WANAFUNZI WANAORUDI SHULE BAADA YA KUJIFUNGUA WAPEWE ELIMU YA SAIKOLOJIA KWANZA

                           Herriet Mkaanga Mkurugenzi wa Taasisi ya My Health Foundation.

Kufuatia waraka wa Serikali ulioelekeza wanafunzi wa kike waliopata ujauzito warejee shule katika mfumo rasmi baada ya kujifungua wadau wa Elimu nchini wameipongeza Serikali kwa hatua hiyo.

Herriet Mkaanga, mwanaharakati wa watoto wa kike na Mkurugenzi wa Shirika la My Health Foundation  ambalo limekua likipigania suala hili kwa muda mrefu, aliishukuru  Serikali kwa hatua hiyo na kutoa maoni yake kuwa wapatiwe Elimu ya saikolojia kabla ya kurejeshwa Shule ili wakafanye vizuri zaidi.

Fika Fahari Shop kwa huduma zaidi za malighafi ya mbalimbali ya kutengenezea Bidhaa.

Mkaanga pia alisema juhudi nyingine zinazotakiwa kuchukuliwa dhidi yao ni kuwezesha mazingira yao ya kujifunzia ili wasiingie tena katika ushawishi wa kupata ujauzito ikiwemo, kuwasaidia taulo za kike, vyakula kwa Shule zenye mabweni.


watoto wakiwa kwenye sare kutoka kituo cha kulelea watoto Step up day care center Sabasaba Morogroro. mawasiliano yao: 0756557228.

kwa mujibu wa Takwimu za Elimu ripoti ya Best 2020 inaeleza jumla ya idadi ya wanafunzi wa kike 1,135 sawa na 0.7% walipata ujauzito katika Shule za Msingi, ilhali shule za Sekondari walikua 5,398 sawa 5.5% mwaka 2019.

Na John Kabambala.

Subscribe to our Newsletter

Get latest updates of our stories, News and other updates from TKT direct to your email.