UTAFITI: SHULE NYINGI ZA MSINGI HAZINA MAZINGIRA WEZESHI KWA WATOTO WENYE ULEMAVU


Kwa mujibu wa Ripoti ya utafiti juu ya upataji Elimu ya awali kwa watoto wenye ulemavu Tanzania  Bara , iliyozinduliwa sepemba 14, 2021na Shirika la Haki Elimu Tanzania,  inaonesha kuwa Shule za Msingi nyingi zilizotembelewa hazijaandaliwa vyema kusaidia upatikanaji wa usawa na ushiriki wa watoto wenye ulemavu katika elimu ya awali.

Karibu 66% ya shule zilizo tembelewa zina njia zenye kokoto na mawe, utafiti huo uligundua kuwa ni 16% tu ya Shule zilikuwa na njia ambazo zilikuwa katika hali nzuri.

Aidha  35% ya shule hazina Barabara hata kidogo, na maeneo madarasa maalum yaliyotengwa kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, yatakayo wawezesha watoto kufikia kiurahisi.

Chanzo:  Ripoti ya Utafiti juu ya upataji Elimu ya awali kwa watoto wenye ulemavu Tanzania Bara 2021.

Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: -

John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com 

Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com

Subscribe to our Newsletter

Get latest updates of our stories, News and other updates from TKT direct to your email.