By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
Tanzania Kids Time
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Mazingira
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Wasiliana Nasi
Reading: MRADI WA BINTI SHUPAVU UNAVYOSAIDIA KUFANIKISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WA KIKE
Share
Notification Show More
Latest News
Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
TANZANIA WILL HOST CIGOFA4 TO FIND CONCRETE SOLUTIONS FOR YOUTH LAND QUESTIONS
Editor's Pick
Aa
Aa
Tanzania Kids Time
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi
  • Contact
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Tanzania Kids Time > Blog > Elimu > MRADI WA BINTI SHUPAVU UNAVYOSAIDIA KUFANIKISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WA KIKE
Elimu

MRADI WA BINTI SHUPAVU UNAVYOSAIDIA KUFANIKISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WA KIKE

Tanzania Kids Time
Last updated: 2024/01/29 at 2:30 PM
By Tanzania Kids Time 7 Min Read
Share
SHARE

 

Picha ya pamoja baina ya wazazi wa Kata ya Ngerengere na watenda kazi wa Shirika la GLAMI

Na Hamad Rashid. 

Mradi wa ‘’Binti Shupavu’’ unaotekelezwa Mkoani Morogoro na
Shirika lisilo la kiserikali la Gilrs Livelihood and Mentorship Initiative (GLAMI),
kwa kuwapatia wanafunzi wa Kike Elimu ya Stadi za Maisha ikiwemo kujitambua,
umekupokelewa vyema na wazazi na walezi baada ya kuonesha nia ya kumsadidia
Binti kukabiliana na changamoto anazoweza kukumbana nazo wakati akiwa Shule.

Shirika la GLAMI linatekeleza Mradi wa Binti Shupavu ikiwa ni
njia ya kufanikisha Lengo la Nne la maendeleo endelevu SDG’s linahohusu Elimu, ambapo
Jumla ya wasichana 824 wameanza kunufaika na Mradi huo kutoka katika Shule za
Sekondari Tisa zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini, ambapo
Mwezi huu wa Tano limekamilisha Programu ya kufanya vikao na wazazi katika
Shule hizo ili kuwajengea uwezo wa malezi kwa watoto wao.

Msimamizi wa Mradi wa Binti Shupavu Mkoa wa Morogoro Einoth
Justine alieleza hatua ya Mradi iliyofikiwa kwa sasa pamoja na kufafanua
matarajio yao kwa wazazi wa wanafunzi wanufaika.

“Mradi wa Binti Shupavu ni Mradi ambao unajihusisha na mabinti ambao wako
Kidato cha kwanza hadi Kidato cha Nne na ni mahususi kwa ajili ya kuhakikisha
hawa mabinti wanapata mafunzo ya Stadi za Maisha pamoja na Elimu ya uongozi
binafsi, ili kuwasaidia kujitambua, kuweza kubaki Shule na kuhitimu Elimu yao
ya Kidato cha Nne na kuendelea mbele zaidi, lakini pia wanafundishwa namna ya
kuwa wastahamilivu kuweza kuzikabili changamoto wanazokutana nazo, ambazo kwa
namna moja au nyingine zingeweza kuwa kikwazo katika safari yao ya Elimu”
Alisema
Einoth Justine.

Einoth Justine akiwa anakabidhi zawadi kwa Mzazi Kassim Abdalah katika Shule ya Sekondari Kisemu

Einoth Justine pia aliongeza kwa kueleza matarajio yao kwa
wazazi “Tangu Mwezi wa Tatu tumekua na mfururizo wa vikao na wazazi, lengo kuu
likiwa ni kuwakumbusha majukumu yao, kusikia kutoka kwako wao wamekua wakifanya
nini kumsaidia huyu Binti kuweza kufikia malengo yake lakini pia tutashirikiana
nao kwa jinsi gani kama Shirika kuhakikisha tunamsaidia Binti kufikia malengo
yake. Matarajio yetu ni kwamba hawa wazazi watakua chachu ya mabadiliko kwenye
Jamii zao wakitimiza majukumu yao, kwa watoto wao hasa wa kike lakini pia
kufuatilia safari yao ya Elimu na kuona kwa namna gani kwa pamoja tunaweza
kuwasaidia hawa mabinti”

Akitoa mchango wake katika kikao cha wazazi na Shirika la
GLAMI, katika Kata ya Ngerengere Mzazi Msafiri Lema, alionesha kuvutiwa na aina
ya mafunzo waliyopewa na wawezeshaji wa kikao hicho, “kwa kweli mmekuja kutufungua
kichwa, kutufungua masikio, tena naenda kuwaambia wale waliokua na udhuru wa
kutofika kwenye kikao hiki, jamani tunatakiwa tufanya moja tufanye mbili katika
malezi ya mabinti wetu ili tuwe na mabinti Shupavu lakini tuwe na Taifa jipya”

Mmoja wa mabinti wanufaika wa Mradi wa Binti Shupavu
anayesoma Kidato cha Tano Shule ya Sekondari Matombo Patricia Lukumay alisema
wakati akiwa mkoani Arusha Mradi wa Binti Shupavu umemsaidia kufikia hatua
aliypo sasa.

