Na, John Kabambala:
Tukio
la mwezi Julai mwaka 1996 lililo tokea Mkoani Mtwara, kumuhusu Issa Ibrahim halitasahaulika kamwe, lilikuwa la mwisho na likaiweka
Tanzania kwenye nafasi ya kufunga ukrasa wa kuwa na wagonjwa wa Polio, hali hii
iliifanya nchi kupeperusha bendera ya hakuna POLIO Tanzania.
Njoo nami kuyafahamu mengi zaidi kupitia Makala hii: Leo tunazungumzia Tatizo
la Ugonjwa wa Polio, Chanzo na Suluhisho lake nchini
Tanzania, karibu usome Makala hii naamini hautajutia muda wako, maana utapata
mambo mapya kuhusu POLIO kwa watoto
ambao ndio wahanga wakubwa wa ugonjwa huu tunao uzungumzia leo. Yamkini
hukuwahi kuyasikia machache kati ya mengi nilio kuandikia kwenye Makala hii, kutoka
kwa alie wahi kuugua ugonjwa huo na wataalamu kutoka –WHO Tanzania.
Issa Ibrahim alikuwa kijana mchangamfu na
mwenye furaha, akicheza na marafiki zake kila siku. Hata hivyo, bahati mbaya,
siku moja Issa Ibrahim alianza kuhisi maumivu makali ya misuli, na muda mfupi
baadaye, alishindwa kutembea. Mama yake, alishtushwa na hali ya kijana wake na
haraka wakampeleka hospitalini.
Baada ya uchunguzi wa daktari, ilibainika kuwa Issa Ibrahim alikuwa ameambukizwa ugonjwa hatari wa polio. Ugonjwa huu
unaosababishwa na virusi unaweza kusababisha ulemavu wa kudumu au hata kifo. Issa Ibrahim alilazwa hospitalini kwa wiki kadhaa, akifanyiwa matibabu
ya kurejesha nguvu katika misuli yake. Ingawa alipata nafuu polepole, ugonjwa
wa polio uliacha athari za kudumu kwenye miguu yake, akibaki na ulemavu wa
kutembea.
Hapa anasimlia zaidi “Nilizaliwa
Wilaya ya Mtwara vijijini Mkoani Mtwara, wakati nikiwa na umri wa miaka mitatu
sikumoja nilienda uani kujisaidia sasa wakati ninarudi ghafla mguu wangu wa
kushoto ukaisha nguvu nikadondoka chini, nikajaribu kunyanyuka ikashindikana.
Basi nikapiga kelele za kuhitaji msaada.nikaita Mamaaa!!!!! Mama
alikuja alipofika nika mwambia nimeshindwa kutembea akaninyua akajaribu
kunisimamisha lakini mguu ukaanza kukakamaa na kuuma sana, akanibeba
akanipeleka ndani kunikalisha.
Basi!! Baadae hali ile hikurejea kwenye ukawaida wake baba alipofika
mama akamueleza jinsi ilivyo tokea mwanzo hadi mwisho, jambo la kushangaza baba
akasema huyu mtoto amelogwa sio ugonjwa wakawaida hakuna haja ya kumpeleka
hospitali huko nikupoteza muda na pesa, baba akawa anamwambia mama maneno hayo.
Mama hakunikatia tamaa sasa nimekuwa mtu wa kubebwa wakati wote au
wanapo niacha ndipo watakapo nikuta maana siwezi kunyanyua tena mguu na
kutembea, siku moja akanipeleka kituo cha afya nilipo pimwa ndio nikagundulika
nina polio, ila imeathiri muguu wataalamu wa afya wakamshauri mama niwe
nakisaidizi cha mkuu kwamaana ya kutembea na magongo” Alisema Issa Ibrahim.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya nchini Tanzania inatoa ufafanuzi
kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa polio kuwa ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi
ambacho huambukizwa kutoka kwa mtu aliyeathirika kwenda kwa mwingine, kwa kula
au kunywa kitu kilicho chafuliwa na kinyesi chenye virusi vya polio. Virusi vya
polio vinapoingia mwilini huathiri mfumo wa fahamu na kusababisha madhara ya
kiafya ikiwa ni pamoja na kupooza kwa ghafla kwa kiungo au viungo na hata
kupelekea kifo.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kwamba “Napenda nichukue fursa
hii kuwataarifu kuwa Wizara kwa kushirikiana na wadau wa afya UNICEF, WHO na HPS tutakuwa na
Kampeni maalum ya utoaji wa chanjo ya matone dhidi ya Polio (nOPV2) kwa watoto
wote wenye umri chini ya miaka nane (8). Kampeni hii itafanyika kwa siku nne
(4) kuanzia tarehe 21 – 24 Septemba, 2023 katika Mikoa sita (6) inayopakana na
nchi zenye mlipuko wa Polio ambayo ni Rukwa, Kagera, Kigoma, Katavi, Songwe na
Mbeya”
“Lengo la kampeni hii ni kuwafikia watoto 3,250,598 waliozaliwa
baada ya mwaka 2016 ili kuwakinga dhidi ya Kirusi cha Polio aina ya pili (Polio
Virus Type 2) kinachoweza kusababisha ulemavu wa kudumu. Kwa Mkoa wa
Rukwa tunatarajia kufikia watoto 391,883 Kagera 729,387 Kigoma 884,477 Mbeya
614,346 Katavi 227,862 na Songwe 402,643” amesema.
Dalili
za Ugonjwa huu wa Polio kwa Mtoto ni Zipi?:
Dalili za awali za ugonjwa wa polio ni pamoja na homa, uchovu,
maumivu ya kichwa, kutapika, kukakamaa shingo na maumivu ya viungo, na kundi
linalo athirika Zaidi ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano 8.
WAGONJWA
WA MWISHO WA POLIO WALIGUNDULIKA LINI HAPA TANZANIA:
Kwamujibu wa Dr. Anthony
Kazoka kutoka shirika la afya ulimwenguni (WHO) ofisi za Tanzania amesema. “Kwa
mara ya mwisho wagonjwa wa polio waligundulika kwenye mikoa mitatu ya Tanzania
bara, mgonjwa wa kwanza aligundulika tarehe 11 mwezi Julai mwaka 1996 Mkoani
Arusha, Mgonjwa wapili aligundulika tarehe 24 mwezi Julai mwaka 1996 Mkoani
Kigoma na mgonjwa wa tatu na wa mwisho aligundulika tarehe 30 mwezi Julai mwaka
1996 Mkoani Mtwara”.
MAENDELEO
YA ISSA IBRAHIM YAKOJE MPAKA SASA?
“Ninaendelea vizuri maana nilipona polio laikini iliniachia
maumivu makali kwenye mguu wangu wakushoto, siwezi kufanya kazi ngumu kwa muda
mrefu nikiwa nimesimama kunawakati ukifika unaisha nguvu ahata kama ninatembea
inabidi nisitishe safari nikae kwanza ukipoa ndio niendelee na safari”.
USHAURI
WAKE KWA JAMII NI UPI?
Ibrahim anaishauri jamii kulingana na uzoefu alioupata kupitia
ugonjwa wa polio tangu mwaka 1996 na kupatiwa matibabu, japokuwa amebakiwa na
ulemavu wa kupooza mguu hayo yote nilisimuliwa na mama yangu baada ya kufikia
umri wa kujitambua, “anasema wazazi/walezi wasije kuwa kama baba yangu alie
kata kunihudumia na kunipeleka hospitali akisema nimelogwa, hakikisheni
mnawapeleka watoto kupata chanjo kila wakati unapofika ilikuepuka ulemavu wa
kudumu na hata vifo wakati mwingine”.
ISSA
IBRAHIM YUPO WAPI KWA SASA?
Ibrahim kwa sasa anaishi Dar es Salaam kwa mama yake mdogo, ambapo
hivi karibuni Mh.Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amewaagiza watendaji wa Wizara
hiyo kumpatia kitengo ndani ya Wizara hiyo Nd.Ibrahim hususani kwenye kitengo
cha elimu kwa umma ilikuendelea kuhamasisha chanjo ya polio nchini.
HALI
YA MLIPUKO WA UGONJWA WA POLIO KWA SASA IKOJE TANZANIA?
Dr.
Anthony Kazoka amesema tangu mwaka 1996 hakuna kisa chochote cha mgonjwa
wa polio nchini, na hii nikutokana na jitihada za serikali kupitia Wizara ya
afya kwa kushirikiana na shirika la afya ulimwenguni (WHO) ofisi za Tanzania
kuhakikisha wanadhibiti mlipuko huo kwa kuanzisha kampeini za utoaji chanjo kwa
watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Visa vya polio vimepungua kwa zaidi ya 99% tangu 1988, kutoka
wastani wa visa 350,000 kwenye zaidi ya nchi 125 zenye ugonjwa huo hadi visa
175 vilivyoripotiwa mnamo mwaka 2019 duniani kote wakati huo Tanzania kukiwa
hakuna kisa chochote cha polio tangu mwaka 1996, hatua iliyosababisha- WHO
kanda ya afrika kuiweka Tanzania kwenye orodha ya nchi zilizo tokomeza mlipuko
huo wa polio na kubakia kwenye nchi za Pakistan na Afghanistan.
SULUHISHO
LA UGONJWA HUU NI CHANJO YA POLIO:
Kwa bahati nzuri, suluhisho la ugonjwa wa polio liko na limekuwa
likifanya kazi kwa mafanikio kote ulimwenguni – ni chanjo ya polio. Chanjo hii
ni ya kuaminika na salama na inatolewa kwa watoto wachanga kwa awamu kadhaa.
Inalinda dhidi ya aina tatu za virusi vya polio na imekuwa ikipunguza kesi za
ugonjwa huu kwa kasi.
Programu za utoaji chanjo zimeendeshwa kwa ushirikiano wa
mashirika ya kimataifa na serikali za kitaifa, na juhudi hizi zimefanya ugonjwa
wa polio kuwa nadra sana katika sehemu nyingi za dunia ikiwemo Tanzania. Kwa
kuchanjwa watoto wote, tunaweza kufikia lengo la kutokomeza kabisa ugonjwa wa
polio. Mwaka huu Serikali kushirikiana na wadau wa maendeleo kama