Winfrida Ndondo-Aga Khan Hospital:
Na, John Kabambala: Katika Manispaa ya Morogoro, kama ilivyo katika maeneo mengine duniani, chanjo kwa watoto ni jambo muhimu sana kwa ustawi wao na jamii kwa ujumla. Hata hivyo, tatizo la kutofuatilia ipasavyo ratiba ya chanjo limekuwa likiathiri maendeleo ya afya na kusababisha ongezeko la magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa watoto. Makala hii inalenga kuangazia tatizo hili, chanzo chake, na suluhisho lililopo ili kuhamasisha wazazi/walezi kufuatilia ratiba ya chanjo kwa watoto wao.
TATIZO NI NINI?
Tatizo kuu linalojitokeza ni baadhi ya wazazi wa kiume kushindwa kushiriki kikamilifu kutofuatilia ratiba ya chanjo kwa watoto wao, badala yake huachiwa jukumu hilo mama wa watoto kama ambavyo amenieleza Joyce Lutagwa mzazi wa watoto wanne na mkaazi wa Kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro, amesema tangu ajifungue watoto wake mumewake hajawahi kushiriki hata siku moja kumkumbusha mwezi wake kuhusu tarehe ya kumpeleka mtoto wao kituo cha afya kwaajili ya chanjo.
Anasema bi, Joyce Lutagwa “hali hii huninyong’onyesha sana kawani kwa siku ambazo inatokea ninaumwa na nitarehe ya kiliniki kwa mtoto, inamaana hawezi kupata chanjo, kutokana na ushiriki wa mume wangu kutoashiriki kwa namna yeyote kufuatilia ratiba za chanjo kwa watoto. Nadhani sasa kwa kipindi hiki mimi ninazungumza kwa niaba ya wazazi wenzangu wanawake ambao hupitia changamoto kama hii, kuiambia serikali kuweka ulazima nakutilia mkazo juu ya kutuhudumia sisi wanawake bila wanaume huduma hakuna”, Alisema.
Bi, Joyce Lutagwa.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya Tanzania iliamua kuandaa ratiba ya chanjo kwa watoto walio kwenye ratiba za chanjo, ilichapishwa kwenye tovuti ya Wizara hiyo na maeneo yote ya zahanati, vituo vya afya na hospitali za mikoa yote kwenye Taifa hilo la afrika mashariki. Lengo kuu la kuandaa na kuweka ratiba hiyo nikuwasaidia wazazi/walezi kufuatilia na kujua tarehe ambayo mtoto anapaswa kupelekwa kwenye kituo cha afya kupata chanjo.
CHANZO CHA TATIZO:
Katika kufahamu kwa undani zaidi juu ya tatizo hili nilimtafuta mtaalamu wa afya ya mama na mtoto kutoka hospitali ya Aga Khan ya mjini Morogoro Winfrida Ndondo, kwanza kabisa nilimuuliza, Kwa uzoefu wako nisababu zipi zinawafanya baadhi ya wazazi kushindwa kufuatilia ratiba za chanjo kwa watoto wao? “Kuna sababu kadhaa zinazochangia tatizo la kutofuatilia ratiba ya chanjo katika Manispaa ya Morogoro kwa baadhi ya wazazi/walezi. Mojawapo ni uelewa mdogo wa umuhimu wa chanjo na athari zake kwa watoto. Baadhi ya wazazi/walezi hawana taarifa sahihi kuhusu magonjwa yanayoweza kuzuilika na madhara yanayoweza kutokea kwa watoto wao iwapo hawatapata chanjo muhimu kwa wakati sahihi ulio pangwa na Wizara ya Afya pamoja na Shirika la Afya Duniani –WHO”.
Winfrida Ndondo Anasema, “hapa hospitalini kwetu tuna ratiba ya wazazi wanao jifungulia hapa wanaacha namba za simu ama wanaokuja kuanzia hapa kiliniki huacha namba za simu asipo hudhulia kwa mara kwanza, tutampigia simu kuulizia kwanini hakufika amepatwa na changamoto zipi. Kisha tuna mueleza kama anaweza kuhudhulia kiliniki siku inayofuata kama chanjo ya mtoto wake ni umri wa kupata chanjo za baada ya wiki tatu au sita, pia tunakuwa tunawashauri wazazi kuwa na ratiba hizi nyumbani tena wanaweza kutengeneza kalenda kwenye simu zinakua zinawakumbusha siku mbili au siku mojan kabla”.
