Na, John Kabambala:
Mpango Mkakati wa Taifa wa Afya Moja nchini Tanzania ni kama hadithi
ya matumaini vile, inayo lenga kuokoa maisha ya jamii ya watanzania. Ni hadithi
inayojumuisha juhudi za serikali na wadau wa afya kuleta mabadiliko chanya
katika afya ya jamii ya kitanzania.
Tanzania ni nchi ya Afrika Mashariki katika Ukanda wa Maziwa Makuu,
inayojumuisha jumla ya eneo la maji na nchi kavu lenye kilometa za mraba
947,303, ambapo kilometa za mraba 886,040 zinajumuisha ardhi na kilometa za
mraba 62,050 zinajumuisha maji (Lake , 2013).
Umewahi kusikia neno,“AFYA MOJA”Unadhani nikitu gani?
Yamkini umewahi kushiriki kuandaa mpango huu, kusoma maeneo mbali
mbali au hata kuusikia ukizungumziwa na wataalamu na viongozi katika ngazi
mbalimbali. Na baadae hukujua kilicho endelea namna ulivyo kamilika na kuanza kufanya
kazi au hukujua kabisa neno hili linahusu kitugani !!!!!.
Makala hii muhimu ya Afya itakusaidia kuufahamu vema mpango huu mkakati wa
Taifa unao husu “AFYA MOJA” jinsi ulivyo
kusudiwa kufanya kazi kwa Binadamu, Mazingira na Wanyama ni muhimu sana ili
kuchukua hatua stahiki.
matishio mengi ya afya ya jamii ni suala lenye changamoto na lenye sura nyingi,
kama ilivyodhihirishwa na mlipuko wa UVIKO – 19, Mnamo Mwaka 2020. Usimamizi na
ukabilianaji wake kwa ufanisi unahitaji njia na hatua nyingi shirikishi na uratibu
endelevu wa sekta mtambuko.
Mwingiliano miongoni mwa binadamu, wanyama, na mazingira unaendelea
kubadilika siku hadi siku, na waliohatarini zaidi ni watoto wachanga, vijana
Mama wajawazito na hata Wazee wenye umri mkubwa zaidi. Hali ya ongezeko la
idadi ya watu na wanyama, mabadiliko ya tabianchi, matumizi ya ardhi na
kuongezeka kwa safari na biashara za kimataifa hutoa fursa za kuenea kwa magonjwa
kwa haraka zaidi.
Takriban asilimia 75 ya
magonjwa ya kuambukiza yaliyojitokeza hivi karibuni na kuathiri wanadamu
kiasili ni magonjwa ya wanyama; aidha, asilimia 60 ya vimelea vya magonjwa yote
ya binadamu hivi sasa inatokana na magonjwa yanayopatikana kwa mifugo. Hivyo
basi kutokana na hali hiyo hupelekea wanadamu hasa watoto wenye kinga ambazo
hazijawa imara zaidi kuwa hatarini kuambukizwa na kuugua na kupata ulemavu na
wakati mwingine kufariki.
HISTORIA YA
DHANA YA AFYA MOJA:
Afya Moja inajumuisha taaluma za afya, lakini pia inajumuisha
wataalamu mbalimbali kwa mfano wataalamu wa wanyamapori, wanaanthropolojia,
wachumi, wanamazingira, wanasayansi wa tabianchi na wanasosholojia.
Dhana ya Afya Moja ilitanguliwa na dhana ya ‘Dawa Moja’ ambayo ina
mizizi ya Kiafrika tangu miaka ya 1960, mtaalamu wa epidemiolojia wa Kimarekani Calvin Schwabe, akiwa anafanya kazi yake na wafugaji wa Dinka nchini Sudan
alianzisha neno ‘Dawa Moja’ kutokana na kufanana kwa dawa ya binadamu na ile ya
mifugo.
Katika miaka ya 1980, dhana ya ‘Dawa Moja’ ilibadilishwa na kupanuliwa
kuwa ‘Afya Moja’ ili kuakisi dhana ya afya kwa mfumo mzima wa ikolojia kama
ilivyoanzishwa na mashirika ya kimataifa: Shirika la Afya Duniani (WHO) na
Shirika la Chakula na Kilimo (FAO).
BARA LA AFRIKA MBINU YA AFYA MOJA ILIANZA KUTUMIKA LINI?
Barani Afrika, mbinu ya Afya Moja ilianza kutumika mwaka wa 2018
wakati programu ya Afya Moja ilipokubalika na Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia
Magonjwa (Africa CDC). Programu hii imezingatia masuala mtambuko ya afya
ya jamii ikiwa ni pamoja na usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawana magonjwa ya
zuonotiki kama maeneo ya kipaumbele.
