Kabambala – Morogoro.
yote ya Kitaifa na Kimataifa hasa kupitia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya
Umoja wa Maitaifa (SDGs). Uwepo wa utapiamlo sugu yaani (udumavu) unadhoofisha maendeleo katika
uhakika wa chakula, uboreshaji wa elimu, na afya bora ya mama na mtoto nchini.
Lishe
duni ndio sababu kubwa ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano nchini Tanzania
na inakadiriwa kugharimu serikali asilimia 2.6
ya Pato la Taifa kila mwaka. Upotezaji huu wa mapato uko katika sekta ya kilimo
na husababishwa na ukuaji duni wa akili na mwili unaotokana na utapiamlo.
MWAKA 2015-2016
HALI YA LISHE ILIKUWAJE?
Kulingana
na Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya ya mwaka 2015-2016, takriban theluthi ya watoto wote chini ya miaka mitano
walikuwa na udumavu na asilimia 14
walikuwa na uzito upungufu, Sababu kuu zinazoongoza kuleta utapiamlo ni ukosefu
wa lishe mchanganyiko na bora kwa kila kaya, upatikanaji mbovu wa huduma za
afya (pamoja na maji safi na salama, usafi wa mazingira), na mienendo duni ya
lishe.
WAKATI HUO MKOA WA MOROGORO
HALI YA LISHE ILIKUWAJE?
Licha
ya maendeleo na juhudi za serikali katika kuhamasisha kilimo chenye tija, utatuzi
wa lishe duni kwa watoto bado nimekuwa changamoto kubwa,katika Mkoa wa
Morogoro, chati ifuatayo inaonesha hali ya lishe ya Mkoa huo kuanzia 1992-2018.
Kama
sehemu ya mkakati kamili wa lishe, USAID inazingatia kupunguza kiwango cha
udumavu nchini Tanzania kupitia mipango na huduma za afya na kilimo katika
ngazi za wilaya na jamii. Uwekezaji muhimu kwenye lishe ni pamoja na, kuimarisha
Taasisi za Serikali za Tanzania na asasi za kijamii (AZAKI) zinazoshughulikia
masuala ya lishe, kuongeza juhudi za mabadiliko ya kijamii na mienendo ili
kuboresha namna ya ulishaji wa watoto wachanga na wadogo na kuongeza
upatikanaji wa lishe yenye afya, lishe mbalimbali kwa mama na watoto.
Mradi
wa lishe wa USAID uliambatana kabisa na Mpango wa Utekelezaji wa Lishe ya Kitaifa
wa Tanzania (2016-2021), Mpango mkakati huo uliithibitishia Serikali ya
Tanzania ahadi ya kupunguza tatizo la udumavu kwa watoto chini ya umri wa miaka
mitano (5) kutoka asilimia 34 hadi asilimia 28 ifikapo mwaka 2021.
UDUMAVU NI NINI?
Udumavu ni hali inayotokea wakati uwiano kati
ya urefu na umri vinakuwa chini kwa vigezo vya ukuaji vilivyowekwa na shirika
la afya duniani. kwa jina jingine udumavu unaweza kuelezewa kuwa ni udhaifu wa
ukuaji wa mwili na maendeleo ya ukuaji wa mtoto unaotokea kwa mtoto kutokana na
lishe duni, kuugua mara kwa mara na kukosa msisimuo wa kisaikolojia na kijamii.
UMUHIMU WA LISHE SHULENI
Umuhimu
wa mpango huu ni kumwezesha kijana rika balehe kuelewa mbinu bora za
kuhakikisha anapambana na udumavu katika familia yake na pia atakapokuwa mzazi
baadae , kikubwa muhimu kijana rika balehe yupo kwenye kipindi ambacho
anapevuka hivyo anahitaji vyakula vyenye mchanganyiko wa makundi yote Matano
ili kuweza kumsaidia katika kipindi hiki muhimu.
SABABU ZA WATOTO KUDUMAA
Lishe duni na kuugua
mara kwa mara katika kipindi cha siku 1000 za
mwanzo za maisha ya mtoto, Taratibu duni za ulishaji watoto wachanga na wadogo, ikiwemo
watoto kutonyonyeshwa maziwa ya mama pekee
katika miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa, na
kupewa chakula cha nyongeza kisichokidhi mahitaji
yao kilishe pale wanapotimiza umri wa miezi
sita, na hadi umri wa rika balehe.
wanawake kabla ya ujauzito, wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua. Wanawake
kuwa na kimo kifupi; kutopangilia uzazi na hivyo kuzaa karibu karibu; na tatizo
la wasichana kupata mimba wakiwa katika umri mdogo.
MADHARA YA UDUMAVU:
Mtoto akidumaa hupata
athari zisizoweza kurekebishwa kwani athari hizo hudumu katika maisha yake
yote, Udumavu husababisha kupungua kwa kasi ya maendeleo ya ukuaji wa akili
hali inayosababisha watoto kupata matokeo duni kielimu, Udumavu husababisha
kupungua kwa kasi ya maendeleo ya ukuaji kimwili hali inayosababisha watoto
kuwa na afya duni.
