By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
Tanzania Kids Time
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Mazingira
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Wasiliana Nasi
Reading: VIJANA WENYE ULEMAVU NA ELIMU YA AFYA YA UZAZI:
Share
Notification Show More
Latest News
Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
TANZANIA WILL HOST CIGOFA4 TO FIND CONCRETE SOLUTIONS FOR YOUTH LAND QUESTIONS
Editor's Pick
Aa
Aa
Tanzania Kids Time
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi
  • Contact
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Tanzania Kids Time > Blog > Afya > VIJANA WENYE ULEMAVU NA ELIMU YA AFYA YA UZAZI:
Afya

VIJANA WENYE ULEMAVU NA ELIMU YA AFYA YA UZAZI:

Tanzania Kids Time
Last updated: 2024/01/29 at 2:30 PM
By Tanzania Kids Time 8 Min Read
Share
SHARE

Na, John Kabambala: Hebu
tafakari…..ikiwa mtu wa kawaida usie na ulemavu unao onekana….unapata
changamoto ya kuelewa nini maana ya afya ya uzazi…na yawezekana kabisa hujui
inatolewa wapi na ufanyeje ili uipate… je, vijana wakike na wakiume wenye
ulemavu tena maisha yao yote nikushinda nyumbani au kwenye vituo vya kulelea
watoto wenye mahitaji maalumu wataipataje….?.

Top of Form

Makala
hii inaangazia jambo hili muhimu kwa vija balehe katika mkoa wa Morogoro,
ambapo utasoma kilicho zungumzwa na vijana wenyewe kutoka kwenye vituo vya
kulelea watoto na vijana wenye mahitaji maalumu,Taasisi za vija wenye makao
makuu yake mjini Morogoro,  pamoja na Daktari bingwa wa masuala ya afya ya
uzazi kutoka hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro.

Hadi
leo, elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wenye ulemavu wa viungo nchini Tanzania
imekuwa ikipuuzwa au kupewa kipaumbele kidogo, hili likiwa mojawapo ya makundi maalum
yenye nahaki pia ya kuelimishwa jambo hili. Hii imekuwa changamoto kubwa inayowakabili
vijana hawa walio nahaki sawa na wenzao wasio na ulemavu kupata elimu na habari
muhimu kuhusu afya ya uzazi.

Mara
nyingi, vijana wenye ulemavu wa viungo wanakabiliwa na unyanyapaa na ubaguzi
kutoka kwa baadhi ya wanajamii hili nijambo lisilo fichika. Hata hivyo baadhi ya watu
huamini kuwa watu wenye ulemavu hawana haki au uwezo wa kujihusisha na masuala
ya ngono na afya ya uzazi. Hii inaweza kusababisha kukosa kujitambua na haki za
kijinsia kwa vijana hawa, na hivyo kupuuzwa kwa elimu ya afya ya uzazi.

Katika
maeneo mengi, vijana wenye ulemavu wanakabiliwa na uhaba wa rasilimali za elimu
na huduma za afya. Hii inaweza kuwa kutokana na ukosefu wa miundombinu
inayowafaa, vifaa vya kujifunzia na kufikia habari, na hata wataalamu wa afya
walioelimika kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa njia inayofaa.

Vijana
wenye ulemavu hawapati elimu muhimu ya afya ya uzazi katika shule au katika
jamii yao. Hii inaweza kuwa kutokana na kutokuwepo kwa programu za elimu ya
afya ya uzazi zinazojumuisha mahitaji yao maalum, au hata kutokana na wataalamu
wa afya kutokupata mafunzo yanayowawezesha kutoa elimu kwa njia inayofaa kwao.

Kwa
muktadha huo wa changamoto nyingi zinazokabiliwa na vijana wenye ulemavu, wakati
mwingine elimu ya afya ya uzazi huonekana kuwa kipaumbele cha chini kabisa,
hasa wanao ishi kwenye familia zenye kipato cha chini na hata wanao inshi
kwenye vituo vya kulelea watoto na vijana wenye mahitaji maalumu. Mambo kama
upatikanaji wa elimu bora, huduma za afya, na haki za msingi mara nyingine
hayapewi kipaumbele zaidi. Hii inaweza kusababisha kupuuzwa kwa umuhimu wa elimu
ya afya ya uzazi.

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya
ya jamii, afya ya uzazi kwa vijana wa rika balehe ni muhimu mno elimu hii, kwani
katika kipindi hiki vijana hukabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo mimba
za utotoni, magonjwa, na utoaji mimba usio salama, ambapo bila elimu muhimu
kutolewa zinaweza kuhatarisha maisha na ustawi wao.

Bi. Linda Ngido ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mehayo Centre for
Disabled Young People, kituo kinachojihusisha na kuwapatia ujuzi na fursa
vijana wenye ulemavu ambaye ameiambia Tanzania
Kids Time
 kwenye mahojiano maalum kwamba hajawahi kuona wataalamu
wa afya ya uzazi kutoka serikalini au kwenye asasi za kiraia kufika kituoni
hapo kwa ajili ya kutoa elimu ya afya ya uzazi.

“Kuna wakati ambao wasichana
wanafikia umri wa kupata hedhi, ukimuelekeza binti mwenye ulemavu kuhusu
kutumia vifaa vya kujistiri hawataki,” anaeleza
Bi, Ngido ambaye ni mwalimu kitaaluma. “Wakati mwingine
wanavitupa.”

Bi, Ngido haelewi ni kwa nini Serikali
na wadau hawajikiti kwenye kuwapatia vijana wa rika la balehe wenye ulemavu
elimu ya afya ya uzazi wakati watu hawa pia ni binadamu kama walivyo watu
wengine ambao hukua na kuanzisha familia zao.

