By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
Tanzania Kids Time
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Mazingira
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Wasiliana Nasi
Reading: MBINU ZA MALEZI YENYE MWITIKIO KWA WATOTO WACHANGA NA WADOGO
Share
Notification Show More
Latest News
Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
TANZANIA WILL HOST CIGOFA4 TO FIND CONCRETE SOLUTIONS FOR YOUTH LAND QUESTIONS
Editor's Pick
Aa
Aa
Tanzania Kids Time
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi
  • Contact
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Tanzania Kids Time > Blog > Elimu > MBINU ZA MALEZI YENYE MWITIKIO KWA WATOTO WACHANGA NA WADOGO
Elimu

MBINU ZA MALEZI YENYE MWITIKIO KWA WATOTO WACHANGA NA WADOGO

Tanzania Kids Time
Last updated: 2024/01/29 at 2:30 PM
By Tanzania Kids Time 9 Min Read
Share
SHARE

 

Na, John Kabambala:

Malezi yenye
mwitikio (responsive parenting) ni mbinu ya malezi inayolenga kutoa mazingira
mazuri kwa watoto ili kuwasaidia kukua na kuendeleza ustawi wao wa kimwili,
kihisia, kijamii, na kiakili. Nchini Tanzania, kama ilivyo katika maeneo
mengine duniani, malezi yenye mwitikio ni muhimu sana katika kujenga msingi
mzuri wa maisha ya watoto na jamii kwa ujumla.

Malezi yenye
mwitikio yanaangalia mahusiano ya karibu baina ya mzazi/mlezi na mtoto, ikizingatiwa
kuwa ushahidi unaonesha umuhimu wa mwitikio wa mahitaji ya watoto kulingana

na ishara
watakazo onesha katika kuchangia ukuaji wao. Utaratibu wa kujumuisha huduma za
malezi jumuishi kwenye huduma zilizopo kama vile afya na lishe bado ni dhana
mpya, hivyo inasababisha ufikiaji mdogo kwa walengwa.

Mifano
michache ya huduma jumuishi ambazo hutekelezwa na wadau katika maeneo mbali
mbali nchini hujumuisha uchangamshi wa awali na afya, lishe na ulinzi wa mtoto.
Afua zilizopo ni chache na zipo kwenye mfumo wa miradi au utafiti zikitekelezwa
kwa kiwango kidogo na kujumuishwa moja kwa moja

katika
program za Afya na Lishe zinazoendeshwa katika vituo vya Afya na ngazi ya
jamii. Kwa hivyo hakuna takwimu za taifa au afua katika kipengele hiki cha
MMMAM kinacholenga watoto wenye umri wa miaka 0-3.

Malezi kwa Makuzi na Maendeleo ya Awali
ya Mtoto:

Malezi kwa
Makuzi na Maendeleo ya Mtoto (CCD) ni mkoba ulioandaliwa wenye mbinu zilizothibitishwa
na Shirika ya Afya Duniani (WHO) na
Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF)
kwa ajili ya watoa huduma za afya ili kutoa unasihi kwenye michezo na
mawasiliano kwa wazazi/walezi wenye watoto wa wenye umri wa miaka 0-3 wakati wa
utoaji wa huduma za afya.

Serikali kwa
kushirikiana na wadau wa maendeleo kupitia WAMJW kitengo cha Afya ya Mama na
Mtoto imeanza kuwekeza kwenye malezi yenye mwitikio kwa kujumuisha mbinu za malezi
kwa makuzi na maendeleo ya mtoto pamoja na mafunzo ya ufuatiliaji wa ukuaji na
maendeleo ya mtoto. Mpaka sasa rasimu ya Mwongozo wa Malezi kwa Makuzi na
Maendeleo ya Mtoto na mkoba wa Malezi kwa Makuzi na Maendeleo ya Mtoto
vimeandaliwa. Lengo la Mwongozo wa Kitaifa wa Malezi Kwa Makuzi na Maendeleo ya
Mtoto ni kuhakikisha huduma za malezi yenye mwitikio zinafika nchi nzima kupitia
mfumo wa afya. 

