WATOTO WANANE WAMEHITIMU ELIMU YA KINDAGATE MJOI DAY CARE AND NURSERY SCHOOL WALEZI WAPONGEZWA

         wanafunzi wahitimu wa Elimu ya kindagate Mjoi day care and Nursery School.

Pongezi hizo zilitolewa na wazazi pamoja na walezi waliohudhuria katika Mahafali ya pili ya kituo cha kulelea watoto mchana, Mjoi day care and Nursery School iliyofanyika katika ukumbi wa nje katika kituo hiko kilichopo Kata ya Kasanga Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Abugae Hamisi ni miongoni mwa wazazi waliohudhuria Mahafali hayo alisema ‘’niwaombe wazazi wenzangu kuwa, Elimu ni huduma na huduma haina mipaka kwa hiyo popote ulipo mlete mwanao hapa Mjoi day care walezi wa hapa wanafundisha vizuri na watoto wanaelewa’’

Mzazi mwingine ni Asia Mohammed ambaye watoto wake wawili wamesherehekea Mahafali Mjoi day care and Nursery School alisema ‘’kwakweli kituo ni kizuri, mwanangu mmoja kamaliza mwaka jana hapahapa na ninashukuru mpaka leo hii yuko vizuri na shule niliyompeleka anafanya vizuri, kituo hiki walimu wake wanafundisha vizuri na kina mazingira mazuri kwa watoto kukaa’’  

                Kikumbi Culture and desgning wanakukaribisha kufika Ofisini kwao Mtaa wa Uhuru karibu na Uhuru Park ujionee vitu vya asili vinavyotengenezwa kwa ajili yako muafrika ikiwemo uchoraji. unaweza kuwapigia sasa:  0659880721 au 0715262709.

Ndugu mwandishi wa Habari leo ilikua ni Mahafali yetu hapa Mjoi day care and Nursery School, tunamshukuru Mungu kwamba wanafunzi wetu tumewaandaa vizuri na hatimaye siku ya leo wameweza kukamilisha muda wao wa kuwepo hapa tayari kwa ajili ya kujiunga na Shule za Msingi’’ alisema Mbwiliza Wilson Mfunya Mkurugenzi wa Mjoi day care and Nursery School.

Mbwiliza aliongeza kuwa ‘’Mwaka 2022 tumejipanga kuboresha zaidi mazingira ya watoto kujifunzia ili kuendele kutoa malezi bora ya watoto kwasababu tunaamini tutakua na watoto wengi zaidi ya Mwaka huu, na niwaombe wazazi na walezi kuwaleta watoto wao hapa sehemu sahihi ya malezi bora ya watoto’’

Ikiwa ni Mahafali ya pili kufanyika Mjoi day care and Nursery School, Jumla ya wanafunzi wanane wamehitimu Elimu ya kindagate ilhali Mwaka 2020 watoto waliohitimu walikua waawili tu.

     Na Hamad Rashid.

Subscribe to our Newsletter

Get latest updates of our stories, News and other updates from TKT direct to your email.