TAKWIMU: KIWANGO CHA USAJILI WA WATOTO WENYE ULEMAVU DARASA LA CHEKECHEA KILISHUKA 2020
Jumla ya watoto wenye ulemavu 6912 walioandikishwa Darasa la chekechea wakike walikuwa 3,334 na wakiume walikuwa 3,578 kwa mujibu wa ripoti iliyozinduliwa septemba 14, 2021ya utafiti juu ya upataji elimu ya awali/ kindagaten kwa watoto wenye ulemavu Tanzania Bara.
Kipengele hiki kilichopo katika ukurasa wa 14 wa Ripoti, kinaonesha kundi la miaka mitano watoto wa kiume walikua 1514 na wa kike wakiwa 1475 ikiwa ndio kundi lenye watoto wengi wenye ulemavu waliongoza kuandikishwa mwaka 2020.
Idadi ya watoto wenye ulemavu walisajiliwa darasa la awali imeshuka kutoka watoto 7578 mwaka 2019 hadi kufikia watoto 6912 mwaka 2020.
Jedwali hapo chini linaonesha uhalisia.
UMRI |
WATOTO WA KIUME |
WATOTO WAKIKE |
JUMLA
|
2020 |
|||
MIAKA 3 |
146 |
158 |
304 |
MIAKA 4 |
695 |
673 |
1368
|
MIAKA 5 |
1514 |
1475 |
2989
|
MIAKA 6 |
843 |
682 |
1525
|
ZAIDI YA MIAKA 6 |
380 |
346 |
726
|
Chanzo: Haki Elimu
Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: -
John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com
Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com