Mkoba wa
mafunzo ya Malezi Kwa Makuzi na Maendeleo ya Mtoto kinawajengea uwezo wahudumu
wa afya wa vituoni na wa kwenye jamii kujumuisha jumbe za uchangamshi wa awali
na malezi yenye mwitikio kwenye huduma za afya. Kitengo cha Afya ya Mama na
Mtoto kimeonesha jitihada ya kutanua wigo wa matumizi ya mkoba wa Malezi Kwa
Makuzi na Maendeleo ya Mtoto kwa kufanya majaribio kwa kuunganisha mkoba wa
Malezi Kwa Makuzi na Maendeleo ya Mtoto na Ufuatiliaji wa ukuaji na Maendeleo
ya Mtoto katika mafunzo kazini.

Pia, Mkoba
wa MMMAM unaonekana katika Mwongozo wa Taifa wa huduma kwa watoto wenye umri
chini siku 28 na uanzishaji wa kitengo cha matunzo ya watoto wenye umri wa
chini ya siku 28. Miongozo hii inatambua umuhimu wa mawasiliano na mtoto
kuanzia ujauzito, mtoto mchanga na mtoto mgonjwa. Pia, mwongozo wa huduma kwa
watoto wenye umri chini ya siku 28 unatambua ustawi wa mama kwa mahusiano bora na
mtoto na ukuaji wake41 . 

Ingawa
huduma za malezi yenye mwitikio zinaweza kuonekana kuwa mbinu mpya nchini, ni
muhimu kutambua mila na desturi nzuri zilizopo zikiwemo za malezi ya watoto
ambazo zinaweza zikaendelezwa na kuboreshwa pale inapowezekana. Aidha, wazazi,
walezi na familia washawishiwe kutumia stadi na uwezo wa kutengeneza vifaa vya
michezo vinavyopatikana kwenye jamii kwa kutumia malighafi zenye gharama ya
chini, mfano chupa 41

https://www.medbox.org/document/national-guideline-for-neonatal-care-and-establishment-of-neonatal-care-unit#GO

tupu, nguo,
vifuu na michanga. Kwa kutumia malighafi hizo familia wanaweza kutengeneza, magari,
mwanasesere, chekeche, vitabu na vingenevyo. Huduma za Afya na Lishe zilizopo nchini
zinatoa fursa ya kutoa huduma za malezi jumuishi. Hii inajumuisha uwepo wa mkakati
wa Huduma za Afya kwenye Jamii ili kusaidia Watoa Huduma za Afya Kwenye Jamii
(WAJA) kutembelea kaya na huduma za malezi jumuishi.

Hii inajenga
mazingira ya watoa huduma jumuishi za malezi yenye mwitikio, uchangamshi wa
awali, ulinzi wa mtoto, pamoja na huduma za afya na lishe. Vilevile, kupitia
Mpango Jumuishi wa Taifa wa Lishe, shughuli za malezi, makuzi na maendeleo ya
awali ya mtoto zimejumuishwa pamoja na programu ya
lishe ambapo inajenga nafasi ya kuenea kwa huduma hizi nchini.

Pia, kuna nafasi
ya kuunganisha na kusambaza programu na vifurushi vya mawasiliano vilivyopo ambavyo
vimejumuisha vipengele vya malezi jumuishi kama vile mradi wa malezi ambao unatekelezwa
na Shirika la EGPAF mkoani Tabora; Programu ya kuharakisha kupunguza udumavu
inayotekelezwa kupitia Shirika la Kimataifa la kuhudumia Watoto katika mikoa ya
Iringa, Njombe, Mbeya na Songwe; na utafiti wa afua za kuwahusisha kina baba
katika Huduma bora za Lishe unaofanyika na Shirika la PCI Mkoani wa Mara.

                     

AJENDA YA KITAIFA YA MALEZI

Ajenda ya
Kitaifa kwa Malezi na familia Tanzania (Familia Bora, Taifa Imara) kwa watoto
kuanzia miaka 0-18 ina nguzo za malezi bora (Lea –Linda – Wasiliana) ambazo
zinajitosheleza katika mbinu za malezi yenye mwitikio. Ajenda ya Kitaifa ya
Malezi inatoa nafasi ya kushughulikia taratibu za malezi kwa watoto na
kuzishughulikia katika programu za Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya
Mtoto za kisekta.

