Wanawake wajawazito, watoto wachanga na wadogo wanakabiliwa
na hatari kubwa kutokana na athari za kiafya zinazohusiana na mabadiliko ya
hali ya hewa, kutokana na idadi kubwa ya mambo ya kisaikolojia, kiafya, kijamii na kitabia.
Kadiri athari mbaya zitokanazo na hali ya hewa zinavyozidi kuongezeka, ndivyo dunia inavyozidi kuingia kwenye matatizo Zaidi ya kibinadamu
hasa afya kwa wanadamu, Ripoti ya Pengo laUzalishaji wa Gesi Chafu Mwaka wa 2023 imesema: Ripoti hiyo inaonyesha kuwa ulimwengu unaelekea kushuhudia ongezeko la joto la nyuzijoto kati 2.5 na 2.9 kuliko viwango vya kabla ya viwanda iwapo nchi hazitaimarisha juhudi kufanya zaidi kuliko zilivyoahidi chini ya Mkataba wa Paris. Makadirio ya uzalishaji wa hewa chafu kufikia mwaka wa 2030 ni sharti upunguzwe na angalau
asilimia kati 28 na 4 ikilinganishwa na sera zilizopo ili kuweza kufikia
malengo ya Mkataba wa Paris ya nyuzijoto 2 na 1.5.
Ulimwengu unaendelea kuweka rekodi za joto la juu zaidi, ambazo zinazidisha matukio mabaya ya hali ya hewa na athari zingine kwa mazingira kote ulimwenguni. • Mwaka huu, hadi mwanzoni mwa Oktoba, siku 86
zilishuhudia joto la zaidi ya nyuzijoto 1.5 kuliko viwango vya kabla ya
viwanda.
Septemba ndio mwezi ulioshuhudia kiwango cha juu zaidi cha joto kuwahi kurekodiwa, huku wastani ya joto duniani ikiwa nyuzijoto 1.8 kuliko viwango vya kabla ya viwanda. • Uzalishaji wa gesi ya ukaa (GHG) uliongezeka kwa asilimia 1.2 kutoka mwaka wa 2021 hadi mwaka wa 2022 na kufikia viwango vipya sawa na Gigatani 57.4 za Kaboni Dioksidi (GtCO2e). • Vivyo hivyo, Uzalishaji wa GHG katika nchi zote za G20 uliongezeka kwa asilimia 1.2 katika mwaka wa 2022. •
Uzalishaji wa hewa chafu unasalia kusambaa kwa njia isiyo na usawa ndani na kati ya nchi, na kuashiria ruwaza ya kimataifa ya ukosefu wa usawa.
Mabadiliko ya hali ya hewa siku hadi siku yanakuwa tishio linaloongezeka, jambo hili linadhihilisha kabisa hatua za haraka zinahitajika kuchukuliwa
ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, kwa kuzingatia wanawake, watoto wachanga na watoto na wadogo. Bila hatua stahiki za haraka kuchukuliwa haki ya afya kwa wote itakuwa ni ndoto kuifikia ifikapo mwaka 2030.
Kwa kuongezeka kwa joto, jiografia na kiwango cha magonjwa
yanayoenezwa na vekta yanabadilika na kuongezeka. Upatikanaji wa maji umekuwa kidogo sana maeneo mbali mbali nchini na duniani kote, (kutokana na ukame) na maji mengi (kutokana na mafuriko) huathiri kilimo, usalama wa chakula, nyumba na miundombinu, pamoja na upatikanaji wa usalama wa maji safi na usafi wa mazingira, na upatikanaji wa huduma za afya na taarifa muhimu kwa jamii.
Hali hii inaweza kudhihirika kama migogoro ya kibinadamu, inayochangia ongezeko la kasi ya watu kuhama maeneo yao ya asili na kutafuta maeneo ya upatikanaji wa maji safi na salama. Lkini pia hali hii inazidi kuzisukuma familia zenye uwezo na kipato cha chini kua masikini Zaidi kuliko kawaida.
Hatari za hali ya hewa kiafya kwa
mama wajawazito na Watoto Wachanga.
