Na, John Kabambala.
miaka mitano ambao wanapatikana kwenye nchi zenye uchumi wa chini na zile zenye
uchumi wa kati amba wapo kwenye hatari ya kutokufikia hatua zao za ukuaji.
Picha hii nikutoka nyaraka ya – MMMAM:
Takribani robo tatu sawa na asilimia 66 ya watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano walio kusini mwa jangwa
la Sahara wapo kwenye hatari ya kutokufikia hatua timilifu za ukuaji kutokana
na kukosa malezi bora, umasikini, utapiamlo pamoja na matatizo mengine ya
kijamii na kiuchumi.Hatahivyo mwandishi mmoja aliwahi kusema “Kila
mtoto ni kitabu cha kurasa tupu, sisi ni waandishi wake wa kwanza”
mwisho wa kumnukuu.
Ndugu msomaji nikukaribishe kwenye makala hii muhumu itakayo kusogeza
karibu kumtafakari zaidi mtoto, jinsi anavyo paswa kulelewa, kutunzwa,
kuelekezwa na kufundishwa, nina hakika hauta jutia muda wako maana wewe
utachukua hatuadhidi ya jambo hili.
Kwa mujibu wa
Takwimu za Taifa za Idadi ya Watu za mwaka 2022 Tanzania ina takribani watoto 16,694,763
(wavulana 8,329,725 Na
wasichana 8,365,038)
wenye umri wa miaka 0 – 8 (sawa na 27.0%
ya watu wote). Hii inamaanisha kuwa katika kila watu wawili, kuna mtoto
mmoja mwenye umri wa miaka 0 – 8.
Kundi hili la watoto wadogo linahitaji kuangaliwa kwa karibu na
kufanyiwa uwekezaji ili waweze kuwa rasilimali bora yenye tija kwa familia na
taifa. Uwekezaji unaopaswa kufanyika ni pamoja na kukabiliana na tatizo la
udumavu, kuwapa huduma bora za malezi ya awali na programu za elimu ambazo zitawawezesha kukua na kufikia ukuaji timilifu na
hatimaye kuwa watu wazima wenye uwezo wa kufanya kazi za uzalishaji mali kwa
tija na hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania pamoja na kujenga jamii
yenye amani na utulivu.
Hadi sasa maendeleo ya mtoto hayajapewa uzito unaostahili, badala yake
msisitizo umewekwa kwenye kupunguza vifo licha ya kwambakipindi cha miaka 0-8
ni fursa muhimu ya kuboresha maendeleo ya binadamu na hivyo kupata mtaji bora
wa rasilimali watu yenye tija. Pia ifahamike kwamba, kukosekana kwa fursa za
ukuaji kwa watoto wenye umri huo kunaweza kusababisha changamoto katika maendeleo
yao ambayo yanaweza kuathiri kizazi na kizazi.
Katika kuyafahamu mengi zaidi kuhusu idara hii muhimun kwenye jamii
nime mtafuta Ndg. Bruno Ghumpi kutoka Taasisi ya Tanzania
Early Childhood Development Netwark (TECDEN) mbali nakuzungumzia hatua na jitihada mbalimbali katika
kutatua changamoto za Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM).
Ndg. Bruno Ghumpi amesema
jamii ya kitanzania inajukumu sasa la kukumbuka ulazima na umuhimu wa
kuzingatia Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto, kwa kufanya hivyo
taifa litakuwa na uhakika wakuwa na wanachi wenye ustadi na weledi wa pekee,
wabunifu na wenye maarifa ambayo yatalinufaisha taifa kipindi cha uhai wao.
Ikumbukwe kwamba miongoni mwa miongozo iliyoandaliwa ni ule wa malezi
jumuishi uliozinduliwa na Shirika la Afya Duniani WHO mwaka 2018 ambao una maono kuwa na“Dunia ambayo mtoto anaweza kufikia
hatua zake za ukuaji na hakuna mtoto atakaeachwa nyuma” Mfumo huu wa malezi jumuishi
unatoa mwongozo sahihi kwa nchi mbalimbali kuwekeza kwenye hatua zote za ukuaji
wa Mtoto.
