SHINE UP DAY CARE CENTER YATAJWA KUWA MKOMBOZI KWA WATOTO KUPATA ELIMU NA MALEZI BORA

Shine Up Day Care Center ni kati ya kituo cha kulelea watoto mchana kilichopo mtaa wa mkwajuni kata ya Mindu ndani ya Manispaa ya Morogoro, kituo hiki kilianzishwa mwaka 2020, na Mwaka 2021 kimetimiza miaka miwili na kufanya Mahafali yake ya pili tangu kuanzishwa kwake mwaka 2020.

Kwa mujibu wa  Mkurugenzi wa kituo hicho Bi, Upendo Mchau kupitia risala iliondaliwa kwa mgeni Rasimi alisema mwaka 2021 wamehitimu watoto kumi na saba (17) ambao wote wamefauru kujiunga na shule ya msingi kuanza Darasa la kwanza mwaka 2022 jambo ambalo ni miongoni mwa mafanikio ya kituo ikiwa ni pamoja na kutoa malezi bora kwa watoto.

Afya ni mtaji wa kwanza katika maisha, ilikufanya yote uyatakayo ni lazima uwe na afya bora,Fukang Health Care niwataalamu wa kutibu magonjwa ya binadamu, wanapatikana Morogoro unaweza kuwapigia simu namba. 0758903458.

Mgeni Rasmi wa Mahafali ndg. Razack Seleman akiijibu Risala hiyo alianza kwa kuwapongeza vijana wenzake wamiliki wa kituo kwa kuanzisha kituo cha  kulelea watoto  ambacho kimekuwa msaada kwa jamii ya watu wa Kata ya Mindu, na kuwa asa wazazi na walezi kufanya uchaguzi sahihi kuwapeleka watoto wao Shine up day care kupata Elimu na malezi yaliyo bora.

Akizungumza kwa niaba ya wazazi, Mlezi wa Shine up day care center Mchungaji Katana Mwangome alisema Kituo cha Shine up dad care kimebadilisha maadili ya watoto kuwa mazuri nidham yao ikiongezeka hivyo wazazi wamekua na matumaini makubwa ya kuwapata viongozi bora wa Taifa la kesho kupitia Shine up day care Center.

Picha zenye ubora,Video zenye ubora na matangazo yenye ubora zaidi huandaliwa na vifaa vyenye ubora zaidi, kwa maana ya Camera za kisasa, unazipata Morogoro kwa ASAK TECHNOLOGY, sim 0658251765.

Miongoni mwa wageni wa heshima waliohudhuria Mahafali ya Shine up day care center ni Diwani wa Kata ya Mindu Mheshimiwa Zuberi Mkaraboko na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkwajuni Bwana Juma Balali.

 Na, Hamad Rashid.

Subscribe to our Newsletter

Get latest updates of our stories, News and other updates from TKT direct to your email.