WATOTO WA KIKE WASHAURIWA WASIFANYE MAPEZNI MPAKA WAKATI WAO WA NDOA UTAKAPOFIKA.

          Deodatus Balile Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF)

Kufuatia waraka wa Serikali ulioelekeza wanafunzi wa kike waliopata ujauzito warejee shule katika mfumo rasmi baada ya kujifungua, wadau wa Elimu nchini wameipongeza Serikali kwa hatua hiyo.

Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania -TEF ambalo limekua likipigania suala hili kwa muda mrefu, ameipongeza Serikali kwa hatua hiyo na kuahidi kuwapambania watoto siku hadi siku kupitia miradi mbalimbali wanayotekeleza kwa ushirikiano na Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

  Katika hatua nyingine amewatahadhalisha wanafunzi wa kike kutojihusisha na ngono hadi wakati wao wa ndoa utakapofika kwa ajili ya manufaa yao na taifa kwa ujumla, Balile ameyasemahayo wakati wa mahojiano maalumu na waandishi wa habari kutoka Tanzania Kids Time(TKT/UN REDIO) mjini Morogoro mwishoni mwa mwezi Novemba.                  Kituo hiki kinapatikana kata ya Kasanga Morogoro Mjini.
Kwa mujibu wa Takwimu za Elimu ripoti ya Best 2020 inaeleza jumla ya idadi ya         wanafunzi wa kike 1,135 sawa na 0.7% walipata ujauzito katika Shule za Msingi, ilhali shule za Sekondari walikua 5,398 sawa 5.5% mwaka 2019.

Na Hamad Rashid

Subscribe to our Newsletter

Get latest updates of our stories, News and other updates from TKT direct to your email.