UTAFITI: SHULE NYINGI HAZINA VYOO KWAAJILI YA WATOTO WENYE ULEMAVU

Ripoti ya utafiti juu ya upataji Elimu ya awali kwa watoto wenye ulemavu Tanzania Bara , iliyozinduliwa sepemba 14, 2021 na Shirika la Haki Elimu Tanzania, imebainisha hali ilivyo kuhusu vyoo kwa watoto wenye ulemavu wa darasa la awali Nchini.

Katika utafiti huo Shule nyingi zina vyoo vya shimo, ingawa katika hali tofauti baadhi ya vyoo viko katika hali nzuri wakati vingine haviko kwenye hali nzuri.

Kwenye Shule zote zilizo tembelewa takriban 75% ya shule hizo hazina vyoo vya watoto wenye ulemavu,watoto hao wenye ulemavu wamekuwa wakishiriki vyoo na watoto wengine wasio wenye ulemavu.

 Ni 15% tu ya shule zina vyoo  vinavyo kidhi mahitaji ya watoto wenye ulemavu,na takriban 10% ya shule zina vyoo vya watoto wenye ulemavu ingawa hazikubadilishwa ili kukidhi mahitaji ya watoto wenye ulemavu, baadhi ya shule ziligundulika kuwa na vyoo vilivyoboreshwa lakini havitumiki.

Kati ya shule za msingi zilizotembelewa katika Manispaa ya Tanga, kulikuwa na vyoo maalum vilivyotengwa kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, ingawa havitumiki, badala yake, vilitumika kama chumba cha makopo matupu ya maji.

Vile vile, katika shule nyingine vyoo vya watoto wenye ulemavu vilikuwepo na viko katika hali nzuri lakini havikutumika kwani walikuwa wamefungwa kila wakati.

Aidha ripoti hiyo ya utafiti ilibainisha kuwa asilimia 70 ya shule zilizotembelewa hazikuwa na vyoo vilivyotengwa kwa wanafunzi wa darasa la awali.

Chanzo: Haki Elimu

Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: -

John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com 

Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com

Subscribe to our Newsletter

Get latest updates of our stories, News and other updates from TKT direct to your email.