Wakuu wa shule za msingi na maafisa elimu katika tarafa ya IGAGALA wilaya ya KALIUA mkoani TABORA wametakiwa kuhamasisha wazazi kuchangia chakula shuleni.
Akizungumza kwenye kikao na wakuu wa shule za msingi, maafisa elimu wa kata na watendaji wa kata katika tarafa ya IGAGALA, Afisa tarafa wa IGAGALA, SIMON MALANDO amesema suala la chakula mashuleni linahitaji ushirikiano wa viongozi wa serikali kutoa elimu na hamasa kwa wazazi,aidha mara baada ya kuhamasisha wazazi wenyewe wasimamie utunzaji wa chakula.
Kwaupande wake afisa elimu kata ya USENYE, DOTTO MDIHU ameshauri shule kuwa na mashamba ya kulima huku mkuu wa shule ya msingi UGANSA, COSMAS LEONARD akisema baadhi ya wazazi hawana mwamko wa kutoa chakula.
Kwa upande wao Mkuu wa shule ya msingi KOMBE, FILIMON SAGATWA na mkuu wa shule ya msingi KAZANA UPATE, JOSEPHINA MSIGALA wamesema kikao hicho kimekuwa chachu ya wao kuongeza bidii hasa kusimamia elimu.
Kwa mujibu wa afisa tarafa amesema kikao hicho kilikuwa na lengo la kupokea matokeo ya darasa la saba katika tarafa yake nakujadili changamoto za waalimu kwenye shule zilizopo kwenye maeneo yao,ilikuendelea kuboresha sekta ya elimu hapa nchini.
Na Simon Jumanne Kaliua Tabora