Kwa mujibu wa Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) inasema Programu ya Afya Moja inajumuisha
kikundi kazi cha wataalamu wa Afya Moja (OH-TWG) chenye mgawanyiko ulio
na uwakilishi kutoka vitengo vitano vya kitaalamu ambavyo ni: ufuatiliaji na
intelijensia ya magonjwa, maandalizi ya dharura na kukabiliana na maafa,mifumo
ya maabara, taasisi za afya ya jamii,utafiti, udhibiti na uzuiaji wa magonjwa.
Wakati wa Mkutano wa 35 wa
Kawaida wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki uliofanyika mwaka 2017, iliamuliwa kwamba dhana ya Afya Moja itumiwe
na mataifa hayo na Jukwaa la Afya Moja la Jumuiya ya Afrika Mashariki
lianzishwe na kuwezeshwa kufanya kazi.
Mnamo mwaka wa 2019, Baraza la 19 la Kisekta la Mawaziri wa Afya wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki liliagiza Sekretarieti ya Jumuiya hiyo kuimarisha
ushirikiano na uratibu wa sekta mbalimbali kwa kuanzisha Mkakati wa Afya Moja
wa kikanda. Inatarajiwa kwamba kupitishwa kwa mkakati huu kutatoa mwongozo wa
utayari wa fani na sekta mbalimbali katika kujiandaa, kuzuia, kutambua na kukabiliana
na matishio ya afya ya jamii katika mipaka ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na
hatimaye kuboresha uratibu katika kukabiliana, kuzuia na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza
yanayohusiana na Afya Moja kwa wanadamu, wanyama na mazingira.
MPANGO WA AFYA MOJA TANZANIA UMEUNGWA MKONO LINI?
Nchini Tanzania, dhana ya Afya Moja, imeungwa mkono na sekta
mbalimbali, na ilikubaliwa kwa mara ya kwanza katika udhibiti wa mlipuko wa Homa ya
Bonde la Ufa mwaka 2007. Katika kipindi hicho, idadi ya mitandao na majukwaa
ya Afya Moja yaliundwa.
Haya ni pamoja na Kituo cha Kusini mwa Afrika cha kufuatilia Magonjwa
ya Kuambukiza (SACIDS), Mtandao wa Afya Moja wa Afrika ya Kati na
Mashariki (OHCEA), Muungano wa Utafiti wa Kiafrika wa Mfumo wa Mazingira na Afya
ya Idadi ya Watu (AfriqueOne) na Mitandao ya Kitaifa ya Afya Moja
ya Utafiti iliyoimarishwa ya Magonjwa ya Kuambukiza (NRN-Biomed), Kikosi Kazi cha
usistisekosi (Cysticercosis) katika Afrika Mashariki na Kusini (CWGESA) na Afya kwa Wanyama
na Maisha (HALI).
Mitandao hii na majukwaa mengi yalianzishwa kwa ushirikiano na wanasayansi
wa utafiti katika vyuo vikuu na taasisi za utafiti ili kukuza utafiti wa Afya Moja
na kutoa uthibitisho kwa watunga sera. Ajenda ya Kitaifa ya Afya Moja nchini Tanzania
ilibuniwa na kurasimishwa wakati wa Mkutano wa Pili wa Wanasayansi wa Afya Moja
pamoja na Taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu (NIMR) uliofanyika mwaka
2013.
Milipuko ya magonjwa ambayo hupunguza upatikanaji wa
wanyama hai na mazao ya mifugo inaweza kupunguza mapato ya kaya, kudhoofisha
mlo wa wanakaya, kudhoofisha hali ya lishe na kuongeza hatari kwa afya, hasa
kwa wanawake na watoto.
Hata hivyo, milipuko inaweza kudhoofisha upatikanaji wa
soko kwa bidhaa hizo. Ukosefu wa usalama wa chakula kwa muda mrefu pia
husababisha tabia hatarishi zinazohusiana na upatikanaji wa nyama, mfano hakuna
mtu ambaye ana uhakika wa usalama wa chakula angefikiria kula mzoga. Madhara ya
magonjwa ya wanyama yanaenea kwa wafanyakazi wanaofanya kazi za uzalishaji na
uchakataji – kwa maao ya mifugo, kilimo, wasafirishaji, na wauzaji. Hivyo
nimuhimu kuzingatia mwingiliano kati ya wanyama na makaazi ya binadamu, ili
kuepusha ongezeko la mlipuko ya magonjwa.