Na, John Kabambala:
Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) bado ni changamoto
kubwa nchini Tanzania, na vijana wenye umri wa rika balehe hasa wasichana
wanakabiliwa na hatari kubwa ya kuambukizwa VVU. Elimu ya afya ya uzazi ni
muhimu sana katika kuzuia maambukizi ya VVU kwa vijana, kwani inawawezesha
kujifunza na kuelewa njia za kujikinga, kujenga uhusiano wenye afya, na kufanya
maamuzi sahihi kuhusu afya yao ya uzazi. Makala hii inalenga kuchambua umuhimu
wa elimu ya afya ya uzazi katika kuzuia ongezeko la maambukizi ya VVU kwa
vijana wa rika la vijana balehe nchini Tanzania.
Tuanzie Mkoani Mbeya, ambako Shirika sililo la kiserikali, Tumaini
Community Services linatekeleza mradi wa ‘Dreams’
yaani ‘Ndoto’ katika Halmashauri ya Mbeya
mjini, Kyela na Mbarali mkoani Mbeya kwa ufadhili wa
mfuko wa rais wa Marekani wa harakati za kupambamba na UKIMWI, PEPFAR kanda ya Tanzania, lengo likiwa kuwawezesha vijana
balehe elimu ya afya ya uzazi, elimu ya kujitambua na elimu ya kiuchumi ili
kupunguza maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI, ambapo mpaka sasa zaidi
ya vijana elfu 30 wamefikiwa na mradi huo kwa Wilaya hizo
tatu.
Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) bado ni changamoto
kubwa nchini Tanzania, na vijana wenye umri wa balehe wanakabiliwa na hatari
kubwa ya kuambukizwa VVU. Elimu ya afya ya uzazi ni muhimu sana katika kuzuia
maambukizi ya VVU kwa vijana, kwani inawawezesha kujifunza na kuelewa njia za
kujikinga, kujenga uhusiano wenye afya, na kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya
yao ya uzazi. Makala hii inalenga kuchambua umuhimu wa elimu ya afya ya uzazi
katika kuzuia ongezeko la maambukizi ya VVU kwa vijana wa rika la balehe nchini
Tanzania.
Sababu zinazo weza kusababisha vijana hawa kupata maambukizi
ya virusi vya UKIMWI miongoni mwazo ni Ukatili
wa Kijinsia, Vijana wa rika la balehe wanaweza kuwa katika hatari zaidi
ya kubakwa au kulazimishwa kufanya ngono bila kinga, ambayo inaweza kusababisha
maambukizi ya VVU.
Ujinga na Kutojua,
Vijana wengi hawana ufahamu wa kutosha kuhusu VVU na njia za kujikinga, na
hivyo wanaweza kuchukua hatari bila kujua, Ubaguzi na Unyanyapaa, Ubaguzi na unyanyapaa kuhusu VVU vinaweza
kufanya vijana waogope kupima na kutafuta huduma za afya.
Tatu Mwambungu kutoka
Wilayani Kyela ni mnufaika wa mradi wa Dreams unaotekelezwa mkoani Mbeya na
shirika la Tumaini Community Services anaeleza sababu anazofikiri kuwa ni visababishi
vinavyowaweka matatizoni vijana balehe hasa wa kike, anasema ni kutokana na kukosa
elimu sahihi ya afya ya uzazi akisema kwamba wanafika umri wa kubalehe lakini
hawana elimu hiyo, “tunakuwa hatujui
kutokana na jamii yetu wanaficha au wzazi wanaficha vile vitu ambavyo binti
anatakiwa kuvijua akishakua amebalehe”.
Je, Kuna umuhimu na ulazima kiasi gani vijana kufundishwa elimu ya Afya
ya uzazi?
“Elimu ya afya ya uzazi inaweza kutoa vijana maarifa na
ufahamu kuhusu VVU, njia za maambukizi, na jinsi ya kujikinga. Vijana
wanapoelewa hatari, wanakuwa na msukumo wa kuchukua hatua za kuzuia. Kujifunza Njia za Kujikinga, Elimu
hutoa taarifa za kina kuhusu njia za kujikinga na VVU, kama vile matumizi ya
kondomu na kupima VVU mara kwa mara.
Kukuza Uhusiano wa
Afya,Vijana wanaweza kujifunza jinsi ya kujenga uhusiano wa afya na
kuzungumza na wenza wao kuhusu masuala ya ngono na afya ya uzazi. Hii inaweza
kusaidia katika kuzuia maambukizi ya VVU. Kutoa Elimu ya Kupima VVU, Elimu ya afya ya uzazi inaweza kutoa
mwongozo kwa vijana kuhusu umuhimu wa kupima VVU na kutafuta matibabu mapema,
na pia kuhusu upatikanaji wa vituo vya kupima VVU” Tatu Alisema.
