Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 50 mkazi wa kijiji cha Mwingilo Kata ya Ikunguigazi wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita ametokomea kusikojulikana baada ya kunusulika kukamatwa na wananchi kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 11.
Mwanamume huyo aliyefahamika kwa jina la Benjamin Samwel mwenye umri wa miaka 50,nahiyo simara yake ya kwanza kufanya matukio kama hayo kwa mjibu wa wananchi wa eneo hilo, hatahivyo kwa maelezo ya Mama Mzazi wa mtoto huyo bi,pili lugwisha na baba mzazi ndg, masele lumwecha wamesema wamekuwa wakisikia taarifa nyingi zinazo muhusu ndg. Benjamin zakuwafanyia watoto wadogo unyama kama huo.
Mtemi wa sungu sungu katika kijiji hicho ndg, JOHN LUSUGA Amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumapili Ya Novemba 10 saa tatu usiku na alipewa taarifa na mama mzazi wa mtoto huyo na akaandaa safu yake ya ulinzi Ili Kumkamata mtuhumiwa huyo lakini hawakufanikiwa kumkamata walipo fika kwenye eneo la tukio akawa amesha fanya ukatili huo na kutokomea kusiko julikana .
Aidha ndg, John lusuga ametoa tahadhari kwa wananchi ambao watajitokeza kununua mali yoyote ya mtuhumiwa bila kibali kutoka polisi ama sungu sungu ambazo sasa zinamilikiwa na mke wa mtuhumiwa bi Joyce mabla watachukuliwa hatua kali za kisheria kwani zimewekwa kizuizini,na atakae bainika kufanya hivyo atafungwa miaka (30) badala ya mtuhumiwa.
Kutokana na maamuzi ya mkutano wa dharura wa wananchi walimtaka mke wa mtuhumiwa alipe gharama zote zilizotumika katika matibabu na ng’ombe Mmoja bila kipingamizi chochote na kutoka kw mke wa mtuhumiwa,hata hivyo Katibu wa sungu sungu katika kijiji hicho ndg Manyasa Daudi,amewaomba wananchi kuwa wa vumilivu kwa kipindi ambacho mtuhumiwa wanaendelea kumtafuta hadi atakapo patikana na akatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa endapo kunamtu atakae muo mtuhumiwa huyo atoe taarifa kwenye ofisi za serikali popote pale.
Kwa upande wake mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho ambaye jina lake limehifadhiwa na ameeleza Chanzo kwani alikuwa amebakwa zaidi ya mara moja na baba huyo jambo lililo mfanya kumueleza mama yake baada ya kuendelea kusikia maumivu ya mara ya kwanza.
Na Nichoraus Paul Lyankando Mbogwe Geita.
Yaani huyo baba serikali ifanye jitihada akamatwe wasiseme katokomea pasipo julikana ili apatiwe adhabu ambayo iwe fundisho kwa wanaume wenye tabia hizo. Na watoto wa kike wajihadhari sana na wawe wazi kwa wazazi wao hata kama wameona kuna mtu anamunyemelea watoe taarifa ili kulinda watoto taifa la kesho
Irene Gomanga – Morogoro
Shukrani sana kwa maoni yako hayo bilashaka jeshi la polisi kwa kushirikiana na jeshi la jadi sungu sungu wataendelea kumtafuta. subribe iliuwe unapata taarifa za matukio mbalimbali kila tupandishapo kwenye tovuti yetu.