HISTORIA YA VAILETH BUKUKU MKAAZI WA MBEYA MJINI.

Hali ya maaambukizi ya virusi vya UKIMWI nchini Tanzania inaonesha watu wanaoishi na VVU hadi kufikia mwezi Disemba mwaka 2020 watu wazima wenye umri wa kuanzia miaka 15 na zazidi ni 1,600,000, Wanawake 1,000,000, Wanaume 600,000 na Watoto chini ya miaka 15 ilikuwa 100,000 Jumla watu wazima na watoto ni 1,700,000. Maambukizi mapya ya VVU kwa kipindi hicho Watu wazima Zaidi ya miaka 15 wailikuwa 58,000 Wanawake 37,000, Wanaume 21,000 na Watoto chini ya miaka 15 walikuwa 10,000 Jumla watu wazima na watoto 68,000.

Vifo vitokanavyo na UKIMWI kwa mwaka 2020 Watu wazima Zaidi ya miaka 15 vilikuwa 24,000 Wanaume 11,000 elfu, wanawake 13,000 elfu na Watoto chini ya miaka 15 ilikuwa elfu 8,000, Jumla ya vifo watu wazima na watoto ilikuwa 32,000 elfu.

Tukiugeukia Mkoa wa Mbeya, Takwimu zinaonesha kwamba Mkoa huo upokwenye nafasi ya tatu kwa ongezeko la maambukizi ya virusi vya UKIMWI hasa kwa vijana walio katika umri wa rika balehe kwa asilimia 9.3%, Mkoa wa Njombe ukiwa nafasi ya kwanza kwa kuwa na maambukizi ya asilimia 11.4% ukifuatiwa na Mkoa wa Iringa kwa kuwa na maambukizi ya asimia 11.3%, Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) mwaka 2020.

Shirika la Tumaini Community Services lenye makao yake makuu Mkoani Mbeya baada ya kuona ongezeko la maambuki ya virusi vya UKIMWI kwa vijana balehe walio kati ya umri wa miaka kumi natano hadi ishirini na nne yanashamiri, walianzisha mradi wakuwawezesha vijana kupata elimu ya afya ya uzazi, elimu ya upimaji wa vvu, elimu ya kujitambua na elimu ya uchumi.

Mradi huo unajulikana kama DREAMS unatekelezwa Mkoani Mbeya kwa Wilaya tatu ambazo ni Mbeya mjini, Kyela na Mbarali kwa ufadhili wa mfuko wa rais wa marekani wa harakati za kupambana na UKIMWI, PEPFAR kanda ya Tanzania, ambao unalenga kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa vijana kwa kuwapatia elimu ya kujikinga na maambukizi ya vvu, elimu ya kujitambua, na elimu ya kiuchumi.

Katika halmashauri ya jiji la Mbeya nimezungumza na kijana mwenye umri wa miaka ishirini na mbili sasa mama wa watoto wawili anaeishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi, kwa ridhaa yake amerusuhu jinalake halisi litumike kwa matumizi ya kuwaelimisha vijana kuhusu hali ya maambukizi ya vvu ambae ni Vaileth Bukuku.

Vaileth Bukuku ni mzaliwa wa Mbeya mjini, akiwa na umri wa miaka nane (8) alipata maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa kufanyiwa ukatili wa kubakwa akiwa nyumbani kwao Mkoani Mbeya, “Nakumbuka ilikuwa sikukuu ya pasaka dada yangu aliniacha nyumbani nikiwa na njaa akaenda kwenye disko maana siku hiyo alikuja kaka mmoja nyumbani ambae alikuwa na mazoea na dada yangu alipofika akaniuliza Vaileth umekula? Nikamwambia hapana sijala akaniambia njoo uchukue pesa ukanunu mchele uje upike, akanipatia shiringi elfu moja nikaenda dukani kununua mchele.