https://download.ei-ie.org/Docs/WebDepot/Report%20Tanzania_UB.PDF

FURSA ZA UJIFUNZAJI WA AWALI

Kujifunza
huanza tangu ujauzito na sio shule ya awali, na unaendelea katika maisha yote ya
binadamu, Ujifunzaji wa awali ni uwezo anaojengewa mtoto kupitia mwitikio wa
mlezi ambapo mtoto anapata ujuzi, sifa na uwezo kupitia vitendo rahisi mfano
kutabasamu, kutazama machoni, kuzungumza, kuimba, kutoa mifano kwa vitendo,
kuigiza, na michezo rahisi ili kuhakikisha mafanikio ya kuzoea mabadiliko kwa
haraka yakiwemo ya kujenga mahusiano na watu wengine. Hivyo, ujifunzaji sahihi
wa awali ni muhimu kwa makuzi ya mtoto kiakili, kijamii, kijinsia, kimwili na
katika maandalizi na utayari wa elimu ya baadae.

Elimu katika vituo vya kulelea watoto
wadogo Mchana

Nchini
Tanzania watoto wenye umri wa miaka 3-4 hawafikiwi na programu za malezi na
makuzi ya mtoto. Mkanganyiko katika sera na Sheria za elimu ya awali
unachanganya watekelezaji na wadhibiti katika utoaji wa huduma katika kundi
hili. Wakati Sera ya Elimu inasema watoto hawa wanaweza kupata elimu ya awali,
Sheria ya Mtoto inatoa mamlaka kwa Kamishina wa Ustawi wa Jamii kusimamia
huduma jumuishi za malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto chini ya miaka 5.

https://www.google.com/search?q=43+Ministry+of+Education+Science+and+Technology+(MoEST)+Education+and+Training+Policy+2014.&oq=43+Ministry+of+Education+Science+and+Technology+(MoEST)+Education+and+Training+Policy+2014.&aqs=chrome..69i57.1169j0j7&sourceid=chrome&ie=UTF-8

Hata hivyo
mtaala na upimaji wa maendeleo kwa elimu ya awali unalenga watoto wa miaka 5.
Aidha, kuwepo kwa changamoto ya mlundikano na mchanganyiko wa umri katika
mikondo ya elimu ya awali imepelekea kupunguza uandikishaji wa watoto wa miaka
3-4. Vilevile kama hakuna programu za kitaifa zinazolenga watoto wa umri wa
miaka 3-4, wengi wa watoto hawa wanakosa fursa za elimu ya awali. Hii pia ina
maana kuwa hakuna programu rasmi ya kitaifa inayoendana na maendeleo ya kundi
hili, hivyo kupelekea watoto hawa wanapojiunga na vituo vya kulelea watoto
wadogo mchana huishia katika mfumo wa kufundishwa badala ya kujifunza kupitia
michezo na kutumia zana kulingana na mazingira yao.

https://download.ei-ie.org/Docs/WebDepot/BEST2016FINAL2SEPT2016-FINALPRINTING-2.pdf

Wakati shule
binafsi na shule za madhehebu ya dini zikiongeza kutoa elimu ya malezi na elimu
ya awali hata hivyo huduma hizi hufikia asilimia 5 tu ya watoto wote wenye umri
huo, mathalani wengi wao wakiwa maeneo ya mijini42. Serikali kwa kushirikiana
na wadau wa maendeleo imewekeza katika mipango mbalimbali ya kutatua changamoto
hii ikiwa ni pamoja na kuandaa kiongozi cha mlezi cha kuwezeshea watoto chini
ya umri wa miaka mitano kujifunza kwa njia ya michezo.

 

You Might Also Like

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi

Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili

Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania

KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.

UWEZO TANZANIA YARATIBU KIKAO CHA MIKAKATI YA KUWASHIRIKISHA WAZAZI UELIMISHAJI VIJANA STADI ZA MAISHA.

Tanzania Kids Time October 6, 2023
Share this Article
Facebook Twitter Email Print
Previous Article SABABU ZA KUWEKEZA KATIKA MALEZI, MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO
Next Article LEILO: MWALIMU WA UJASIRI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA
Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

Facebook Like
Twitter Follow
Youtube Subscribe
Telegram Follow
- Advertisement -
Ad image

Latest News

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
//

Tanzania Kids Time: A platform spotlighting children’s and women’s issues in Tanzania, focusing on education, health, and environmental conservation.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

© 2023 Tanzania Kids Time. Powered by Digital Media Innovation Program. All Rights Reserved.

Join Us!

Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..

Zero spam, Unsubscribe at any time.

Removed from reading list

Undo
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?