Picha kutoka -TMA
Na, John Kabambala:Athari za kiafya kwa watoto wakati wa baridi kali
nchini Tanzania ni suala linalohitaji umakini. Tatizo hilo linaweza kuwa na
athari kubwa kwa afya na ustawi wa watoto. Njia bora ya kukabiliana na hali
hiyo ni kuelewa tatizo, kuchunguza chanzo chake, na kutafuta suluhisho muhimu.
Historia ya Baridi nchini Tanzania inatuonesha
kwamba,Tanzania kama nchi nyingine za
Afrika Mashariki, hukumbwa na msimu wa baridi kila mwaka. Msimu huu huanzia mwezi Juni hadi Agosti, na katika maeneo ya
juu ya milima ya nyanda zajuu kasikazini kama vile Kilimanjaro na Mbeya, nyanda
za juu kusini hali ya baridi inaweza kuwa ya kuvutia. Baridi hii huletwa na
hewa kutoka kaskazini mwa jangwa la Sahara na pia kwa sababu ya urefu wa maeneo
haya ambayo yanapata joto kidogo kutokana na kuyakaribia mawingu.
Kwa mujibu wa taarifa ya hali ya hewa
iliotolewa mwishoni mwa mwezi Mei 2023 inaonesha kwamba, kusini mwa mkoa wa
Morogoro unatarajiwa kuwa nahali ya joto lachini nyuzi joto 7-16 “Hali ya joto la
bahari katika ukanda wa tropiki ya kati ya bahari ya Pasifiki inatarajiwa kuwa
ya juu ya wastani, hali inayoashiria uwepo wa El Niño katika msimu wa Kipupwe
2023, hivyo kutarajiwa kusababisha mchango mdogo katika mwenendo wa mvua nchini
hususan maeneo ya pwani”. Alisema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus
Chang’a.
Kupitia taarifa hiyo ilieleza athari zinazoweza kujitokeza
pamoja na kutoa ushauri kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za
hali ya hewa katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku, nakushauri jamii
kuchukua tahadhari za kiafya dhidi magonjwa yanayoweza kusababishwa na baridi,
vumbi na matumizi ya maji yasiyo safi na salama.
Kupitia taarifa hiyo ya TMA imenisukuma kuandaa makala hii ambayo inaangazia athari za
kiafya kwa watoto wakati wa msimu huu wa baridi nchini Tanzania, Baridi ni
msimu ambao unaweza kuwa na madhara ya kiafya kwa watoto wadogo nchini
Tanzania. Hali ya hewa ya baridi kali inaweza kuathiri vibaya afya ya watoto na
kuongeza hatari ya magonjwa mbalimbali. Katika makala hii, tutachunguza
historia na athari za kiafya zinazowakabili watoto wakati wa msimu wa baridi nchini
Tanzania.
Picha kutoka -TMA
DKT.
WA WATOTO ANASEMAJE KUHUSU MSIMU HUU WA BARIDI:
Monica
Apolo ni Dkt. wa watoto kutoka hospitali
ya taifa ya Muhimbili nilimuuliza tutarajie nini kwa kipindi hiki cha msimu huu
wa baridi? ” Kwa kipindi hiki cha msimu wa baridi watoto hupatwa na
changamoto za magonjwa mbalimbali iwapo wazazi/walezi hawatachukua hatua,
watoto wanaweza kusumbulia na Pumu, Mafua makali, Ugonjwa wa Macho na Ugonjwa
wa ngozi. Wasimamizi na walezi wa watoto wanapaswa kuhakikisha wanawavalisha
ngua nzito, soksi,kofia na wakati wa usiku kuwafunika shuka nzito, ili
kuwapatia joto la nyuzi joto 15-25, kama
eneo la kusini mwa mkoa wa Morogoro ambako kunatarajiwa kua na nyuzi joto la
chini 7-16 kwa mujibu wa taarifa ya
TMA watoto wahakikishiwe usalama wa joto
kwa uangalizi” Dr. Monica Appollo
alisema.
ATHARI ZA KIAFYA KWA WATOTO WAKATI WA BARIDI:
Athari za Kiafya kwa Watoto wakati wa Baridi Kali
Msimu wa baridi kali unaleta athari kadhaa za kiafya kwa watoto nchini
Tanzania, hali ya hewa ya baridi kali inaweza kuathiri mwili wa mtoto na
kusababisha magonjwa na matatizo yafuatayo:
1. Mafua Msimu wa baridi kali huambatana na
kuongezeka kwa magonjwa ya mafua na influenza. Watoto wadogo wako katika hatari
kubwa ya kuambukizwa virusi vinavyosababisha mafua. Dalili za mafua ni pamoja
na homa, kikohozi, pua kujaa, na hisia za uchovu. Watoto ambao wana mfumo
dhaifu wa kinga wanaweza kuwa katika hatari ya kupata madhara makubwa kutokana
na magonjwa haya.
