“Usiku ule tuli lala na kuamka salama
asubuhi….lakini hakuna hata mmoja kati yetu alie hisi kuwepo kwa hali tofauti
kiafya kwa mtoto wetu….. nikana kwamba siku hiyo ilikuwa nyeusi tiii, yenye giza nene isio na huruma wala
tumaini hata kidogo….saa chache tu baada ya kupambazuka asuhi, historia ya
furaha iligeuka kuwa ya huzuni,,, sitaisahau siku hii, hakika nikumbukizi yenye
uchungu…..”
Na, John Kabambala: Katika kijiji kidogo kilichopo karibu na
mji mkuu wa Tanzania Dodoma, alipo zaliwa msichana mmoja tulie mpa jina la Nenka Bryiyo . Mtoto wa kwanza na
wapekee katika familia yao ya mzee Bryiyo
Mkoma, baada ya wazazi wake kuhangaika kwa zaidi ya miaka kumi hivi kwenye
ndoa yao pasipo kupata mtoto, baadae akazaliwa mtoto wa kike wakamwita “ Nenka”
hakika walimfurahia sana kumpokea duniani. Kuanzia utotoni, Nenka alikuwa na tabasamu la kuvutia na
alikuwa na ndoto kubwa za kufikia malengo yake maishani.
Maisha yake ya utotoni yalijawa na furaha
na upendo kutoka kwa familia yake. Nenka
alikuwa na shauku ya kujifunza na alipenda shule. Aliweka bidii kusoma na
kufaulu vizuri katika masomo yake. Pamoja na changamoto za kiuchumi katika
familia yao, wazazi wake walijitahidi kuhakikisha wanampa elimu bora ili
azifikie ndoto zake.
KIINI CHA MAKALA HII KINAANZIA HAPA: NI KIPI
KILIMSIBU NENKA?
“Nakumbuka
akiwa darasa la tatu (3) maisha yake yalibadilika ghafla wakati Nenka siku isio tarajiwa alianza
kuonyesha dalili za kuumwa. Alipata homa kali, uchovu, macho na ngozi yake yakawa
na rangi isiyo ya kawaida” alisema Steloy
Jaiso mama mzazi wa Nenka.
Wazazi wa huyu mtoto walipatwa na
wasiwasi kubwa lakini kwa haraka sana walichukua hatua ya kumpeleka hospitalini
kwa uchunguzi zaidi, maana mtoto huyu alikuwa kama mboni ya macho yao.
Nenka alihitaji matibabu ya haraka na tena matibabu
ya kibingwa. Wazazi wake, ingawa walikabiliwa na changamoto ya kifedha,
walifanya kila wawezalo kumkatia bima ya afya ili kumwezesha mtoto wao kupata
matibabu yanayohitajika, kwa wakati sahihi bila kujali hali walio nayo ngumu ya
kiuchumi.
“Baada
ya uchunguzi wa kina, daktari alikuja kutuelezea majibu walio yabaini alipo uliza
“wazazi wa Nenka wapo?” Mke wangu alipiga kelele sana kwa
hofu akidhani kwamba Nenka amefariki..kumbe
haikua hivyo daktari alisema mtoto huyu lazima aanzishiwe matibabu kuanzia sasa
ili kunusuru uhai wake” Alisema Bryiyo
Mkoma baba wa mtoto.
HOMA YA INI NI NINI?
Ili kupata majibu ya maswali yangu nilimtafuta
daktari wa watoto kutoka katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Morogoro Dkt.
Hawa Ngasongwa, nae anatoa ufafanuzi huu kuhusu homa ya INI. “Homa ya ini ni ugonjwa
unaosababishwa na virusi vinavyoingia mwilini kwa binadamu na kusababisha ini
kupoteza uwezo wakufanya kazi zake vizuri na kusinyaa na mwishoni kabisa
kusababisha saratani inayoweza kupelekea kifo kwa watoto” alisema.
CHANZO CHA UGONJWA HUU NI NINI?
“Aasilimia kubwa kwa watoto ni maambukizi
kutoka kwa mama mjamzito mwenye maambukizi haya kwenda kwa mtoto wake mchanga
wakati wa kujifungua, Kushirikiana vitu vya ncha kali kama kiwembe,sindano
mswaki nk na Kuongezewa damu yenye maambukizi ya homa ya ini”
DALILI ZA UGONJWA HUU WA INI
KWA WATOTO NI ZIPI?
“Hizi dalili zinafanana na maradhi mengine
ya Watoto, hivyo ni muhimu kufanya
vipimo haraka mara tu mtoto akionesha dalili hizi, kuna watoto wasioonyesha
dalili yoyote, lakini miongoni mwa viashiria vya ugonjwa huu moja wapo ni
kuchoka, homa, kukosa hamu ya kula, kichefuchefu na hata kutapika, manjano kwa
manjo na Ngozi ya mwili (jaundice), kuharisha, maumivu ya tumbo, kupata mkojo wenye rangi iliyokooza
(cocacola urine)” Dkt. Ngasongwa
Madhara ya homa
ya ini ni makubwa kwa watoto, inashauriwa kupata chanjo mara tu baada ya kupima
kama hunamaambukizi ya homa ya ini ili kujikinga. Chanjo hii inasaidia kuandaa
mwili kutengeneza kinga dhidi ya ugonjwa huu. Na ili kinga hii iwe thabiti, ni
lazima kukamilisha awamu zote za chanjo kulingana na muongozo wa njano hii.
