Na, John Kabambala:
Mwangaza
wa matumaini ulikuwa ukibadilika kuwa giza kwa msichana mmoja mdogo tulie mpa
jina la Leilo. Alikuwa na miaka kumi na tatu tu, lakini ndoto zake zilikuwa
kubwa kama anga la usiku lenye nyota nyingi. Leilo alitamani kuwa daktari,
kutoa matibabu kwa watu wa kijiji chake, na kuifanya dunia kuwa mahali bora.
Kwenye makala hii
utakao wasoma na walio shiriki kuelimisha jamii kupitia visa na ushauri wao ni
pamoja na, Leilo, Bakita Andrea, Maria Mussa
na Kijana wa kiume Kassima.
Lakini, kwenye njia ya Leilo kuelekea ndoto zake, kulikuwa
na kivuli kikubwa kinachoitwa Kassima
hata hilo sio jina halisi. Kassima, kijana mwenye umri wa miaka ishirini na tano,
alijulikan kwa kuwa na tabia mbaya kwenye kijiji hicho. Alijaribu kumvuruga
Leilo, akimtisha na kumfuata kila mahali. Alitumia maneno machafu na vitisho
vya kikatili, akimwonyesha uovu wa ulimwengu.
Leila alijawa na hofu na machungu. Alikuwa amefungwa katika
lindi la aibu na udhaifu. Hakuwa na uhakika wa kufichua mateso yake kwa mtu
yeyote, na alihisi ange mueleza mtu mwingine angeweza kutupwa kando bila kupewa
msaada wowote. Ndoto zake za kuwa daktari zilififia polepole, kama jua
linalofifia magharibi.
Ndugu msomaji wa makala hii, wakati nafanya nae mahojiano kuhusu kisa
hiki, fahamu zangu zilikuwa zinakija na kuondoka mara baada ya kuuvaa uhusika
wa msichan huyu “Leilo”.
Lakini siku moja, Leilo aliamua kusimama kwa ujasiri na
kutoa mapambano. Aliamua kuzungumza na dada yake mkubwa, Amina, kumwelezea kila
kitu. Amina alimsikiliza kwa makini, akimtia moyo kwa upendo na kumweleza kuwa
yuko tayari kusimama naye bega kwa bega.
Kwa pamoja, Leilo
na Amina walifanya uamuzi wa kuwasiliana na wazazi wao na walimu wao kuhusu
mateso ya Kassima. Walitoa sauti yao dhidi ya ukandamizaji huu. Walikuwa sauti
ya haki na usawa, na walitafuta msaada wa jamii yao.
Sauti ya Leilo na
Amina ilisikika kote kijijini.
Kiongozi wa kijiji alisikia kilio chao cha ujasiri na aliamua kuchukua hatua.
Kassima alikamatwa na kushtakiwa kwa ukatili wa kijinsia. Alipelekwa mahakamani
na hatimaye alihukumiwa kutumikia kifungo.
Baada ya tukio hilo, Leilo
alianza kurejesha ndoto zake. Alishiriki masomo yake na kuchukua hatua kuelekea
kuwa daktari mwenye bidii. Kwa mara nyingine, aliona jua la matumaini
likichomoza.
Ikumbukwe kwamba nchini Tanzania umri wa balehe ni kipindi
kinachoambatana na hatari zaidi kwa wasichana, hasa kwa wale waishio katika
mazingira magumu, jambo linaloonyesha umuhimu wa kuongeza na kuendeleza uimarishaji
wa uelimishaji kuhusu usawa wa kijinsia, haki na maendeleo yao ya wasichana.
Ili kuisaidia Serikali katika kuelimisha kundi hili lililopo
kwenye hatari zaidi, vyama vya kiraia, jamii, wazazi, walezi, viongozi wa dini,
viongozi wa kimila, wasichana na wavulana wenyewe wanapaswa kushiriki
kikamilifu kila mmoja kwa sehemu yake, ili kukabiliana na changamoto zinazo
wazunguka wasichana.
Niliwatafuta na kufanya mazungumzo na baadhi ya wasichana
walio katika umri wa rika balehe, kusikia wanafahamu nini kuhusu masuala ya
ukatili wa kijinsia, Bakita Andrea mkazi wa Manispaa ya
Morogoro ni msichana mwenye umri wa miaka kumi natatu (13) mwanafunzi wa
darasa la tano katika shule ya msingi saba saba “A” iliopo Manispaa ya
Morogoro, anaelezea vitendo vya ukatili.
“Ukatili ni unyanyasaji wa kijinsia kwakuwafanyisha kazi
ngumu zisizo endana na umri wao kuwapiga, kuwanyanyasa na kuwatenga, ukatili
huwakuta sana watoto wakike, wengine hufanyiwa ukatili na wazazi wao, ndugu zao
jamaa na marafiki n ahata walimu wao. Nakumbuka juzijuzi shule ya Mazimbu
alijinyonga mwanafunzi wa darasa la tano kwa kufanyiwa ukatili na babayake
aliharibika sehemu zake za siri kwasababu alikuwa akibakwa na babayake”
Amesema.
Aidha Bakita anasema madhara yanayoweza
kujitokeza kwa binti alie fanyiwa ukatili, “Ukatili wa namna hiyo
huleta madhara kwa mtoto wakike kwa kumuharibia sehemu za siri nakumfanya awe
hayupo makini darasani kwa sababu akiwa darasani mudawote nimtu wakuwaza
nikirudi nyumbani usiku kazi kwa baba ataanza kuni fanyia vitendo vya ukatili”.
Bakita akapaza sauti yake kwaniaba ya wasichana
wengine kwa Serikali kuhusu watu wanao fanya vitendo vya ukatili dhidi ya
watoto wakike, “Serikali ikomeshe vitendo vya ukatili na itoe adhabu
kali kwa wale wanao wafanyia watu vitendo vya ukatili”.
Hata hivyo Maria Mussa yeye ni mwanafunzi
wa darasa la saba shule ya msingi Uhuru iliopo katika Manispaa ya Morogoro,
anaeleza anayo yafahamu juu ya ukatili wanao fanyiwa watoto hasa wakike.
“Nakumbuka kulikuwa na watoto watatu waliokuwa wakiishi na
bibi, babu na binamu yao, kumbe binamu yao akawa kila siku anaingia kwenye
chumba cha hao watoto watu nyakati za usiku wakiwa wamelala na kuwa fanyia
ukatili kwa kuwarawiti na kuwambia wakipiga kelele nawaua”.
Maria akatoa ushauri kwa jamii hususani wazazi, “Wazazi
wawe wanawalinda watoto na wawe wanakaa nao watoto karibu wenyewe kwa sababu
watoto wakienda kulelewa na watu wengine ndio wanawafanyia ukatili”
Amesema.
Kassima, kwa upande wake, alipewa fursa ya kubadilisha tabia
yake. Alikuwa na muda wa kujifunza kutoka kwa makosa yake na kuelewa kuwa
upendo wa kweli haujengwi kwa kutumia nguvu na udhalilishaji.
Kisa cha Leilo kinatufundisha
kuwa ukatili wa kijinsia unaweza kushindwa kwa ujasiri na mshikamano. Kinatufundisha
kuwa tunaweza kusimama dhidi ya ukandamizaji na kuibadilisha jamii yetu kuwa mahali
salama kwa kila mtu. Leilo
alionyesha ujasiri wa kutoka kwenye giza na kuongoza njia kuelekea mwangaza wa
matumaini.