WAZAZI WAHIMIZWA KUWAPELEKA WATOTO WAO KITUO CHA VALENTINE DAY CARE CENTER KILICHOPO MAZIMBU

Akizungumza katika Mahafali ya pili ya Kituo cha kulelea watoto mchana yaliyofanyika katika kituo hicho kilichopo Mtaa wa Reli Kata ya Mazimbu, Mgeni Rasmi wa hafla hiyo Mwenyekiti wa Mtaa wa Reli Henry Sebastian Mapunda alisema, wazazi na walezi ni vyema kuwapeleka watoto wao Valentine day care ili wakapate malezi bora kulingana umri wao.
Keki kama hizo utazipata kwa Aishan Makeki wako masika kituo cha daladala Manispaa ya Morogoro, wanapokea oda zote wasiliana nao kupitia: +255 713 835 087.

Kwa upande wa Mwalimu mlezi wa Valentine day care Salome Mbowe alisema, “watoto wananipenda na mimi ninawapenda”.

Salome aliongeza kwa kuwapongeza wanafunzi wake Benedict Sanga na Naurath Simba kwa uelewa mzuri walionao akiahidi kuwa amejipanga kuongeza ujuzi zaidi kwa Mwaka wa 2022 akiamini watoto watakua wengi zaidi ya Mwaka huu wa 2021.


Darasa la Ujasiriamali likiwa linaendelea katika Chuo cha Victory Morogoro, ambao sasa wanaendelea kupokea wanafunzi kwa ajili ya muhula mwingine wa masomo, Chuo kipo Sabasaba Jengo la CCM Mkoa Ghoroga ya Tatu, mawasiliano yao ni: +255 715 176 176.

Tanzania kids time ilizungumza na Mzazi Suzana Mzumbwe ambaye ni Mama wa Mwanafunzi Benedict Sanga aliyehitimu Elimu ya Chekechea, alisema “mtoto wangu amesoma hapa na leo amehitimu, kwakweli ni Shule ambayo wamemlea vizuri, kitaaluma yuko vizuri, Mwalimu wake yuko vizuri maendeleo ya mwanangu nimeyapenda yako vizuri na nina uhakika Shule atakayoenda atafanya vizuri” alisema Suzana Mzumbwe.

Mkurugenzi wa Valentine day care Center Mwalimu Margareth Valentine alisema, Kituo chake kinapokea watoto wa kuanzia umri wa Mwaka mmoja hadi miaka mitano hivyo wazazi na walezi wanaosumbuka kutafuta binti wa kazi za nyumbani sasa wamepata suluhisho.

Bi Margareth aliongeza kuwa, wanapokea watoto wa aina mbili, wanaotoka sa sita mchana na wanaotoka sa kumi jioni.

Kituo cha kulelea watoto mchana Valentine day care kimefanya Mahafali yake ya pili ambapo watoto waiwili wamehitimu Benedict Sanga na Naurath Simba.

Na John Kabambala.

Subscribe to our Newsletter

Get latest updates of our stories, News and other updates from TKT direct to your email.