Wananchi wa kata ya Kihonda Magorofani walalamika kuhusu watoto wao kupangiwa shule iliopo kata nyingine ambayo nikata ya Mazimbu na isiwe kata walio somea, wakizungumza nje ya geti la ofisi za Manispaa ya Morogoro mapema leo hii,
Akizungumza kwa niaba ya wazazi wenzanke walioandamana Bi, Vicktoria Charlse amesema uchaguzi uliofanyika hawakutenda haki kwani serikali ilianzisha mpango wa kila kata iwe na shule yake ilikupunguza msongamano wa watoto kwa darasa moja, hivyo haiwezekani watoto wakata husika wasipangiwe kwenye shule iliopo kwenye kata yao wakapangiwa kata nyingine kata husika wakaletwa watoto kutoka kata nyingine.
Aidha kwa upande wa wanafunzi waliopangiwa shule iliopo kata nyingine ni Jamari Amiri alieambatana na wazazi wake kufahamu nikwanini uchaguzi na upangaji washule hizo umepangwa hivyo,amesema hakulidhishwa na uchaguzihuo kwani walikopelekwa nimbali kutoka kwenye kata hiyo.
Hata hivyo kwa upande wa serikali kwangazi ya Manispaa ya Morogoro kupitia kwa Afisa Elimu sekondari Leonard Akwilapo amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati wakiendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo iliojitokeza kwenye kata ya Kihonda.
Umbali wa shule ulipo na uwezo wa mzazi ndo shida hasa ukizingatiaaa hali ya uchumi ilivo kwa sasa
Bilashaka mkuu ndio maana wana lalamika.