Winfrida Ndondo:
Huduma za kuelimisha umma kuhusu chanjo na umuhimu wake zinaweza kuwa duni au hazifiki kikamilifu kwa jamii, njia kuu zinazo tumika kwa utoaji elimu ya afya ni kupitia vituo vya afya, zahanati na Hospitali ambako wazazi wengi wa kiume hawahudhulii kuambatana na wazazi wenzao wakike wakati wa kupeleka watoto kwenye huduma za chanjo. Hii inaathiri uelewa wa wazazi/walezi na kuwafanya washindwe kufuatilia ratiba ya chanjo kwa watoto wao.
ATHARI ZA MTOTO ASIPO PATIWA CHANJO:
Bi, Winfrida Ndondo anafafanua kwamba, iwapo mtoto akikosa chanjo muhimu kunauwezekano wa kusababisha ongezeko la maambukizi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika, kama vile surua, polio, kifaduro, na magonjwa ya kupooza, hivyo kunawatoto wengine walipooza situ kwamba walizaliwa hivyo hapana, ila inawezekana kabisa wazazi/walezi walipuuzia kufuatilia ratiba za chanjo kwa watoto wao mwaisho wasiku mtoto akapata ugonjwa wa kupooza wao bilakujua kwamba kilischo sababisha ni ukosefu wa chanjo.
Wanaume kwa maana ya wazazi wakiume wametupiwa lawama zaidi kwenye jambo hili kwa lugha nyingine nikwamba wazazi hawa jinsi ya kiume wanachangia watoto wengi kupatwa na ugonjwa ambao ungeweza kuzuilika, kutokana na mchango wao hafifu katika kushiriki ufuatiliaji wa ratiba za chanjo kwa watoto wao. Nimezungumza na Mathiasi Katema mkaazi wa Kata ya Mazimbu Manispaa ya Morogoro juu ya lawama hizo wanazotupiwa, “nikweli kabisa wanawake wanacho sema kwamba hatushiriki vyakutosha kwenye kukumbuka kwamba kesho ni ratiba ya chaanjo ya mtoto, mara nyingi jukumu hilo nikana kwamba ni la wanawake tu, nadhani sasa serikali igeukie kundi hili tupewe elimu kuhusu faida na madhara ya kushindwa kufuatilia ratiba za chanjo kwa watoto, ilikupunguza magonjwa kwa watoto wetu”.
Ndg. Mathiasi Katema:
UTATUZI WA JAMBO HILI NI NINI?
Kwa kushughulikia tatizo hili la kutofuatilia ratiba ya chanjo, hatua kadhaa zinahitajika kuchukuliwa. Kwanza kabisa, serikali ya Manispaa ya Morogoro inapaswa kuwekeza zaidi katika kampeni za elimu kuhusu chanjo na umuhimu wake. Hii inaweza kufanyika kwa kuimarisha huduma za afya ya umma na kuwahamasisha wataalamu wa afya kutoa elimu ya kina kwa wazazi/walezi juu ya umuhimu wa chanjo na madhara ya kutofuatilia ratiba ya chanjo.
Pili, ni muhimu kuwezesha upatikanaji wa chanjo kwa urahisi kwa wazazi/walezi. Vituo vya afya na zahanati zinapaswa kuhakikisha kuwa kuna upatikanaji wa chanjo za lazima kwa wakati wote. Pia, kampeni za chanjo zinaweza kuandaliwa kwa ushirikiano na taasisi za kijamii na viongozi wa jamii ili kuhamasisha wazazi/walezi kuchukua hatua na kufuatilia ratiba ya chanjo.
Tatu, teknolojia ya mawasiliano inaweza kutumika kwa faida katika kuelimisha na kuhamasisha wazazi/walezi. Matumizi ya ujumbe mfupi wa simu (SMS) na mitandao ya kijamii yanaweza kuwa njia nzuri ya kuwakumbusha wazazi/walezi juu ya ratiba ya chanjo kwa watoto wao. Mifumo ya ufuatiliaji wa elektroniki inaweza kuwekwa ili kusaidia watoa huduma za afya kufuatilia na kumbukumbu za chanjo zilizotolewa kwa watoto.
Kufuatilia ratiba ya chanjo kwa watoto ni muhimu sana katika Manispaa ya Morogoro. Tatizo la kutofuatilia ratiba hii limekuwa likisababisha kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika. Kwa kuwekeza katika elimu kwa wazazi/walezi, kuhakikisha upatikanaji wa chanjo, na kutumia teknolojia ya mawasiliano, tunaweza kupunguza tatizo hili na kuimarisha afya ya watoto na jamii kwa ujumla. Ni wajibu wetu sote kuhakikisha tunazingatia ratiba ya chanjo na kuchangia katika kujenga jamii yenye afya na maendeleo thabiti.