Patricia Lukumay alisema “kupitia Binti Shupavu imenisaidia kujua
jinsi ya kutatua changamoto na kukataa vishawishi kwa kusema Hapana kwa kile
ambacho nakiona sio sawa kwangu, kingine imenisaidia jinsi ya kuwa na uwezo wa
kuhimili changamoto zangu, kama kukata tamaa, kuacha Shule labda kuona Somo
flani huliwezi, kuchapwa mwishowe unaona uache Shule hivyo kupitia Binti Shupavu
imenisaidia kunipa njia vitu gani vya kufanya pale ninapokabiliwa na changamoto
kama kufeli somo flani ikiwemo kuomba ushauri kwa wenzangu au kumuomba ushauri
Mwalimu”

Mwanafunzi Patricia Lukumay akifurahia zawadi kutoka GLAMI aliyokabidhiwa na Diwani wa Kata ya Lundi Apia Mkami.

Afisa Elimu Kata ya Ngerengere katika Tarafa ya Ngerengere
Lydia Ntapara alieleza matumaini yake kupitia Mradi wa Binti Shupavu.

“Aah mimi kama Afisa Elimu kata kupitia huu Mradi wa Binti Shupavu
nitahakikisha nafuatilia kwa ukaribu zaidi, kwani kwangu katika kipengele cha
Elimu inanisaidia sana baada ya kujua malengo ya Binti shupavu na jisni
tutakavyoshirikia kwa pamoja kumjenga Binti, na pia nitafuatilia zaidi ili
nijenge mabinti wengi kama nilivyo mimi na wengine kama kina Mama Samia”
Alisema
Lydia Ntapara.

Afisa Elimu Kata Lydia Ntapara Kata ya Ngerengere  kushoto na kulia kwake ni Afisa ustawi wa Jamii Wilaya ya Morogoro vijijini Zebedayo Mbamba

Zebedayo Mbamba ni Afisa ustawi wa Jamii katika Halmashauri
ya Wilaya ya Morogoro Vijijini amekua akishiriki kutoa Elimu ya Haki za Mtoto
na Ukatili wa kijinsia katika vikao vya wazazi wa wanafunzi wanufaika wa Mradi
wa Binti Shupavu, akihojiwa na muwakilishi wetu alisema, “tumekutana na wazazi wengi ambao
wanafunzi wao wanasoma Shule tofauti tofauti katika Halmashauri yetu ya
Morogoro vijijini, hakika kwa Elimu tuliokua tunatoa kwa wazazi tumeona
inafaida na matunda mengi sana kwasababu mwitikio wa wazazi ulikua mkubwa sana
na ni Elimu ambao wazazi wengi wameonesha kuifurahia kwa sababu walikua
hawaijui kwa mfano katika eneo langu nilikua nawafundisha juu ya haki za Mtoto
ili watambue nini wanapaswa kuzitimiza, wengi walikua wakishangazwa na hivi
vitu mfano hasa katika haki ya kumshirikisha Mtoto, kwamba wanapaswa kuwa
marafiki wa Mtoto wengi walikua wakishangazwa. Wazazi wengi walifurahia na hiko
kitu na walionesha kwamba kumbe walikua wameweka Daraja baina yao na wanafunzi”

             Zebedayo Mbamba akiwezesha wazazi Matombo Sekondari.

Mwalimu Mlezi katika Shule ya Sekondari Matombo Mwanamvua
Bakari alisema, mafunzo wanayopewa wasichana Shuleni ni sehemu ya kuwasaidia
wazazi katika wajibu wao wa malezi ambapo wanafunzi pia wameyapokea vyema. “

Mwanamvua Bakari alisema “Hawa mabinti wenyewe wako tayari kupokea
mafunzo na wamependa sana kwa sababu sehemu kubwa ya haya mafunzo ni sehemu
ambayo walezi na wazazi wao hawawezi kufanya na hawajawahi kuyapata kwakweli,
kwa hivyo hawa wawezeshaji wa Mradi wa Binti Shupavu wao wamekuja kuchukua
nafasi ya Mzazi na Mlezi kwenye kuwapa yale mafunzo ambayo mabinti walikua
hawayapati majumbani mwao”

Orodha ya Shule za Sekondari zilizofikiwa na Mradi wa Binti
Shupavu katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro vijijini ni pamoja na
Ngerengere, Bwakila chini, Kisemu, Kiroka, Mkuyuni, Fatemi, Gwata na Matombo
Sekondari.

You Might Also Like

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi

Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili

Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania

KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.

UWEZO TANZANIA YARATIBU KIKAO CHA MIKAKATI YA KUWASHIRIKISHA WAZAZI UELIMISHAJI VIJANA STADI ZA MAISHA.

Tanzania Kids Time May 23, 2023
Share this Article
Facebook Twitter Email Print
Previous Article RIPOTI YA ALIVE JINSI INAVYOTUMIKA KUIAMSHA JAMII KUWANOA VIJANA
Next Article UTUMIKISHWAJI WATOTO KWENYE MIGODI:
Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

Facebook Like
Twitter Follow
Youtube Subscribe
Telegram Follow
- Advertisement -
Ad image

Latest News

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
//

Tanzania Kids Time: A platform spotlighting children’s and women’s issues in Tanzania, focusing on education, health, and environmental conservation.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

© 2023 Tanzania Kids Time. Powered by Digital Media Innovation Program. All Rights Reserved.

Join Us!

Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..

Zero spam, Unsubscribe at any time.

Removed from reading list

Undo
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?