Na, John Kabambala.
Ulipozinduliwa, ulikuwa ni kama mwanga mdogo uliowaka kwenye
giza la usawa wa kijinsia na elimu nchini Tanzania. Mradi wa “Dunia Yangu
Bora” uliotekelezwa na Shirika la CAMFED ulianza kama ndoto. Ndoto ambayo
ilikuwa na nia ya kuwawezesha wasichana wa vijijini kutimiza ndoto zao za elimu
na kuinua hadhi zao katika jamii. Hebu tuwe mashahidi wa makala hii ya
mafanikio ya mradi huu kupitia macho ya wasichana wa Tanzania.
Ilikuwa asubuhi na mapema, barabara za kijijini zilijaa furaha
na matumaini. Tuliokuwa tunaitwa “Washiriki wa Mradi wa Dunia Yangu
Bora” Programu ambayo ilijikita kuwezesha Stadi za Maisha, kumbe walikuwa wanawake wa kesho, wasichana wadogo wa vijijini walio
na ndoto kubwa. Walifika kwenye shule wakiwa na vijitabu vyao na mioyo yao
iliyojaa shauku ya kuya ona matumaini mapya kama wenzao waliokuwa shuleni.
Zamoyoni Selemani
alikuwa miongoni mwa wasichana waliochangamka sana. Kwa mara ya kwanza alipokuwa akipitia mlango
wa shule, alihisi kama ameingia kwenye ulimwengu mpya. Na hapo ilikuwa ni baada ya kuhitimu masomo yake, na sasa kuanza mpango wa kujitolea kuwafundisha wasichana na wavulana shuleni mambo ya Stadi za Maisha.
MSAADA WA SHIRIKA LA CAMFED
Shirika la CAMFED nchini Tanzania ni moja ya mashirika
yanayopambana kuhakikisha yanachangia katika kutimiza malengo ya 17 ya maendeleo
endelevu ya Umoja wa Mataifa yaani SDGs, Lengo namba 4 linazungumzia elimu
bora na lengo namba 5 linazungumzia usawa wa kijinsia, yote hayo yakiwa
yanalenga kutomwacha nyuma mtu yeyote katika maendeleo ya ulimwengu ifikapo
mwaka 2030.
Shirika hili la CAMFED lilileta matumaini kwa wasichana kama Zamoyoni
Selemani mmoja kati ya wasicha walionufaika na mpango wa Stadi za Maisha ulio anzishwa na Shirika
hilo, ulio kuwa ukijulikana kama “Dunia Yangu Bora” liliwasaidia wasichana na hata wavulana, kuwezeshwa elimu ya Stadi hizo za Maisha, na wo waendelee kujitolea kwenye jamii yao, pamoja na hayo, CAMFED ilianzisha vikundi vya wasichana shuleni
ambavyo vilijengewa ujasiri wa uongozi miongoni mwa wasichana hao.
MIONGONI MWA
WANUFAIKA WA MRADI HUU WANASEAMAJE?
Asha ni mnufaika
wa mpango huu wa kujitolea kufundisha vija Stadi za Maisha Shuleni na sasa amekuwa muelimishaji maarufu anayewasaidia wengine kama yeye ambavyo alisaidiwa, kutokana na sababu mbalimbali wamejikuta wakiishi katika mazingira magumu. Asha
anasema, “mimi kama msichana nimepitia huko kwa sababu baada ya
kumaliza elimu yangu ya sekondari, baba alikuwa na matatizo yaliyompelekea
kuugua kwa muda mrefu. Kwa hivyo ikanibidi niende kutafuta kazi,
nikaajiriwa.”
Mpango huu wa Stadi za Maisha na uelimishaji lika kupitia “Dunia Yangu Bora” ulibadilisha maisha ya
wasichana hawa wa Tanzania. Kupitia elimu, wasichana walianza kuona fursa
nyingi zaidi. Walijifunza kuhusu afya, haki zao, na jinsi ya kusimama kidete
dhidi ya ubaguzi na unyanyapaa uliokuwa ukifanywa kwenye jamii yao dhidi ya
wasichana. Walijenga ujasiri wa kuwa viongozi wa kesho na kuchangia katika
maendeleo ya jamii zao.
ZAMOYONI AMENUFAIKAJE NA SHIRIKA LA CAMFED?
Mbali na elimu alio ipata kupitia uwezeshaji mwingine wa Shirika, alipata elimu ya Stadi za Maisha kupitia mpango wa “Dunia Yangu Bora” uliokuwa ukitekelezwa
na Shirika la CAMFED Tanzania ulikuwa kama jua linalong’aa katika maisha ya msichana huyo, kama ambavyo Zamoyoni
Selemani alivyo pata nafasi ya kufanya kazi kama mratibu wa miradi ya Shirika hilo kwa Wilaya
mbil ikiwemo Wilaya ya Kilosa na Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro, na hapa
anelezea zaidi.