“Watoto wenye ulemavu nilioanza
kuwa nao kwenye kituo hiki, wavulana na wasichana, sasa hivi ni watu wazima,
wameoana wenyewe na wana watoto wanasoma,” anaeleza Ngido ambaye alilazimika kuacha kazi yake ya ualimu kufanya kazi
yake ya sasa. “Kwa hiyo, siyo kwamba hawa watu wenye hali hii hawawezi kuwa na
familia. Hapana, wanaweza.”

Tanzania Kids Time ilitembelea kituo kingine kijulikanacho  Erick Memorial Foundation for Education and
Rehabilitation for the Disabled (EMFERD)
kituo hiki kipo mkoani Morogoro kinajihusisha na kutoa huduma kwa watoto na
vijana wenye ulemavu.

Hapa na kutana na baadhi ya vijana wanao lelewa kwenye kituo hiki,
wengi wao wako katika rika balehe ambao ni wenye ulemavu, walikiri kwamba
hawajawahi kufikiwa na kupatiwa elimu ya afya ya uzazi, kutoka kwa wataalamu wa
afya serikalini au Taasisi zingine za kiraia hali ambayo wanasema
inawasononesha na kuwatenga na jamii.

“Hii huduma tunaihitaji kwa sababu watu wenye ulemavu nao wana
haki zote za msingi kama vile ya] kuoa au kuolewa,” Benedict Mwenyasi, kijana mwenye ulemavu wa viungo kutoka EMFERD,
aliiambia Tanzania Kids Time, “[Wadau] sisi wanatusahau
[kutupatia elimu hii].”

                                   
Je,wadau wanaizungumziaje
Serikali kushirikiana na wadau wengine wa afya ya uzazi nchini Tanzania kuweka
mikakati na kuchukua juhudi za pamoja za kuhakikisha kwamba kundi hili nalo
linafikiwa kwenye utoaji wa elimu ya uzazi nchini.

Moja kati ya wadau hawa ni Obed Mtagulwa, mwanzilishi mwenza na
Mkurugenzi Mtendaji wa Care Youth Foundation, shirika linalojihusisha na kutoa
elimu ya uzazi kwa vijana rika balehe.

“Hizo sehemu wanazokaa watu
wenye mahitaji maalum huwa tunaenda kwa ajili ya kutoa huduma ya misaada pekee
yake, bado hatujafika kupeleka elimu ya afya ya uzazi,” anakiri Mtagulwa. “Kuna haja kubwa sana ya
kuwapa elimu [watu hawa].”

Nikabisha hodi ofisi yam ganga
mkuu wa mkoa kitengo cha afya ya uzazi nakutana na daktari bingwa wa afya ya
uzazi Hospitalini hii ya rufaa Morogoro Dkt.
Deodata Ruganuza
yeye anaanza kwa ameonya
kwamba endapo wadau hawataweka kipaumbele kwenye kuwapatia watu wenye ulemavu
elimu ya afya ya uzazi haki za msingi za watu hao zitakuwa hatarini kukiukwa.

“Tusipoweka kipaumbele katika hili kundi, [vijana walemavu walio
katika rika balehe] watakuwa wanakosa kitu cha muhimu sana kwao na kwa familia
zao watakazoanzisha,”

Ni
haki ya kila kijana, bila kujali ulemavu wake, kupata elimu sahihi kuhusu afya
ya uzazi. Elimu hii inawawezesha kujitambua, kujilinda na kujiamulia katika
masuala yanayohusu miili yao. Ni muhimu kwa jamii kuondoa unyanyapaa na
ubaguzi, kuimarisha upatikanaji wa rasilimali za elimu na huduma za afya, na
kuhakikisha kuwa elimu ya afya ya uzazi inatolewa kwa njia inayojumuisha
mahitaji ya vijana wenye ulemavu.

Hii
itasaidia kujenga jamii yenye uelewa zaidi na yenye haki kwa kila mmoja,
Dk
Ruganuza
aliiambia Tanzania
Kids Time
 kwenye mahojiano maalum yaliyofanyika ofisini kwake mjini
Morogoro.

 

You Might Also Like

THROUGH MZF NOW TRADITIONAL BIRTH ATTENDANCE THEY IMPROVE WOMEN’S WELL-BEING FOR SAFE DELIVERY

TOWARDS TEN YEARS OF MILELE ZANZIBAR FOUNDATION, READ THE ACHIEVEMENTS OF THE SHEHIA PROJECT

MABADILIKO YA HALI YA HEWA NITISHIO LINALOWAKABILI WANAWAKE WAJAWAZITO NA WATOTO.

MTI WA MATUMAINI WA ZINDULIWA ARUSHA: UNICEF

LISHE BORA NI MTAJI: NIMUHIMU KUWEKEZA KWA WATOTO,FAO:

Tanzania Kids Time August 15, 2023
Share this Article
Facebook Twitter Email Print
Previous Article THE FINDINGS OF THE ADAPT PROJECT IN TANZANIA.
Next Article UMUHIMU WA MALEZI JUMUISHI KWA WATOTO:
Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

Facebook Like
Twitter Follow
Youtube Subscribe
Telegram Follow
- Advertisement -
Ad image

Latest News

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
//

Tanzania Kids Time: A platform spotlighting children’s and women’s issues in Tanzania, focusing on education, health, and environmental conservation.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

© 2023 Tanzania Kids Time. Powered by Digital Media Innovation Program. All Rights Reserved.

Join Us!

Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..

Zero spam, Unsubscribe at any time.

Removed from reading list

Undo
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?