Tanzania ni moja ya nchi zenye uchumi wa kati wa chini, ambapo
asilimia 43 ya watoto wapo kwenye hatari ya kutokufikia hatua timilifu za ukuaji
na maendeleo kutokana na viashiria vya hatari mbalimbali vya maendeleo kama
vile utapiamlo, umasikini, kukosekana kwa uhakika wa chakula, msongo wa kifamilia, miundombinu duni na uhaba wa
rasilimali pamoja na utelekezaji na unyanyasaji wa watoto.
Vilevile wazazi au walezi kutokuwa karibu na watoto wao suala ambalo
linachangiwa na kukosekana kwa uelewa wa kina wa MMMAM.Programu za malezi
jumuishi nchini Tanzania zinahitaji kupewa kipaumbele na msisitizo kutokana na
kukosekana kwa uratibu mzuri na zinatekelezwa kama sehemu za program za kisekta
au tafiti zinazofanywa na wadau zikilenga baadhi ya umri wa watoto na kutekelezwa
kwenye maeneo machache.
Kutoka Wilayani Kilosa nimezungumzana na Frida Jemes mwenye mtoto mmoja wakiume namuuliza, Swali: Utahakikishaje
kuwa mtoto atakuwa kwenye mazingira na malezi yanayo paswa yenye adabu na afya
bora? Bi,Frida Jemes:- “Hakika nimtihani mzito, masha yangu
yanategemea nitoke niende kutafuta ndipo kipatikane chakula na mahitaji mengine
ya muhimu, ijapokuwa sina uwezo wakutafuta na kumlipa dada wakazi kunisaidia
kumlea mwanangu. Kwa miezi tisa yote ile nilio vumilia nikaweza mikiki mikiki
yote ya utafutaji naamini hata kumlea nitaweza, staki kumpa mtumwingine
anilelee mwanangu ili afya yake hii alio zaliwa nayo isipotee.
Na kwa sababu mimi nina rafiki zangu nesi
na daktari hao ndio hua nawasumbua sana kuhusu maendeleo ya mwanangu ninavyo
ona mabadiliko tu, nimewafuata hukohuko kwenye vituo vyao vya kazi, nilikuwa
nafanya hivyo pia wakati wa ujauzito wa huyu mtoto kwa hiyo sina hofu juu ya
malezi yenye adabu na afya bora kwa
mwanangu”.
Kwa mujibu wa nyaraka ya Mfumo wa Malezi Jumuishi inaonesha kwamba,
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa MMMAM imeandaa Programu
Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto itakayo tekelezwa
kwa kipindi cha miaka mitano (2021/22-2025/26). Programu hii ilianzishwa chini
ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa wati ule.
Aidha mpango huu umelenga kutatua changamoto za ukuaji na maendeleo ya
watoto wenye umri wa miaka 0-8. Programu hii itatoa mchango katika kufanikisha
Mpango wa tatu wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano 2021/22 – 2025/26 kwa
kutambua kwamba watoto ambao wanakosa kufikia kikamilifu hatua za ukuaji ni
changamoto kwa maendeleo ya taifa na tishio kwa malengo ya kiuchumi na kijamii
ikiwa ni pamoja na kujenga nchi ili kufikia uchumi wa kati.
Kutokana na sababu hizo, programu hii imelenga kuwekeza moja kwa moja
kwenye maendeleo ya watu ili kuharakisha upatikanaji wa atokeo chanya ya
maendeleo ya awali ya mtoto kwa kuhimiza ushiriki wa sekta mbalimbali katika
kutoa huduma za malezi jumuishi yenye vipengele vitano:Vya afya bora kwa mtoto na mama/mlezi; lishe ya kutosha kuanzia
ujauzito; malezi yenye mwitikio; fursa za ujifunzaji wa awali; ulinzi na usalama
kwa watoto.
Programu Jumuishi ya Taifa ya MMMAM inatakiwa izingatiwe na afua zote
za malezi zitekelezwe kwa ujumuishi kwa kuwa inalenga kuleta matokeo chanya
katika ukuaji na maendeleo ya awali ya mtoto na kufikia maono: “Watoto wote
Tanzania wapo kwenye mwelekeo sahihi wa kufikia ukuaji timilifu”.