Na, John Kabambala:
Historia ya msichana huyu ilianza kuchanua tangu mwaka 2011, Nimiongoni kati ya vijana wadogo
walio tunukiwa uongozi nyakati za umri wao mdogo kuawahi kutokea kwenye jamii hiyo, kijana ambae anaaminiwa
kwenye vikao mbalimbali katika kuleta suluhisho na utulivu wa myoyo ya wana
nchi. Yawezekana umewahi kulisikia au hujawahi kabisa, ndoto zake nikuwa
kiongozi mwenye fikra tunduizi, je
ni nani huyu?
Vuta pumzi ufuatane name katika
Makala hii itakayo kusogeza karibu kumfahamu msichana huyu ambae ameendelea
kuwa mfano kwa wasichana wenzake, kupitia siku hii muhimu ya watoto wa kike duniani ambayo huazimishwa kila tarehe 11,Oct ya kila mwaka.
Tuanzie hapa, msichana mmoja jasiri na mwenye juhudi anayeitwa Nuru
Madagi, msichana huyu ni mkaazi wa Kata ya Mkambarani katika Wilaya ya
Morogoro Vijijini. Alikuwa na ndoto
kubwa ya kupata elimu ili aweze kujenga mustakabali bora kwa familia yake na
kijiji chake. Hata hivyo, maisha yalikuwa na changamoto nyingi kwake. Baba
yake, ambaye alikuwa mwanakijiji wa kawaida, alipata ugonjwa mbaya
uliosababisha kushindwa kwake kufanya kazi, na hivyo familia ilikumbwa na
umaskini mkubwa.
Nuru
alilazimika kusitisha masomo yake ili aweze kusaidia familia yake. Alikuwa na
ndugu wadogo yaani (wadogo zake)
ambao pia walihitaji huduma na malezi. Alikuwa na umri mdogo, lakini hakuwa na
chaguo jingine ila kuanza kutafuta kazi ndogo ndogo za kuweza kusaidia familia
yake. Alikuwa na moyo wa chuma na hakukata tamaa, huku akitumaini kwamba siku
moja angepata nafasi ya kuendelea na masomo yake, ili azitimize ndoto zake
zilizo kuwa zimeanza kufifishwa umasiki wa familia.
ELIMU NA UFADHILI:
Bahati nzuri, shirika la Camfed Tanzania lilisikia kuhusu kisa
chake cha kuacha shule na wakati alikuwa na uwezo mzuri kwenye masomo na juhudi zake za kutaka kusoma. Camfed
ilimuwezesha Nuru kurejea shuleni na
kutoa msaada wa kifedha na vifaa vya shule. Alikuwa na hamasa kubwa na bidii ya
kusoma na kwa msaada wa Camfed, Nuru alifanikiwa kuhitimu elimu ya
msingi na baadaye elimu ya sekondari.
Akiwa na elimu yake hiyo, alianza kujitolea kwa kijiji chake na
kuwa mfano kwa wengine. Alitambua umuhimu wa elimu na stadi za maisha, na
akaamua kujitolea kufundisha vijana wenzake stadi za maisha. Alijifunza jinsi
ya kuwasaidia vijana kujenga ndoto zao na kufikia malengo yao, kama
alivyofanikiwa yeye mwenyewe.
Programu hii ya Stadi za Maisha imelenga sehemu kuu 3. 1. Kupunguza utoro kwa kufuatilia
mahudhurio ya wanafunzi, 2.kupunguza
mimba za utototoni kwa kuwafundisha wanafunzi kujitambua na 3. Na kuongeza ufaulu kwa kuwahimiza
watoto waweze kujisomea.
Mimi Kama mwezeshaji nimekuwa nikifanya kazi mbali mbalikama
vile: 1.kuwezesha elimu hii ya stadi
za Maisha kwa wanafunzi Mara moja kwa wiki, 2. Kuwasaidia wanafunzi wenye huitaji wa Masada wa kiuchumi na
kijamii akiwa shuleni na nje ya shule, kwa kuwaongoza kwenye ngazi za serikali,
za Kijiji kata na hata madawati ya misaada ya kisheria, 3. Kuunda makundi ya kujifunza wanafunzi amabyo wanayatumia shuleni
na nje ya shule, 4.kufanya
ufuatiliaji wa wanafunzi majumbani na 5.
Kuwahamasisha wanafunzi kuhudhuria shuleni.
KUHUSU UONGOZI:
Nia ya Nuru ya kuwa kiongozi katika jamii
ilisukumwa na uzoefu wake wa kupitia changamoto na matatizo katika maisha yake
ya awali. Alikuwa shuhuda wa jinsi umaskini na ukosefu wa elimu vinavyoweza
kuathiri watu na jamii nzima. Hii ilimfanya kuona umuhimu wa kuchukua hatua na
kusaidia kubadilisha hali ya mambo katika jamii yake.
Nuru alipata fursa ya kujifunza na kukua kupitia msaada wa
Camfed na elimu yake. Akiwa na elimu, alitambua kwamba alikuwa na uwezo wa
kufanya tofauti katika maisha ya watu katika kijiji chake. Nia yake ya kuwa
kiongozi ilijengwa juu ya malengo yake ya kusaidia watu wengine kujikwamua na changamoto
zilizokuwa zikiwakabili.