Badae alirudi tena huyo kaka akaniuliza unatamani kunywa soda? Nikamjibu ndio natamani akaniambia twende ukachukue soda, yule kaka hakunipeleka dukani akanipeleka chooni tulipofika chooni alinibaka nikaumia sana yeye akaondoka nikajikokota kutoka chooni nikashindwa hata kuingia ndani, dada alipokuja usiku sana akanikuta mlangoni akanibeba nikamuelezea jinsi ilivyo kuwa akachemsha maji yamoto akanikanda akanipatia na panado akanimbia usimwambie mtu yeyote, Amesema.

Aidha Vaileth alipofikisha miezi mitatu baadae alianza kuumwa mara kwa mara vidonda vikaanza kumtoka akashindwa hata kuudhulia masomo shuleni, Vaileth anasema “siku moja alikuja jirani yetu nyumbani akaniuliza mbona sikuhizi hujikucheza na watoto wenzako nyumbani na sikia hata shuleni huendi unatatizo gani, sikumwambia kesho yake akarudi tena ikabidi nimwambie ukweli kuwa mimi nina umwa akanichukuwa akanipeleka hospitali tulipofika daktari akamwambia yule mama aenda polisi akachukue pf3 maana anaonekena huyu binti kunakitendo alifanyiwa mbali na magonjwa ya zinaa anamaambukizi ya virusi vya ukimwi .

Mwaka 2019 mradi wa Dreams ukamfikia Vaileth Bukuku kwa sababu alikuwa ndani ya vigezo mradi ulikuwa ukivitaka kwa vijana waliokuwa katika mazingira hatarishi ya kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi, na walio wahi kubeba ujauzito wakiwa katika umri mdogo wanaoishi kwenye Wilaya ambazo zimelengwa kutekelezwa mradi, ambapo huduma ya upimaji ili kujua hali zao za maambukizi ya virusi vya Ukimwi ilifanyika kisha kuwa wanufaika wa mradi huo.

Hata hivyo wataalamu kutoka shirika la Tumaini Community Services walimshauri Vaileth kuwa mfusi mzuri wa matumizi ya dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi na kuendelea kujilinda yeye mwenyewe na kuwalinda wengine ilikutoendelea kuchochea maambukizi mapya kwa jamii, hasa kwa vijana balehe.

Anashukuru mradi wa Dreams kupitia shirika la Tumaini Community Services kwa kumpeleka chuo cha ufundi VETA kujifunza ufundi wa kushona na matumizi ya kompyuta ambao baada ya kuhitimu walikabidhiwa vyeleani kila binti mnufaika wa mradi huo alie somea masuala ya ushonaji, na sasa wamejiajili wenyewe kwa kufungua ofisi ya kushona nguo na kujipatia kipato, wakati huo wakiwa niwaelimishaji wa vijana kuhusu kujikinga na maambukizi ya vvu ikiwemo kutumia kondom wakati wa kufanya ngono.

Malengo ya Vaileth yalikuwa kusoma na kuwa muhandisi wa kompyuta, lakini sasa anaona ameshindwa kuyatimiza kwa sababu tiyari ameshapata watoto wawili na yeye ndio mzazi pekee anaewahudumia pasipo kuona usaidizi kutoka kwa wazazi wenzie wa watoto hao, hivyo basi anasema nguvu nyingi amewekeza kwa watoto wake kuwaandalia mazingira mazuri ya kuja kusoma ili baadae watimize ndoto zao.

Ushauri wake kwa vijana ambao tiyari wanaishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi wafuati ushauri wa wataalamu wa afya ikiwemo kuzingatia muda wa matumizi sahihin ya dawa za kufubaza virusi vya ukimwi, wajilinde na wawalinde wengine wasisambaze virusi vya Ukimwi kwa makusudi kwa wale ambao hawajapima kujua hali zao za kiafya wajitokeze wakapime kujua hali zao ilikuishi kwa Amani na furaha, ilikama hawana maambukizi waendelee kuwa waamifu na wale ambao watagundulika kuwa na maambukizi ya vvu waanze kliniki mapema.

Na. John Kabambala.

Subscribe to our Newsletter

Get latest updates of our stories, News and other updates from TKT direct to your email.