Uzazi: Hatari za hali ya hewa, ikiwa ni pamoja na joto kali, huusishwa na hatari za kuongezeka kwa matatizo ambayo husababisha matokeo mabaya ya uzazi.
Hizi zinaweza kujumuisha sababu nyingi za magonjwa ya uzazi na watoto wachanga na vifo vitokanavyo na magonjwa kama vile kisukari cha ujauzito, matatizo ya shinikizo la damu wakati wa ujauzito, kuzaliwakabla ya wakati, kuzaliwa kwa uzito mdogo na kuzaa mtoto aliyekufa.
Mbali na hatari za kiafya zinazohusiana na lishe duni, maji, usafi na usafi wa mazingira, athari zinazo changiwa na hatari za hali ya hewa na athari zake wakati na baada ya ujauzito inaweza kuathiri afya ya akili na kuchangia wasisi wasi kubwa wanawake wenye ujauzito.
Wanawake na wasichana hubeba mzigo usio na uwiano wa athari za mabadiliko ya hali ya hewa, kwa kuwa inachangia mwingiliano changamano wa majukumu ya kijinsia na kijamii ndani ya nyumba na jumuiya zao. Athari zinazosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, pamoja na ukosefu wa kifedha na uchumi duni, msongo wa mawazo, pia huwaweka wanawake na watoto katika hatari kubwa ya kufanyiwa ukatili.
Watoto
Matukio ya hali ya hewa mbaya, kama vile mafuriko na dhoruba
kali za kitropiki, yanaweza kuongeza viwango vya unyogovuna shida kwa watoto, na athari zinazoweza kudumu za afya ya akili hadi utu uzima uliokithiri matukio ya hali ya hewa yanaweza pia kuathiri vibaya akili ya wazazi na walezi kiafya kutokana na hofu, matatizo ya kifedha na upotevu wa nyumba na rasilimali zingine, kwa mfano. Dhiki ya baada ya maafa kwa
wazazi, inaweza kuathiri juu ya utendaji na usimamizi wa familia na kuongeza
hatari ya malezi duni. Ongezeko la joto kupita kiasi, mvua na baridi kali,
huathiri moja kwa moja afya za watoto.
SULUHISHO:
Afya ya wanawake wajawazito, watoto wachanga na watoto wadogo
huonyesha uthabiti wa kushindwa kwa ustahimilivu wa jamii kiafya. Ushahidi
unaohusisha ongezeko la joto duniani na matokeo mabaya ni ambayo yanahitaji kuchukua hatua. Ingawa mabadiliko ya hali ya hewa yataathiri watu wote, ni muhimu kukumbuka kuwa wanawake, watoto wachanga na watoto wadogo wanaathiriwa kwa kiasi kikubwa kuliko kundi linguine zaidi.
Shirika la Afya Duniani (WHO),
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Watoto (UNICEF),
na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu kwa pamoja (UNFPA) yanatoa wito kwa Nchi Wanachama, washirika
na wadau kulinda afya za wanawake wajawazito, watoto wachanga na watoto wadogo dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi. Ili kufikia afya njema na mustakabali endelevu na wenye usawa kwa wote.
Kuimarisha mifumo ya afya thabiti
kwa uendelevu.
Hatua zinahitajika ili kupunguza utoaji wa kaboni katika
sekta ya afya ili kuboresha afya. Sekta ya afya inawajibika kwa hadi 4.4% ya gesi zote chafu
zinazo zalishwa, ingawa uzalishaji huu haujashughulikiwa au kudhibitiwa.
Vituo vya afya kupitia Wizara ya afya nchini vinapaswa kuhakikisha upatikanaji wa ubora wa huduma za afya kwa wanawake na watoto. Ni muhimu kwamba programu za uhamasisahaji kuhusu utunzaji na kulinda mazingira ilikuokoa afya za makundi haya maalumu nivyema zipewe uzito na umuhimu kwa mahitaji ya wanawake, watoto, vijana, jamii na wafanyakazi wa afya ili kuzijumuisha kwenye shughuli zinazoendelea za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.