Dkt. Steward Kilumile
ni Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Miyombweni kilichopo Wilaya ya Mbarari
anasema elimu kuhusu afya ya uzazi inayotolewa kwa vijana anaona inaleta
mabadiliko. Akisema, “kupitia mradi kama huu wa dreams kwa kuwa wanapata
elimu kwenye vikundi inazidi kuwapa vijana upeo dhidi ya mazingirea
hatarishi.”
Aidha Dkt. Steward
Kilumile Serikali iongeze msisitizo
ufikishwaji wa elimu hii kwa Vijana, na vijana wengi wa Tanzania
wanaishi vijijini, na hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa elimu ya afya ya uzazi
inawafikia pia katika maeneo haya. Hii inaweza kufanyika kwa kutoa semina na
mikutano katika vijiji, na hata kuongeza vitengo maalumu kwa vijana kwenye
vituo vya afya katika maeneo ya mbali.
Kujumuisha Wazazi na Walezi: Wazazi na walezi
wanaweza kuwa sehemu muhimu ya mchakato wa kutoa elimu ya afya ya uzazi.
Kuwajumuisha katika mafunzo na kampeni kunaweza kusaidia kuunda mazingira bora
ya kujadili masuala ya afya ya uzazi nyumbani. Kutoa Elimu Kwa Kuzingatia
Utamaduni: Elimu inapaswa kuendana na utamaduni na mila za eneo husika. Hii
itawezesha kukubalika kwa elimu hiyo kwa jamii na kupunguza unyanyapaa.
Jonathan Mwashilindi
ni Mkurungezi wa shirika hilo la Tumaini anasema wasichana wenye umri mdogo
kutokana na kukosa muongozo mzuri ndipo wanajikuta wanapata ujauzito wakiwa
bado watoto wadogo na hawajui hao watoto watakaozaliwa watawatunza kwa namna
gani. Kwa msingi huo anatoa wito kwa kila mtu katika jamii kushiriki katika
kusaidia “ili hawa mabinti ndoto zao waweze kziishi baadaye.”
Mfuko wa rais wa Marekani wa harakati za kupambamba na UKIMWI, PEPFAR kanda ya Tanzania
umekuwa ukisaidia serikali ya Tanzania kuboresha sekta ya afya kwa ujumla wake
hasa katika kupambambana katika kupunguza maambukizi ya vvu nautoaji wa elimu
ya afya ya uzazi kwa vijana balehe, jitihada hizo zimeendelea kujidhihilisha
kupitia miradi mbalimbali inayo husu afya.
Njia za Kutoa Elimu ya Afya ya Uzazi
Ndg. Jonathan Mwashilindi Anapendekeza hatua zifuatazo zikifanyika kwa uhakika na kwa ushirikiano wa kila sekta
zinaweza kutoa matokeo mazuri. Shule, Elimu ya afya ya uzazi inaweza
kuingizwa kwenye mtaala wa shule ili kufikia vijana wa shule kwa ufanisi.
Makongamano na
Semina,Kuandaa makongamano na semina kwa vijana wa balehe inaweza kuwa
njia nzuri ya kutoa elimu ya afya ya uzazi, Vyombo vya Habari, Matangazo kwenye redio, televisheni, na
mitandao ya kijamii yanaweza kutumiwa kutoa taarifa kwa vijana, Vituo vya Afya, Vituo vya afya
vinaweza kuwa vituo vya kutoa elimu ya afya ya uzazi na kupima VVU.
Katika ulimwengu wa sasa, teknolojia inaweza kutumika kutoa
elimu ya afya ya uzazi kwa njia ya programu za simu na tovuti. Hii inaweza
kufanya elimu kuwa inapatikana kwa vijana kwa urahisi na kwa njia inayowafikia.
Elimu ya afya ya uzazi ina jukumu kubwa katika kuzuia
maambukizi ya VVU miongoni mwa vijana wa rika la balehe nchini Tanzania. Kwa
kutoa elimu hii kwa njia inayofaa na kuongeza ufikiaji wake, inaweza kusaidia
kubadilisha tabia za vijana, kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya yao
ya uzazi, na hatimaye kupunguza maambukizi ya VVU. Ni jukumu la pamoja kwa
serikali, mashirika ya kijamii, wazazi, na jamii kwa ujumla kufanya kazi kwa
pamoja ili kuhakikisha kuwa vijana wanapata elimu hii muhimu na wanaweza kuwa na
maisha yenye afya na mafanikio.