Kwa kuwa alipitia wakati mgumu katika maisha yake na alipata
msaada kutoka kwa shirika la Camfed, alihisi wajibu wa kurudisha fadhila kwa
jamii yake. Alitaka kuwa mfano kwa vijana wenzake na kuwaonyesha kwamba
wanaweza kufikia malengo yao licha ya changamoto za maisha. Alitambua kuwa kwa
kuwa kiongozi katika jamii, angeweza kuongoza kampeni za kuelimisha watu kuhusu
umuhimu wa elimu, ustawi wa jamii, na stadi za maisha.
Nia yake ya kuwa kiongozi ilikuwa inaongozwa na dhamira ya
kuleta mabadiliko chanya katika jamii yake na kuwasaidia wengine kufanikiwa.
Alijua kwamba kama kiongozi, angekuwa na jukumu la kuhamasisha, kuongoza, na
kuelimisha wenzake kuhusu njia za kuboresha maisha yao. Kwa njia hii, Nuru
alitaka kuhakikisha kwamba watu katika jamii yake wanapata nafasi ya kujenga
mustakabali bora kama alivyofanya yeye mwenyewe.
MAFANIKIO:
“Kupitia program hii imenisaidia Mimi binafsi kujiamnini,
kutambua haki zangu Kama msichana na kujiwekea malengo. MOja kati ya nafasi
ninazo hudumu kwazo tangu mwaka 2021 – 2023, Nimekuwa katibu msaidizi, wa
wanafunzi wafadhiliwa wa Camfed,(CAMA)Ngazi ya wilaya ya morogoro na katibu
ngazi ya Taifa. Nimekuwa Chachu ya uchangiaji wa elimu kwa watoto hasa wa
kike, mfano kwa sasa nimeanzisha Kampeni ya uchangiaji wa taulo za kike kwa
wanafunzi kwa kushikikiana na wadau mbalimbali kwenye ngazi za serikali, mfano
Kijiji na kata ninayoishi”.
Nuru sasa ni mfano wa mafanikio kwa
familia na kijiji chake na ni mkufunzi wa vijana mwenye uzoefu mkubwa
kushughulikia masuala na changamoto za vijana. Amegusa maisha ya watu wengi kwa
kuwahamasisha kufuata ndoto zao na kutoa mchango chanya kwa jamii.
Kupitia maadhimisho ya Siku ya
Watoto wa Kike Duniani ni fursa nzuri ya kuwapa wasichana ujumbe wa kuhamasisha
na kuwapa mwongozo wa jinsi wanavyoweza kufikia malengo yao na kujenga
mustakabali bora. Kuwezesha Elimu:
Wasichana wanapaswa kuelimishwa juu ya umuhimu wa elimu na jinsi inavyoweza
kubadilisha maisha yao. Wazazi, walimu, na jamii wanaweza kuwahimiza wasichana
kusoma na kujifunza kwa bidii.
Kupinga
Mimba za Utotoni: Siku ya Watoto wa Kike iwe
kumbukizi na itumike kutoa elimu juu ya athari za mimba za utotoni na umuhimu
wa kulinda haki za wasichana. Jamii inaweza kufanya kazi pamoja kuzuia mimba za
utotoni na kuhakikisha wasichana wanapata nafasi ya kumaliza elimu yao. Wasichana
wanaweza kuelimishwa juu ya stadi za ujasiriamali na jinsi wanavyoweza kujenga
kazi zao wenyewe. Hii inaweza kuwasaidia kuwa wajasiriamali na kujitegemea
kiuchumi.
Kuhamasisha
Kujiamini: Kujiamini ni muhimu kwa maendeleo ya wasichana. Wanapaswa
kujifunza kujiamini katika uwezo wao na kutambua kwamba wanaweza kufanikiwa
katika kila eneo la maisha yao. Wasichana wanapaswa kujua haki zao za msingi na
kuwa na ufahamu wa jinsi ya kuzitetea. Hii ni pamoja na haki ya elimu, haki ya
afya, na haki ya kushiriki katika maamuzi yanayowahusu.
Siku hii ya Watoto wa Kike itumike kuhamasisha kupinga ubaguzi
wa kijinsia na unyanyasaji. Wanapaswa kujua kwamba hawapaswi kuvumilia
unyanyasaji wa aina yoyote na wanapaswa kutafuta msaada wanapopatwa na hilo.
Pia wasichana wanapaswa kuhimizwa kushiriki katika masuala ya kijamii na
kisiasa. Wanaweza kuelimishwa kuhusu jinsi ya kuwa sehemu ya michakato ya
kuleta mabadiliko katika jamii yao.
Kuelimisha
Juu ya Afya ya Uzazi: Elimu juu ya afya ya uzazi ni
muhimu kwa wasichana. Wanapaswa kujua jinsi ya kujilinda na kupata elimu juu ya
uzazi wa mpango. Kuonyesha Mifano Mzuri: Wasichana wanahitaji kuwa na mifano
mizuri katika jamii yao. Wanaweza kuhamasishwa kuchunguza mifano wa wanawake
waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali na kuwaiga.