MTOTO WA TWAHA RUBAHA KIDUKU, SAMEER TWAHA AKABIDHIWA UBALOZI WA GREEN APPLE DAY CARE CENTERS

Sameer Twaha ambaye ni mtoto wa Bondia anayefanya vizuri nchini Tanzania amepewa ubalozi wa kuvitangaza vituo vya kulelea watoto mchana, vya Green Apple day care Centers vilivyopo Kata ya Kilakala, Kata ya Mazimbu na Kata ya Mkundi katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ubalozi utakaodumu kwa kwa muda wa miaka miwili.

Bondia Twaha Kiduku akisani mikataba ya ubalozi wa Mwanae Sameer Twaha.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika katika Kituo cha kata ya Kilakala, Mkurugenzi wa Green Apple day care, Mwajabu Kusaga alisema  “mimi kama Mkurugenzi wa Gree Apple na  mdau wa watoto tumeona Sameer awe Balozi wa vituo vyetu vya day care ni kwanini Sameer, kwasababu kama ambavyo Baba yake Sameer kwa kipaji alichonacho na sisi pia Green Apple tunaamini kwenye vipaji vya watoto, sasa tukaona kwa kumtumia Sameer na nembo ya Baba yake hivyo ni mudada wa Sameer kuweza kuhamasisha watoto wengine waweze kujihusisha katika vipaji mbalimbali walivyonavyo ikiwemo Ngumi’’

Nae Bondia Twaha Rubaha Kiduku amepokea vyema ubalozi wa mtoto wake akishukuru uongozi wa Shule za Green Apple kwa kumchagua mtoto wake kuwa balozi wa Green Apple day care.

“Nipende kuwaambia watu wa Morogoro wenye watoto wao wa umri kama huu kuwaleta watoto wao katika vituo vya Green Apple day care centers kikukweli mazingira ni mazuri na kuna utulivu” alisema Bondia Twaha Rubaha maarufu Twaha kiduku.

Aishan Makeki ni watengenezaji wa Keki bora wanakukaribisha katika Ofisi yao iliyopo Masika Morogoro kwa mahitaji ya Keki popote ulipo watakuhudumia piga simu namba: 0713835087 au 0625900801.

Miongoni mwa waliohudhuria katika mkutano huo wa waandishi wa Habari ni Mzazi aliyejitamburisha kwa jina moja la Rahma ambaye ni mzazi wa mtoto Najma Ally anayesoma katika kituo cha Green Apple Kilakala, alisema mtoto wake alivyompeleka hakuwa afahamu hata kuzungumza vizuri lakini sasa anaweza hata kutaja majina yake na kujitamburisha kwa kiingereza pamoja na kujiamini kwake kumeongezeka.Chuo cha Victory kinachotoa mafunzo mbalimbali ikiwemo ujasiriamali, kinawakaribishia katika muhula mpya wa masomo kwanzia December 2021, chuo kipo Sabasaba jengo la CCM Mkoa wapigie sasa: 0715176176.Rahma aliongeza kuwa “ mwanangu katika mtihani wa mwezi wa sita alishika nafasi ya kwanza na mtihani wa mwezi wa kumi na mbili amekua wa pili, kwa hiyo naweza sema kwamba Green Apple ni Shule nzuri sana na walimu wake ni rafiki pia mtoto anakua na hamasa ya kwenda Shule”

Subscribe to our Newsletter

Get latest updates of our stories, News and other updates from TKT direct to your email.