|
|
Karagwe.
Wanawake
wilayani karagwe mkoani Kagera kupitia katika vikundi vyao vya
maendeleo wametakiwa kujikita katika utoaji wa elimu ya lishe ili
kuwezesha wilaya hiyo na mkoa wa Kagera kwa ujumla kuondokana na udumavu
kwa watoto.
Akizungumuza na wanawake wa kikundi cha
wanawake na maendeleo katika kata ya Kayanga wilayani Karagwe wakati wa
zoezi la kuwajengea uwezo kuhusu njia za kujikomboa kiuchumi katibu wa
mbunge wa jimbo la Karagwe Ivo Ndisanye amesema kwamba kutokana na
wilaya Karagwe kuwa miongoni mwa wilaya zinazokabiliwa na hali ya
udumavu kwa watoto ni vyema wanawake kupitia katika vikundi vyao vya
maendeleo wakajikita katika utaoaji wa elimu ya kuhamasisha lishe nzuri
hasa kwa watoto ili kusaidia wilaya Karagwe na mkoa Kagera kwa ujumla
kuondokana na udumavu.
Aidha wilaya Karagwe
imeendelea kukabiliwa na hali ya udumavu kutokana na idadi kubwa ya familia
kuendelea kula chakula cha aina moja, kuuza vyakula vyenye lishe
sokoni badala ya kuvitumia ni pamoja na baadhi ya wakina mama kutojali
lishe kwa watoto wao na kujikita zaidi katika shughuli za ujasiriamali.
Hata hivyo baadhi ya wanawake Jovitha Kombe diwani wa viti maalum tarafa
Nyabiyonza na Doresela Reopord wamesema kuwa kutokana na elimu
waliyopatiwa watasaidia vikundi vingine vya wakina mama kuvijengea uwezo
wa kuedelea kuelimisha suala la lishe kwani bado mwitikio wa wakina
mama wilayani Karagwe kuthamini suala la lishe kwa watoto hasa vijijini
haujaridhisha.
Na mwandishi wetu Jovinus Ezekieli kutoka Karagwe Kagera.