MAHAKAMA YAWAFIKIA WANANCHI ZAIDI YA 30,000 KUWAPA ELIMU YA SHERIA NDANI YA SIKU 7, MOROGORO


Mahakama kuu Kanda ya Morogoro imewafikiwa wananchi zaidi ya Elfu Therathini kuwapatia Elimu na ushauri wa kisheria sambamba na kujibu changamoto zao mbalimbali za kisheria ndani ya siku saba za maadhimisho ya wiki ya Sheria.

Mafanikio hayo ya Mahakama yalielezwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Morogoro, Paul Joel Ngwembe Februari 02, 2022, katika maadhimisho ya Siku ya Sheria yaliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha haki jumuishi Kihonda, wakati akieleza kazi zilizofanywa na Mahakama katika kipindi cha Wiki ya Sheria akitaja maeneo waliyofika na kutoa Elimu, na kwamba wananchi watambue juhudi za hizo ni kwa ajili yao, kwasababu katika maisha ya Binadamu Sheria haikwepeki.

Jaji Ngwembe pia alizungumzia maendeleo ya Teknolojia namna ilivyo na kasi, ikileta manufaa makubwa pamoja na athari ikiwemo Ugonjwa wa Uviko 19, akisema kuwa wamejipanga kuipeleka mahakama mtandaoni ili kupunguza baadhi ya changamoto zinzoazoweza kujitokeza ikiwemo Rushwa.

“Mahakama inaamini maisha yote ya Binadamu yanaongozwa na Sheria, hivyo binadamu hawezi kuikwepa Sheria katika maisha yake yote” alisema Jaji Mfawidhi Paul Ngwembe.

 “katika maadhimisho haya Wiki ya Sheria Kituo chetu cha haki jumuishi, tulikua na maeneo tofauti tofauti ya utoaji Elimu, tulikua na Kituo pale viwanja vya Chamwino, pale Kituo cha mabasi Msamvu, Kiwanja cha Ndege pale Fire, Soko kuu la Chief Kingalu, tumetembelea Shule za Msingi Saba, Sekondari Nne, Chuo cha ualimu Kigurunyembe na magereza yote mawili ambapo ni Gereza la Mahabusu na Gereza la mtego wa Simba’’ aliongeza Jaji Ngwembe

Serikali ya Mkoa wa Morogoro ilitoa ahadi ya kuendelea kuwezesha miundombinu ya mawasiliano katika Mkoa wa Morogoro ili kufanikiwa kwa Mahakama ya kidijitali, alitoa ahadi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Morogoro ALBERTH MSANDO aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

“Nichukue fursa hii kuahidi kwamba tutahakikisha tunashirikiana na Mahakama kufikia malengo yake, tunapozungumzia Mahakama ya kidijitali haiwezi kufanikiwa kama hatutaweka Miundombinu ya mawasiliano katika maeneo yote, Serikali imeendelea kuwa na mpango wa kuhakikisha kwamba katika vijiji vyote kunakua na mawasiliano ya Internet (mtandao) kutoka kwenye vyombo vyetu vya mawasiliano” alisema Mkuu wa Wilaya Wakili Msomi, Alberth Msando.

MARIAMU KAPAMA ni Mwenyekiti msaidizi wa Chama cha wanasheria wa kujitegemea TLS Mkoa wa Morogoro, alisoma Hotuba yao ambapo Pamoja na mambo mengine alieleza athari za UVIKO 19 ilivyoathiri utendaji kazi na kuleta madhara kwa baadhi ya wapendwa wao, akiishauri Mahakama kuitumia Teknolojia vema katika kukabiliana na janga hilo.

Hotuba ya Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali, ilisomwa na Wakili Mfawidhi Mkoa wa Morogoro XAVIER NDALAHWA, Akiahidi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itaendelea kuboresha mfumo wa TEHAMA ili kuunga mkono jitihada za Mahakama.

“Niseme tu kwamba, tumeshuhudia matumizi ya Mtandao, kusajili na kusikiliza mashauri yakifanikisha katika utoaji wa Haki hasa katika kipindi cha Uviko 19, ambapo mashauri yalisikilizwa bila msongamano Mahakamani, mfumo wa mahakama umelea faida kubwa ikiwa ni pamoja na kuokoa muda na gharama” alisema Xavier Ndalahwa.

Maudhui mengine na jumbe za Siku ya Sheria nchini yamepambizwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wanamuziki na wanasanaa, CHEDY ELLY SENZIGE ni mtunzi kutoka Morogoro alisoma Shairi maalumu la Siku ya Sheria.

 ‘’zama za mapinduzi ya nne ya viwanda, safari ya maboresho kuelekea mahakama mtandaoni’’ ndio kaulimbiu ya Siku ya Sheria itakayodumu kwa Mwaka wote wa 2022.

Na Hamad Rashid- Morogoro.

Subscribe to our Newsletter

Get latest updates of our stories, News and other updates from TKT direct to your email.