TAKWIMU: KIWANGO CHA USAJILI WA WATOTO WENYE ULEMAVU DARASA LA AWALI KILISHUKA 2020


Jumla ya watoto wenye ulemavu 6912 walioandikishwa Darasa la chekechea wakike walikuwa 3,334 na wakiume walikuwa 3,578 kwa mujibu wa ripoti iliyozinduliwa sepemba 14, 2021ya utafiti juu ya upataji elimu ya awali/ kindagaten kwa watoto wenye ulemavu Tanzania Bara.

Kipengele hiki kilichopo katika ukurasa wa 14 wa Ripoti, kinaonesha kundi la miaka mitano watoto wa kiume walikua 1514  na wa kike wakiwa 1475 ikiwa ndio kundi lenye watoto wengi wenye ulemavu waliongoza kuandikishwa mwaka 2020. 

Idadi ya watoto wenye ulemavu walisajiliwa darasa la awali imeshuka kutoka watoto 7578 mwaka 2019 hadi kufikia watoto 6912 mwaka 2020. 

Jedwali hapo chini linaonesha uhalisia. 

 

 

UMRI

WATOTO WA KIUME

WATOTO WAKIKE

JUMLA

 

2020

MIAKA 3

146

158

304

MIAKA 4

695

673

1368

 

MIAKA 5

1514

1475

2989

 

MIAKA 6

843

682

1525

 

ZAIDI YA MIAKA 6

380

346

726

 

Chanzo: Haki Elimu

Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: -

John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com 

Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com

Our main partner

Subscribe to our Newsletter

Get latest updates of our stories, News and other updates from TKT direct to your email.