UTUMIKISHWAJI IPOJE WILAYANI SONGWE?
Na, John Kabambala: Wilaya ya
Songwe iko katika Mkoa wa Songwe nchini Tanzania. Ilianzishwa rasmi Mwezi
September,2015 na ni moja kati ya Wilaya mpya zilizoanzishwa baada ya
kugawanywa kwa Mkoa wa Mbeya.
Kuhusu
utumikishwaji wa watoto katika kilimo cha zao la tumbaku Wilaya ya Songwe, ni
jambo ambalo limekuwa likijitokeza katika maeneo mengi ya Tanzania, ikiwemo
wilaya hiyo. Utumikishwaji wa watoto katika kilimo ni suala la kusikitisha
ambalo linawanyima watoto haki zao za msingi, kama elimu na afya, na kuwaweka
katika hatari ya kudhurika kimwili na kisaikolojia.
Tumbaku ni
zao muhimu la biashara nchini Tanzania, na wilaya ya Songwe imekuwa moja ya
maeneo yenye kilimo kikubwa cha zao hilo, kwa bahati mbaya, watoto wamekuwa
wakitumikishwa katika hatua mbalimbali za uzalishaji wa tumbaku, ikiwa ni
pamoja na kulima, kuvuna, kukausha na hata kusaidia katika usindikaji wa
tumbaku.
CHANZO CHA TATIZO
HILI?
“Familia nyingi hapa kijijini shughuli za
kiuchumi zinategemea kilimo cha tumbaku, zamani kabla ya kuletwa mradi wa
kupinga utumikishwaji wa watoto Prosper
mashambani walitumia watoto wao kama nguvu kazi, ndio maana kuna Shule Fulani
kwenye kata hii kufelisha darasa zima ilikuwa kawaida tu. Maana wazazi wengi
walishindwa kuthamini umuhimu wa elimu, ila kilimo cha zao la tumbaku wakakipa
kipaumbele, Lakini sasa hali hiyo imepungua sana” Alisema Maria Kawana
mkaazi wa kijiji cha Gua Kata ya Gua Wilani Songwe.
Tanzania ni
miongoni mwa nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa na Shirika la Kazi Duniani
(ILO) zilizoridhia Mikataba yote inayolenga kuwalinda, kuwatetea na kuendeleza
haki za Watoto. Mikataba hiyo ni Mkataba wa Haki za Mtoto wa 1989 wa
Umoja wa Mataifa, Mkataba ya Shirika la Kazi Duniani Na. 138 unaohusu
umri wa chini wa mtoto kuajiriwa na Na. 182 Unaohusu kazi hatarishi
zisizoruhusiwa kufanywa na Mtoto.
Serikali
imekuwa mstari wa mbele tangu mwaka 1994 kupambana na tatizo la
utumikishwaji wa watoto kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi kwa
kuweka Mipango na Mikakati ya kitaifa na sheria zinazotekelezwa hapa nchini.
Sababu kuu
za utumikishwaji wa watoto katika kilimo cha tumbaku ni umaskini, ukosefu wa
elimu, na mazingira duni ya kijamii. Watoto wengi hulazimika kusaidia familia
zao katika shughuli za kilimo ili kusaidia katika kupata kipato cha familia.
Aidha, kukosekana kwa fursa za elimu na ufikiaji mdogo wa huduma za kijamii
katika wilaya hiyo huwafanya watoto wawe katika hatari zaidi ya utumikishwaji.
Serikali ya
Tanzania na mashirika ya kitaifa na kimataifa yamechukua hatua kadhaa za
kukabiliana na tatizo hili, miongoni mwa mashirika ya kitaifa ni TDFT ambalo
nimekuwa likitekeleza mradi wa Prosper Reset unao waondoa watoto
wanaotumikishwa katika kilimo cha zao la Tumbaku kwa Mikoa mitatu Tanznaia
ambayo ni Tabora, Mbeya na Songwe.
Ndg. Fredrick
Malaso yeye ni
meneja mradi wa Prosper Reset
anasema tangu mwaka 2011 mradi huo ulianza kutekelezwa katika Wilaya tatu za
mkoa wa Tabora (Sikonge,Urambo na Kaliua), kufikia mwaka 2018 mradi uliongeza
Wilaya mbili Chunya na Songwe kutoka kwenye Mikoa ya Mbeya na Songwe.
HUO:
ya mafanikio ya mradi huo ni pamoja na kuwaondoa watoto 24,150 kutoka katika utumikishwaji, na kusaidia kaya 970 kuwapa elimu ya kuanzisha shughuli
za ujasiliamari na biashara ndogondogo za kuongeza kipato kupitia vikundi 56 vilivyo anzishwa na kusimamiwa na
Mradi huo.
Kwa upande
wake Afisa kazi Mkoa wa Songwe Bi, Pendo
Lugendo amebainisha kwamba, Sheria za kazi zinakataza utumikishwaji wa
watoto, na kuna juhudi za kuongeza uelewa kuhusu haki za watoto na kuzuia
utumikishwaji kupitia elimu na mafunzo kwa wazazi na jamii kwa ujumla.
Pamoja na
changamoto hizo, jitihada za Serikali na Wadau wanashirikiana kuhakikisha kuwa
watoto wanapata haki zao za msingi na wanakuwa katika mazingira salama na yenye
maendeleo, ili kutokomeza utumikishwaji wa watoto katika kilimo cha tumbaku na
maeneo mengine ya Wilaya ya Songwe.
JE, SULUHISHO NI
NINI/NINI KIFANYIKE
Vyombo vya
habari vina nafasi muhimu katika kuongeza uelewa na kuhamasisha umma kuhusu
athari za utumikishwaji wa watoto wadogo, Wananchi wanaweza kuchukua hatua kwa
kutoa taarifa kuhusu matukio ya utumikishwaji, kushiriki katika harakati za
kutetea haki za watoto, na kusaidia katika kuweka mazingira salama kwa watoto.
Serikali,
NGOs wananchi, na mashirika ya kimataifa wanahitaji kufanya kazi pamoja ili
kuzidisha jitihada za kupambana na utumikishwaji wa watoto wadogo. Ushirikiano
huu unaweza kujumuisha kubadilishana uzoefu, kuendeleza mikakati ya pamoja, na
kuimarisha mifumo ya sheria na utekelezaji.
Suluhisho
lingine ni kuweka mkazo kwenye elimu na ufahamu kuhusu haki za watoto. Elimu
bora na endelevu inaweza kusaidia kubadilisha mitazamo na mila potofu
zinazochangia utumikishwaji wa watoto. Pia, ni muhimu kukuza fursa za kiuchumi
kwa familia na kujenga mifumo ya ulinzi wa watoto ili kuwalinda na kuwawezesha.
Uhamasishaji
kuhusu uelewa na kushiriki katika kampeni za kupinga utumikishwaji, kama vile kampeni
za kutetea haki za watoto na kuelimisha jamii, inaweza kuleta mabadiliko
makubwa. Umuhimu wa kuwapa sauti watoto wenyewe na kusikiliza maoni yao, kwani
wao pia ni sehemu muhimu ya mchakato wa kutafuta suluhisho la tatizo la
utumikishwaji katika eneo husika.
Naamini
kwamba makala hii itakuwa ni mwanga wa matumaini na mwito wa hatua za haraka
katika kukabiliana na utumikishwaji wa watoto wadogo.