MIMBA ZA UTOTONI ZIMEONGEZEKA MKOA WA MOROGORO KUTOKA 800 HADI ZAIDI YA 1200


   Pichani ni Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro Bi, Jissica Kagunila

Matukio ya Mimba za utotoni yaliyoripotiwa Ofisi ya Afisa ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, yaliongezeka kutoka 800 mwaka 2019/2020 hadi kufikia zaidi ya 1200 Mwaka 2020/2021.

Akithibitisha Takwimu hizo Afisa usatawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro Bi, Jessica Kagunila, alisema sababu ya Mimba za utotoni kuongezeka inachangiwa na Mila na Desturi za Mkoa huo pamoja na malezi yasiyo mazuri ya watoto.

“Tukianza kwa Mwaka 2019/2020 matukio ya mimba za utotoni yaliyoripotiwa ni 800 lakini tukija kwa Mwaka 2020/2021 yameongezeka hadi kufikia zaidi ya 120, hii ni kutokana na Mila na desturi na malezi yasiyo mazuri kwa upande wa walezi na wazazi’’ alisema Jessica Kagunila

Kwa mujibu wa Ofisi ya muendesha Mashtaka Mkoa wa Morogoro DPP, matukio ya mimba za utotoni ambayo kisheria huitwa matukio ya ubakaji yanaongezeka kutokana na watuhumiwa wa makossa hayo kutoa Rushwa kwa waathirika na kesi kukosa ushahidi Mahakamani, alisema kaimu uendesha mashtaka wa Mkoa wa Morogoro Flora Massawe.

“Inatokea mara nyingi mahakamani, mashahidi wengi ambao ni wahanga watoto wanakuja kugeuka yaani ule ushahidi waliotoa Polisi kwamba wamefanyiwa kitendoi cha ubakaji na flani wakifika mahakamani wanakuja kukataa, na hii tumebaini kutokana na wazazi kuridhia kufanya makubaliano na mtuhumiwa kuna kiasi cha Pesa wanalipana, basi huku kesi zinaharibika’’ alisema Flora Massawe

Afisa ustawi wa Mkoa wa Morogoro Bi, Jessica alieleza namna ambavyo watazidi kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha matukio ya Mimba na Ndoa za utotoni yanapungua.

Bi, Jessica alisema “Elimu sio suala la ustawi wa Jamii peke yake, maendeleo ya Jamii na wadau wengine wa Elimu tutaendelea kushirikiana kuzunguka shuleni kutoa elimu na hata kuwafikia wazazi kadri tutakavyoweza pamoja na walimu ambao wanakaa muda mrefu na watoto’’

Katika kumulikia juhudi za Sekta binafsi kushirikiana na Serikali juu ya kutokomeza Mimba za utotoni Mkoa wa Morogoro, Tanzania kids time ilizungumza na Mratibu wa Miradi Evarist Momburi, kutoka Shirika la SAWA WANAWAKE TAZNANIA lililojikita katika kusimamia ulizi wa Mtoto na utoaji Elimu jumuishi kwa Shule za Msingi, ili kusikia maoni yake pamoja na juhudi zao katika hili.

“kama tunataka tupunguze hili tatizo la Mimba za utotoni, dawa yake ni kujenga mabweni na kujenga Shule shikizi ambazo zitasaidia kupunguza ule umbali wa mwanafunzi kutembea kuifata Shule ilipo, na hili tulifanya utafiti tukagundua watoto wengi walikuwa wanakatiza masomo kwa sababu walikua wanapata changamoto ya umbali kuifata Shule ilipo’’

Alisema katika Mkoa wa Morogoro Shirika la, SAWA WANAWAKE TANZANIA tayari limeshaboresha mabweni ya wasichana katika Shule za Sekondari za DOMA na MVOMERO na Mwaka 2022 wamejipanga kuifikia Shule ya Sekondari WAMI DAKAWA kupitia Mradi wake wa TUWALINDE WATOTO.

 

 

Subscribe to our Newsletter

Get latest updates of our stories, News and other updates from TKT direct to your email.