VIPAJI VYA WANAFUNZI WA SUN SHINE DAY CARE VYAWAKOSHA WAGENI WAALIKWA KATIKA MAHAFALI YA KUHITIMU CHEKECHEA

Siku ya tarehe 04/12/2021 yalifanyika Mahafali ya wanafunzi wanane waliohitimu Elimu ya Kindagate katika kituo cha kulelea watoto mchana Sun shine kilichopo eneo la Nanenane Manispaa ya Morogoro, ambapo wahitimu walionesha uwezo mkubwa kutumia vipaji walivyonavyo ikiwemo mitindo ya mavazi na kuimba.

Mgeni Rasmi katika hafla hiyo Afisa muuguzi Rachel Missago alisema ‘’nimefurahishwa na uwezo walioonesha watoto nimeona wanavipaji lakini pia walimu wamefanya kazi kubwa mpaka sasahivi tunashuhudia maendeleo mazuri ya watoto wetu, walimu walezi hongereni sana’’

     wanafunzi wahitimu wa Sun shine day care wakiwa wamevalia mavazi ya harusi

Bi, Rachel aliongeza kuwa wazazi wanapaswa kujitoa ili kuchangia kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za walimu ili kuendelea kufurahia malezi bora wanayopata watoto ikiwa ni pamoja na kuchangia vifaa vya michezo au Rasilimali Fedha.

Akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Sun Shine day care, Witness Foya alisema kituo kimekua na mafanikio makubwa tangu kianzishwe, ambapo kikubwa ni wazazi kuwa waelewa na kupenda huduma ya malezi ya watoto yanayotolewa kituoni hapo.

Asaki Technology ndio Duka pekee la vifaa Bora ukiwa Mjini Morogoro wanapatikana Mtaa wa Ngoto wapigie kwa kupata huduma uitakayo: 0658251765.

Mwadawa Milambo ni miongoni mwa wazazi waliohudhuria Mahafali alisema ‘’kwakweli hii Sun Shine day care ni mkumbozi katika Jamii yetu, ni Kituo ambacho kinafanya vizuri, kinafundisha vizuri na kinawalea watoto wetu katika malezi bora’’

Zakwetu Africa ni Brandi ya ushonaji Nguo za kisasa za kiafrica iliyopo Mtaa wa Uhuru Mjini Morogoro, karibu ujipatie mavazi tofauti tofauti unaweza piga simu kwa mawasiliano: 0693550074.

Kituo cha Sun shine day care, kilianzishwa Mwaka 2018, hii ikiwa ni Mahafali yake ya Nne kufanyika Mwaka 2021 kikiwa na jumla ya wanafunzi wanane waliohitimu tayari kujianga na Shule za Msingi kwa ajili ya masomo ya Darasa la kwanza Mwaka 2022.

Na Hamad Rashid

Subscribe to our Newsletter

Get latest updates of our stories, News and other updates from TKT direct to your email.