Kupungua kwa uwezo wa
kufanya kazi hali inayosababisha kupungua kwa tija na mapato kiuchumi, Kuongezeka
kwa uwezekano wa watoto waliodumaa kuwa na uzito uliozidi au kiribatumbo, kuugua
magonjwa ya moyo, kiharusi, shinikizo kubwa la damu, na kisukari wakati
wanapofi kia umri wa utu uzima.
Kupitia mradi wa USAID/Lishe Endelevu uliokuwa
ukitekelezwa nchini kwa mikoa minne ukiwemo Mkoa wa Morogoro chini ya Shirika
la Save the Children kwa
kushirikiana na Asasi za kiraia ikiwemo UMWEMA kwa Mkoa wa Morogoro, ili
kuhakikisha wanayafikia malengo ya kupunguza Udumavu kwa Watoto na Vijana
balehe ulianzisha mpango wa kuhamasisha afua za lishe kwa vijana balehe
mashuleni ilikuwapa mbinu wezeshi vijana rika jinsi ya kuweka kipaumbele aina
ya vyakula wanavyotakiwa kula.
Akizungumza kwa niaba ya meneja
wa asasi ya Umwema Bi, Felista Mwalongo
ameniambia kwamba, “malengo ya uhamasishaji afua za lishe, ulilenga kuwafundisha
ratiba ya vyakula kuanzia asubuhi hadi usiku huku wakiwezeshwa kupata mbinu
mbalimbali za kuhakikisha kuna upatikanaji wa chakula cha kutosha, kwa makundi
yote 5 wawapo nyumbani kwa kuwasaidia wazazi wao namna ya upangaji milo na
kuandaa bustani majumbani.
Pia
kuanzisha bustani za mfano mashuleni ambazo zinatumika kuwapa ujuzi vijana ili
waweze kwenda kuzifanya nyumbani na kuwa washauri wazuri juu ya masuala ya
Lisha katika jamii inayomzunguka hasa kwa vijana rika balehe ambao
hawakubahatika kupata mafunzo hayo”.
MBINU ZIPI ZILITUMIKA
KUTOA ELIMU HII?
Mbinu
zilizo tumika ni michezo iliyokuwa nalengo la kumuandaa kijana kujua akitumia
aina fulani ya chakula bila kujali yale makundi Matano nini athari yake, Pia
jinsi ya kujua kuweka vipaumbele pindi anapotaka kufanya manunuzi ya aina
yoyote baada kuuza mazao aliyoweza kuzalisha kupitia shughuli za shamba na
ufugaji.
MRADI ULIFANIKIWA KWA KIASI GANI?
Mafanikio
ya mpango huu ni kuweza kuwafikia vijana wa rika balehe mashuleni kwa asilimia
mia kulingana na malengo ya mradi, hivyo kwa kiwango hicho cha vijana
waliofikiwa wamekuewa chachu katika familia zao ambako huko kuna Watoto chini
ya miaka miwili ambao wameweza kuondokana na udumavu kupitia vijana rika balehe
kuhamasisha afua za lishe kwa wazazi wao.
Mpango
huu umeweza kuwaongezea vijana rika balehe kufanya chaguzi sahihi ya vyakula
walavyo kwani wamejua ni bora kula chakula chenye kukuletea virutubishi kuliko
kupenda kula vyakula visivyo na faida katika mwili
Programu
ya Lishe endelevu ilitumia utaratibu wa kuunda klabu za lishe ambapo huko ndiko
vijana waliweza kupata elimu na mbinu mbalimbali,Vijana wa lika balehe baada ya
kupata elimu shuleni kupitia club zao waliweza kwenda kuzifanya majumbani kwao na jamii kwa ujumla, Mfano
mzuri wa shule ambayo ilifanya vizuri wakati wa utekelezaji wa mpango huu ni
shule ya sekondari Mafiga, Mbinu pekee zilizotumika katika shule hii ni
uhamasishwaji ambao ulifanyika kupitia mwalimu aliyeteuliwa kusimamia clabu
iliyoundwa shuleni.
Shule
hii iliweza kuwa na bustani ya mbogamboga na matunda ambayo kila mwanaclabu
alihamasika kuihudumia ili mwisho wa siku waweze kutumia vyakula
vilivyopatikana katika eneo la shule yao, na hata kupitia bustani walizo
zianzisha nyumbani kwao kwa kushirikiana na wazazi.
Kuna
changamoto chache ambazo ziliukabili mpango huu ikiwa nipamoja na Ukame na
ukosefu wa maji kwa baadhi ya shule kupelekea bustani za mfano kukauka, kuhamahama
kwa waalimu ambao walipewa mafunzo ya jinsi ya kutumia zana za kufundishia. Pia
bustani zilihitaji vifaa vya kutunzia kama keni za kumwagilia hivyo sio shule
zote ziliweza kuwa na vifaa vya umwagiliaji.
KIFANYIKE ILI KUZUIA UDUMAVU?
Tuhakikishe kuwa
wanawake wanakuwa na hali nzuri ya lishe wakati wa ujauzito na wakati wa kunyonyesha
baada ya kujifungua, pia vijana balehe wahamasishwe umuhimu wa lishe katika
makuzi yao ilikuondoa udumavu kwenye familia zao.