“miradi yetu
imejikita sana katika kumsaidia mtoto wa kike, katika elimu yake lakini
hatuishii katika elimu. Vilevile kwa mto wa kike ambaye ameshamaliza shule,
tunamwendeleza katika vyuo vya ufundi, lakini pia tunawapeleka katika vyuo vya
kati, ngazi ya cheti na diploma, lakini pia wale ambao hawana sifa za kwenda
vyuo tunawapa miradi ambayo wanaweza wakafanya biashara zao katika kata zao,
hii yote ni kuhakikisha kwamba mtoto wa kike hawezi kuwa tegemezi katika
mazingira ya sasa.” Alisema Zamoyoni Selemani.
Kupitia macho yao, tunajifunza kuwa kutoa fursa sawa za
elimu na Stadi za Maisha kwa wasichana ni uwekezaji katika mustakabali bora wa jamii na taifa kwa
ujumla. Mpango huu ulibadilisha maisha ya wasichana hawa na kuwapa matumaini na
ujasiri wa kusimama na kuchukua hatamu za maisha yao. Hii ni simulizi ya
mafanikio, na ni matumaini yetu kuwa jitihada za kuwawezesha wasichana
zitaendelea kuangaziwa na kusaidiwa ili kujenga dunia bora kwa wote.
TUSIKIE KUTOKA KWA MWALIMU MSIMAMIZI WA MPANGO HUO SHULENI:
Elisifa Nasali ni mwalimu katika Shule ya sekondari Kimamba na
pia ndiye mlezi wa wanafunzi wanufaika wa mradi wa CAMFED anasema, wengi kama Zamoyoni
na Asha wamenufaika lakini uhitaji bado ni mkubwa, “watoto ni wengi ambao wana shida. Ingewezekana
tungeongezewa hata namba ya watoto ambao wangepata msaada Wasichana wengi walionufaika na mradi wa
“Dunia Yangu Bora” uliotekelezwa na Shirika la CAMFED Tanzania
walipata msaada mkubwa ambao ulibadilisha maisha yao kwa njia nyingi muhimu” alisema Mwalimu.
Aidha Mwl. Nasali
alisema mradi huu ulitoa ufadhili wa elimu kwa wasichana ambao uliwawezesha
kulipia ada za shule, kununua vifaa vya shule, na kufidia mahitaji yao ya kila
siku. Ufadhili huu ulikuwa kama daraja lao kuelekea elimu bora na fursa za
kujifunza. Wasichana walinufaika na vifaa vya shule kama vile vitabu, sare za
shule, na vifaa vingine muhimu. Hii iliwawezesha kushiriki kikamilifu kwenye
masomo bila kikwazo chochote.
SHIRIKA LILI WAFANYIA
NINI KINGINE?
CAMFED ilianzisha vikundi vya wasichana shuleni ambavyo
vilikuwa na malengo ya kuwajengea ujasiri, kuwafundisha kuhusu haki zao, na
kuwawezesha kuwa viongozi katika jamii zao. Wasichana walipata mafunzo ya
kuendeleza ujuzi wa maisha kama vile stadi za ujasiriamali na uongozi. Mradi
ulitoa ushauri na msaada wa kisaikolojia kwa wasichana. Hii ilikuwa muhimu
katika kuwasaidia kukabiliana na changamoto za kibinafsi na za kijamii ambazo
zinaweza kuwa na athari kwa masomo yao.
CAMFED ilifanya kazi na jamii kubadilisha mitazamo kuhusu
elimu ya wasichana. Wasichana waliwezeshwa kusimama kidete dhidi ya ubaguzi wa
kijinsia na unyanyapaa wa kijamii unaoweza kuwazuia kufikia ndoto zao. Baadhi
ya wasichana walinufaika na ufadhili wa kuanzisha miradi midogo midogo ya
kujiajiri. Hii iliwawezesha kujifunza stadi za ujasiriamali na kuwa na njia
mbadala za kujipatia kipato.
Kupitia msaada huu, wasichana waliweza kusoma bila vikwazo
vikubwa, kujenga ujasiri na uongozi, na kushiriki kikamilifu katika maendeleo
ya jamii zao. Walipata fursa za kutimiza ndoto zao na kuwa nguvu ya mabadiliko
katika jamii zao na taifa kwa ujumla. Mpango wa “Dunia Yangu Bora”
ulikuwa mwongozo wa maisha yao na kichocheo cha mafanikio yao.
Hakika CAMFED wasichana
wote walionufaika kupitia mpango huu hawata kusahau: