Na, John Kabambala:
Yespa Manispaa ya Morogoro hapa ndipo
historia ya binti Marrystella Kagambi inapo anzia, yupo binti mmoja aitwae Marrystella
Kagambi, usistajaabu kulitaja jina lake hii ni kwa sababu yeye ameniruhusu
kutumia jina lake halisi, akiwa na maana ya kuisaidia jamii maana yeye kwa sasa
nimuelimishaji jamii kuhusu kujilinda na kuwalinda wengine dhidi ya vvu. Marrystella
Kagambi alipata maambukizi ya virusi vya UKIMWI miaka 30 iliyopita wakati
alipokuwa mdogo. Wakati huo, elimu kuhusu virusi hivyo ilikuwa ndogo, na watu
wengi walikuwa na hofu na unyanyapaa kuhusu UKIMWI.
Marrystella Kagambi alikua katika familia yenye upendo na
msaada, binti huyu yeye alizaliwa akiwa na maambukizi kutoka kwa mama yake. Baada
ya kuzaliwa Mama yake hakuishi muda mrefu hatimae alifariki na kumuacha Marrystella
Kagambi angali bado mtoto na akalelewa na nduguzake, walijitahidi kumpa elimu
juu ya jinsi ya kudhibiti virusi vya UKIMWI na kudumisha afya yake. Walimwambia
kuwa UKIMWI haukumaanishi mwisho wa maisha, na alikuwa na jukumu la kujitunza
kwa kumeza dawa za ARV kwa wakati na kufuata ushauri wa daktari.
Kutokana na upendo wa familia yake na kujitolea kwa Marrystella Kagambi kwa matibabu yake,
aliweza kujifunza kuishi na virusi vya UKIMWI na kuendeleza maisha yake. Miaka
30 baadaye, Marrystella Kagambi bado alikuwa na afya njema na aliendelea
kutoa mchango mkubwa kwa jamii yake. Alianzisha kikundi cha kuwasaidia watu
wanaoishi na virusi vya UKIMWI katika eneo lake analo ishi, na kusaidia wengi
kupata matibabu na msaada wa kijamii. Amekuwa mfano wa kuigwa kwa jinsi
alivyoweza kudumisha matumaini, nguvu, na upendo licha ya changamoto za maisha
yake.
Suala la maambukizi ya virusi vya HIV vinavyo sababisha ugonjwa
wa Ukimwi bado linawakosesha usingizi wataalamu wa afya ulimwenguni kote, Tangu
ugonjwa wa Ukimwi ulipogunduliwa miaka ya 1980, kumekuwa na fikra mbalimbali
kwa baadhi ya wanajamii kuhusu jinsi virusi vyake vinavyoweza kusambazwa, Je
maisha ya waathiriwa wa ugonjwa huo katika jamii yakoje hadia sasa? Leo
nimepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa waathirika katika Mkoa wa Morogoro.
Hali ilivyo kuwa kwa Marrystella Kagambi:
“Haikuwa halaka na rahisi kwa umri wangu niliokuanao kuelewa umuhimu wa kumeza
dawa kwa wakati na kilasiku ukizingatia sikufahamu kwanini ninameza dawa pasipo
ukomo, nyakati nyingi sikuwa mfuasi mzuri wa dawa ikiwa dada zangu ambao
walikuwa wasimamizi wangu hawakukumbuka kuniambia muda umefika wa kumeza dawa
hata mimi sikujali.”
Ni miaka 30 sasa akiishi na hali ya maambukizi ya vvu, binti huyu anaeishi
Yespa Kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro jina lake Marrystella Kagambi
anasema alizaliwa akiwa na maambukizi ya vvu, amegundua kua yupo katika hali
hiyo alipofika darasa la sita dada yake alipompeleka kituo cha afya kwa ajili
ya kujua hali yake kiafya, akiwa mkubwa mwenye kutambua jambo lolote ndipo
alipojua kwanini alikuwa akisisitizwa kumeza dawa pasipo ukomo.
