UTAFITI: WATOTO WA
MKOA WA RUKWA NI MASKINI ZAIDI TANZANIA.
Matokeo ya Utafiti wa hali ya Uchumi Tanzania Mwaka
2017/2018 yanaonesha Mkoa wa Rukwa unaongoza kwa kuwa na watoto Maskini zaidi
kwa upande wa Chakula na Mahitaji ya Msingi.
Aidha Mkoa wa Dar es salaam umekua na kiwango kidogo katika
upande wa umaskini wa mahitaji ya Msingi wakati Mkoa wa Mara nao ukiwa na
kiwango kidogo cha Umaskini wa Chakula kwa watoto wa umri wa miaka 0-17.
Jedwali hapa chini linafafanua maelezo yaliyotangulia hapo
juu, kwa mujibu wa Utafiti wa Serikali kupitia kitabu cha hali ya Uchumi wa
Taifa Mwaka 2018.
MKOA. |
UMASKINI WA MAHITAJI YA MSINGI |
UMASKINI WA CHAKULA |
RUKWA. |
47.6% |
21.2% |
DAR ES SALAAM. |
9.6% |
———————————— |
MARA. |
———————————————- |
1.9% |
Imeandaliwa na John Kabambala & Hamad Rashid.