“Usiku
ule tuli lala na kuamka salama asubuhi….lakini hakuna hata mmoja kati yetu alie
hisi kuwepo kwa hali tofauti kiafya kwa mtoto wetu….. nikana kwamba siku hii
ilikuwa nyeusi tii, yenye giza nene isio
na huruma wala tumaini hata kidogo….saa chache tu baada ya kupambazuka asuhi,
historia ya furaha iligeuka kuwa ya huzuni,,, sitaisahau siku hii, hakika
nikumbukizi yenye uchungu”Maneno hayo yalisemwa na Steloy Jaiso.
UTAMKINGAJE MTOTO DHIDI YA HOMA YA INI?
“Njia za kujikinga na athari za homa ya ini
kwa watoto, ni kupima mama wajawazito na kuwapa chanjo na matibabu na watoto
wao mara tu wakijifungua, kujikinga na kuchangia vitu vya ncha kali, kupatiwa
damu yenye maambukizi na kuwa na taadhari kwa njia zote za maambukizi” Dkt.
Ngasongwa
Matibabu ya
homa ya ini kwa watoto, kama imegundulika mapema na kuanza matumizi ya dawa hupona,
Dawa atakazo tumia ni kuliingana na shida ya mtoto kama za kuzuia kutapika,
kupoza homa, lishe bora na kupumzisha mwili.
Kuna mionzi
(chemotherapy) kulingana na steji ya saratani ya ini Kuna kupandikiza ini
(liver transplant), Lishe bora , kula mlo kamili na kupumzika vya kutosha, Mara
tu anapoona dalili tu apelekwe hospitali kupata ushauri na matibabu sahihi.
JE HOMA YA INI HUTOFAUTIANA?
Dkt. Hawa Ngasongwa“Ndio, kuna aina ya homa ya ini inapona
haraka tu na hata bila matibabu, kuna zingine hupelekea kusinyaa kabsa kwa ini
(liver cirrhosis )na kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi, na unaweza umwa tena
homa ya ini baada ya kupona ikisabbaishwa na mambo mbalimbali”.
TUREJEE TENA KWA NENKA BRYIYO
Kwa mujibu wa maelezo ya Bryiyo Mkoma baba mzazi wa mtoto anasema, baada ya
miezi kadhaa Nenka Bryiyo nuru
ilianza kuonekana katika afya yake akapata nafuu hatimae kupona, msichana
huyu alivutiwa na huduma za afya
kutokana na namna madaktari walivyo kuwa wakihangaika kwa upendo na upole
kuokoa uhai wake. Hapo ndipo wazo la kuwa mtaalamu wa afya ili aweze kusaidia
wengine walio katika hali kama aliokuwa nayo lilipo chipua. Baada ya kurejea Shuleni na kuendelea na masomo yake kama
kawaida, alijifunza na kuweka bidii kwenye masomo ya afya, na anaendelea vizuri.
Historia ya mtoto Nenka ilikuwa moja ya changamoto kubwa kurejesha afya yake ya awali,
lakini pia ni historia ya nguvu, ujasiri, na yenye matumaini. Alipitia wakati
mgumu katika maisha yake, lakini kupitia juhudi za Madaktari, wazazi wake, walibadilisha
maisha yake na kurejesha furaha maishani mwake na katika familia na jamii yake
maana kwa pamoja walionyesha umuhimu wa mshikamano ili kuleta matokeo chanya.
MTAZAMO WA DAKTARI NA WAZAZI KUHUSU HOMA YA INI
NI UPI?
Dkt. Hawa Ngasongwa anasema wazazi/walezi wachukue hatua mara baada tu ya kuona hali
tofauti kwa watoto wao isio ya kawaida, wapelekwe kwenye vituo vya avya ili
wataalamu wakawanyie uchunguzi na kuanzishiwa matibabu kwa ushauri na kwa
maelekezo ya mataalamu wa afya. Kwa kufanya hivyo magonjwa yote yaweza kutibika
kama sio kuzuilika yasiendelee na kumathiri mtoto.
“Sisi
hatukusita baada ya kuona hali ya mtoto wetu imebadilika kwa siku hiyo, nilicho
mwambia mke wangu chukua bima na umbebe mtoto mgongoni twende kituo cha afya
kwa ajili ya kumfanyia vipimo mwanetu. Mimi pia nili beba baisikeli na
kuwapakiza kuelekea kituo cha afya, hivyo wazazi wenzangu kuna haja ya
kukimbilia kituo cha afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watoto wetu, kama
ambavyo sisi tulifanya na tumejionea matokeo yake” Bryiyo Mkoma.