“Kusema kweli nilipo gundua kwamba nimtu ninaeishi na maambukizi ya vvu nilisikitika
laki haikuniumiza sana kwa sababu niliyapata tangu kuzaliwa kwangu kutoka kwa
mama yangu, tofauti na mtu ambae akipata maambukizi akiwa anajitambua huumiza
sana kwani huanza kujiuliza jamii itamtazamaje juu ya mwenendo wa afya yake”.
Unyanyapaa.
Miongoni kati ya changamoto ambazo amewahi kukutana nazo kuhusu unyanyapaa ni
shuleni kwa baadhi ya walimu wake wa darasa, akiwa bado shule ya msingi alikuwa
na kidonda sikioni chamuda mrefu hakiponi hali ile ilisababisha nzi mranyingi
kwenye sikio lake, mwalimu mmoja wakike sikumoja aliniita pembeni ya darasa
akamwambia kuanzia kesho asiende tena shuleni hadi kidonda hicho kitakapo pona.
“Nilipo fika nyumbani nilimueleza dada yangu alicho niambia mwalimu dada
alichukia sana, kesho yake asubuhi niliambatana nae kwenda shuleni tulipofika
wakakaa kikao na mwalimu mkuu na yule mwalimu aliekuwa ameniambia
nisiendeshuleni hadi kidonda kitakapo pona, kumbe mwalimu yule hakuwai kujua
haliyangu ya maambukizi kiukweli niliruhusiwa nikaendelea na masomo kama kawaida
ila sijawahi kusahahu tukio hilo lililo nifikirisha, nikajiuliza kwani mwenye
maambukizi hapaswi kuchangamana na watu wengine?”
Aidha Marrystella anasema tangu wakati huo akaanza kua mfuasi mzuri wadawa
kipindi cha masomo yake ya shule ya msingi hadi sekondari akamaliza kwa uzuri
japo hakufanikiwa kuendelea na elimu ya juu lakini alipata maarifa yakuendesha
maisha yake, na huduma zinazotolewa kwenye vituo vya afya wanazipata kwa wakati
pasipo shida yeyote kutoka kwa wahudumu na mambo yameboreshwa hakuna tena
unyanyapaa wa aina yeyote.
“Nashukuru MUNGU sasahivi wakati mwingine ninachukuliwa na vituo vya afya na
hosipitali ya Mkoa kwenda kuelimisha vijana wenzangu kuhusu namna ya kujitokeza
kupima afya zao na kuchukua hatua madhubuti kwa wanaogundulika wana maambukizi
na hata wasio na maambukizi, tunawashauri maisha ya kuishi baada ya kujua hali
zao.”
Mahusiano:
Bi,Kagambi anasema, Ukiwa unaishi katika hali ya maambukizi sio sababu ya
kutokuwa na mpenzi..hapana isipokuwa inabidi ufuate ushauri wa wataalamu wa
afya ni nyakati gani zinafaakwako kuwa na mpenzi au kama unataka kubeba
ujauzito kila hatua, mfano mimi nina mpenzi wangu tunaishi nae hadi sasa na
tunatarajia kufunga ndoa nikiwa kwenye hali hii ya maambukizi ya vvu, bahati
nzuri na yeye anafahamu kuwa nipo kwenye hali hiyo na tunaishi kwa ushauri wa
daktari.
Ushauri:
Hata hivyo Marrystella anaishauri jamii. “ushauri wangu hususani kwa vijana
wajitokeze kwenda kujua hali zao za kiafya na wachukue hatua baada ya kupata
majibu, huduma kwenye vituo vya kutolea huduma kwa watu wanaoishi na maambukizi
ya vvu zimeboreshwa mno huwezi kujutia ukifika kwa lengo la kupata ushauri,
kupima hata kuchukua dawa wasiogope milango ipowazi kuwa na vvu sio mwisho wa
maisha.”
Historia hii fupi ya Marrystella Kagambi inatufundisha
kuwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI hayazuii kufikia ndoto zetu au kuendeleza maisha
yetu. Kwa elimu, matibabu, na msaada wa kijamii, watu wanaweza kuishi maisha
yenye afya na furaha licha ya kuwa na virusi vya UKIMWI. Marrystella Kagambi ameonyesha
kuwa na matumaini, nguvu, na upendo, unaweza kuwa chombo cha mabadiliko katika
jamii yako na kuwasaidia wengine.