TAKWIMU: RUZUKU INAYOTOLEWA NA SERIKALI KWENDA SHULE ZA MSINGI HAIKUKIDHI MAHITAJI YA ELIMU YA AWALI

Kutoka katika Ripoti ya utafiti juu ya upataji Elimu ya awali kwa watoto wenye ulemavu Tanzania Bara , iliyozinduliwa sepemba 14, 2021 na Shirika la Haki Elimu Tanzania, imebainisha Utafiti uliotaka kuelewa ufadhili wa watoto wa shule ya awali wenye ulemavu, mahojiano waliyofanyiwa na maofisa wa wizara miongoni mwao kutoka -TAMISEMI wamefichua kuwa hakukuwa na fedha maalum kwa ajili ya shule ya awali kwa watoto wenye ulemavu.

Kwa kuwa elimu ya shule ya awali ni sehemu ya elimu ya msingi, hivyo hufadhiliwa kupitia ruzuku ya mwanafunzi, ambapo TZS 10,000 hutengwa kwa kila mwanafunzi. Kuhusu suala la kiasi kinachotengwa,  60% hutarajiwa kwenda moja kwa moja shuleni na 40% iliyobaki inatumika kwa vitabu vya kiada.

Matokeo kutoka kwa wakuu wa shule, walifichua kuwa ruzuku ya mwanafunzi iliyopokelewa haikukidhi elimu ya awali, Kando na hayo, ruzuku ya mwanafunzi haitegemei usawa, Kwa hivyo hakukuwa na ufadhili maalum kwa shule ya awali wanafunzi wa shule kutoka serikalini.

Wakuu wa shule waliulizwa zaidi kama kulikuwa na ufadhili wa kusaidia wanafunzi wa shule za awali wenye ulemavu katika mazingira ya elimu-jumuishi.

Takriban 72.3%  wakuu wa shule waliohojiwa walikiri kuwa hawakua na fedha za ziada kusaidia wanafunzi wenye ulemavu lakini Kati yao wakuu wachache wa shule walioripotiwa kuwa na ziada ya fedha, vyanzo vya ufadhili vilitokana na michango ya wazazi (30.4%), ufadhili kutoka kwa wafadhili (56.5%), kujitegemea shuleni (39.1%) na vyanzo vingine (34.8%).

 Chanzo:  Haki Elimu

Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: -

John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com 

Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com

Our main partner

Subscribe to our Newsletter

Get latest updates of our stories, News and other updates from TKT direct to your email.