2. Pneumonia: Pneumonia ni mojawapo ya
magonjwa hatari yanayosababishwa na msimu wa baridi kali. Hali ya hewa baridi
inaweza kuongeza hatari ya maambukizi ya bakteria na virusi katika mapafu ya
watoto. Pneumonia inaweza kusababisha matatizo ya kupumua, homa, kukohoa, na
maumivu ya kifua. Watoto wachanga na wale walio na mfumo dhaifu wa kinga wako
katika hatari kubwa ya kuathiriwa na pneumonia.
3. Athari za Ngozi: Baridi kali inaweza kuathiri
ngozi ya watoto na kusababisha matatizo kama vile ngozi kavu, kukasirika, na
kuwasha. Watoto wadogo wanaweza kuwa na mabusha au michubuko kwenye ngozi
kutokana na kuvaa mavazi yasiyofaa kwa kipindi cha baridi. Ni muhimu
kuhakikisha watoto wanavaa mavazi yanayowalinda vizuri dhidi ya baridi na
kutumia losheni za kujikinga ili kudumisha afya nzuri ya ngozi.
4. Maambukizi ya njia ya hewa: Watoto wakati wa
baridi kali wanaweza kuwa katika hatari ya kuambukizwa maambukizi ya njia ya
hewa kama vile bronchitis na maambukizi ya sikio. Mabadiliko ya ghafla ya joto
na hewa kavu yanaweza kuathiri mfumo wa kupumua wa watoto na kuwafanya kuwa
rahisi kuambukizwa. Watoto wanaoishi katika mazingira yasiyo safi na wale walio
na matatizo ya upumuaji wako katika hatari zaidi.
Annastazia Thomas yeye
ni mzazi wa mtoto mmoja mkaazi wa Kata ya Mjimkuu Manispaa ya Morogoro anasimlia
changamoto aliowahi kuipitia katika malezi ya mtoto wake kipindi cha msimu wa
baridi kama huu, “Nakumbuka nilikua kwetu
kijijini na kwa sababu alikuwa mtoto wa kwanza sikuwa naelewa chochote
kuhusiana na athari za baridi kwa mtoto mdogo.
Nilipata shida sana kumsaidia
mtoto, hadi bibi alipo amka na kuniambia mfunike nguo nyingi kasha bibi
aliwasha moto usikuule ili nyumba ipate joto, kwani hatukua na namna ya
kumpeleka kwenye kituo cha afya usiku ule, asubuhi ilipofika hali ile ilikuwa
imepungua nikampeleka kituo cha afya baada ya kufika dkt.alivyo mpima alisema “mtoto
huyu leo asingepata huduma ya afya uwezekano wa kumpoteza ulikuwa mkubwa” kumbe
alikuwa na Pneumonia
tangu siku hiyo nikawa makini wakati wa baridi kwa mtoto” Annastazia Thomas, alisema.
KIPI MZAZI/MLEZI AFANYE
KIPINDI HIKI CHA BARIDI?:
Hakikisha
watoto wanavaa mavazi yanayowalinda vizuri dhidi ya baridi, kama vile sweta,
jaketi, soksi, na kofia, Epuka mabadiliko ya ghafla ya joto, kwa mfano,
kuwaweka watoto ndani ya vyumba vyenye joto kali baada ya kuwa nje katika hali
ya baridi, Hakikisha watoto wanapata lishe bora na ya kutosha ili kuimarisha
kinga yao dhidi ya magonjwa, Weka mazingira ya ndani safi na salama ili kuzuia
maambukizi ya njia ya hewa, Pata chanjo zinazopendekezwa kama vile chanjo ya
pneumonia na influenza.
Baridi
kali inaweza kuwa na athari mbaya kwa watoto nchini Tanzania. Watoto wadogo
wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa kama vile mafua, pneumonia, na
maambukizi ya njia ya hewa. Ni muhimu kuchukua tahadhari za kutosha kwa kuvaa
mavazi yanayofaa, kudumisha usafi, na kuhakikisha lishe bora kwa watoto.
Vilevile, ni vyema kupata chanjo sahihi ili kulinda watoto dhidi ya magonjwa
yanayosababishwa na msimu wa baridi kali. Kwa kufanya hivyo, tunaweza
kuhakikisha kuwa watoto wetu wanabaki salama na wenye afya wakati wa msimu huu.
Elimu na uelewa: Ni
muhimu kutoa elimu kwa wazazi na walezi juu ya athari za baridi kali kwa watoto
na jinsi ya kuchukua hatua za kuzuia. Hii inaweza kujumuisha kufundisha umuhimu
wa kuvaa nguo za kutosha, kuhakikisha lishe bora, na kudumisha usafi, wazazi
wanapaswa kuhakikisha wanawanunulia majaket watoto wao pamoja na viatu vizito
ambavyo vitawasaidia kujinga wakati wa msimu huu wa baridi.