UTAFITI: 72.5% YA SHULE ZIN A VYUMBA VYA MADARASA YA AWALI KWA WATOTO WENYE ULEMAVU

Kwa mujibu wa Ripoti ya utafiti juu ya upataji Elimu ya awali kwa watoto wenye ulemavu Tanzania Bara , iliyozinduliwa sepemba 14, 2021 na Shirika la Haki Elimu Tanzania, imebainisha Utafiti uligundua kuwa 72.5% ya shule zina madarasa yaliyotengwa kwa ajili ya wanafunzi wa Darasa la awali kwa wenye ulemavu.

Hata hivyo, 66% ya madarasa yalipangwa kama madarasa ya shule ya msingi, na 32% ya madarasa katika shule zilizo tembelewa yangeweza kuelezewa kuwa yanafaa, madawati ya ukubwa wa mtoto, kona za kujifunzia na maonyesho ya darasani.

Katika shule nyingine takriban 7.5% watoto wa darasa la awali walikuwa wakipokezana na wanafunzi wa madarasa mengine.

Hata hivyo takriban 3.8% shule zilizofikiwa hawakuwa na Darasa maalum au Darasa la kupokezana badala yake  madarasa yao yalifanyika nje.

Chanzo:  Haki Elimu

Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: -

John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com 

Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com

Our main partner

Subscribe to our Newsletter

Get latest updates of our stories, News and other updates from TKT direct to your email.