wake.

 HATUA
ZIPI ZILICHUKULIWA BAADA YA KIFO CHA SPERIUS ERADIUS?

Baada ya tukio la kifo
cha

Sperius
Eradius
aliekuwa mwanafunzi wa Shule
ya Msingi Kibeta iliopo katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera,mnamo mwezi Machi,
Mwaka 2019,  Mahakama Kuu ya Kanda ya
Bukoba ilimuhukumu kunyongwa hadi kufa Mwalimu Respicius Patrick baada ya kupatikana na hatia ya kumuua alie kuwa mwanafunzi
wa Shule ya Msingi Kibeta na kumuachia huru mwalimu Herieth Gerald baada ya
kutopatikana na hatia.

NJIA IPI ITUMIKE
KULETA SULUHU YA CHANGAMOTO HII:

Mtandao
wa Elimu Tanzania (TENMET) umechapisha  kwenye tovuti yake  mambo yanayo paswa kuzingatiwa kuhusu utoaji
wa adhabu shuleni, mojawapo ni Vyombo vya habari vizidi kujikita zaidi kwenye
habari za uchunguzi na kuibua vitendo vyote vya ukatili na kuhabarisha umma juu
ya namna bora za kumlinda mtoto, na kila mwananchi atambue kwanza ulinzi wa
mtoto ni jukumu la kila mmoja bila kuangalia wadhifa, jinsia, kabila, dini au
mahali, sambamba na mafunzo kwa waalimu juu ya malezi ya watoto na utoaji wa adhabu
mbadala.

Haki Elimu kupitia kwa Mshauri Mwelekezi
Dkt. Meena anasema viboko sio tiba
ya mwanafunzi mwenye tabia mbaya, bali viboko vinaweza kumjengea usungu mtoto
na chuki kwa mwalimu husika, matokeo yake hataweza kuwa naumakini darasani
mwisho wake nikushindwa kufaru masomo, hasara kwa mafamilia na taifa kwa sababu
taifa linaendelea kuzalisha watu wasio kuwa na utambuzi na maarifa juu ya
elimu.

Mwalimu Rosemary
Budala
kutoka Shule ya Msingi Mvuha amesema, ni vyema kurejea kwenye kanuni
zinazowaongoza walimu kwenye utendaji kazi wao wa kila siku na kuhakikisha
walimu na wazazi wanauwelewa vya kutosha na kutekeleza kanuni ya utoaji adhabu
ya viboko mashuleni.

You Might Also Like

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi

Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili

Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania

KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.

UWEZO TANZANIA YARATIBU KIKAO CHA MIKAKATI YA KUWASHIRIKISHA WAZAZI UELIMISHAJI VIJANA STADI ZA MAISHA.

Tanzania Kids Time April 23, 2023
Share this Article
Facebook Twitter Email Print
Previous Article JUMA LA ELIMU 2023: TENMET INAHAMASISHA UCHANGIAJI WA UBORESHAJI ELIMU
Next Article UMUHIMU WA LISHE SHULENI MOROGORO.
Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

Facebook Like
Twitter Follow
Youtube Subscribe
Telegram Follow
- Advertisement -
Ad image

Latest News

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
//

Tanzania Kids Time: A platform spotlighting children’s and women’s issues in Tanzania, focusing on education, health, and environmental conservation.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

© 2023 Tanzania Kids Time. Powered by Digital Media Innovation Program. All Rights Reserved.

Join Us!

Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..

Zero spam, Unsubscribe at any time.

Removed from reading list

Undo
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?