Imeelezwa kuwa chanzo kikuu cha mtoto kudumaa
akili ni kukosa lishe bora, kupata maradhi ya mara kwa mara na kutokuwa na makuzi mazuri.

Hayo yameelezwa katika mafunzo
ya siku mbili yaliyotolewa na Shirika la umoja
wa mataifa Elimu, sayansi na
utamaduni-UNESCO kwa wazazi na
walezi katika Ukumbi wa ofisi ya afisa mtendaji wa kata ya IBISABAGENI
Wilayani SENGEREMA ambapo mwezeshaji wa mafunzo
ADAM SALUM anasema mtoto
akikosa lishe bora hatakuwa na
makuzi mazuri , uwezo wa akili kudumaa pamoja na kupata maradhi ya mara kwa mara.

Naye Afisa maendeleo ya
Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya SENGEREMA ambaye pia ni mratibu wa mradi huo unaofadhiliwa na UNESCO Bwana ABELL BARNABAS amewataka wazazi na walezi walioshiriki mafunzo hayo
kwenda kuyafanyia kazi ipasavyo Elimu ya mafunzo pamoja na kuwa mabalozi
wema katika jamii.

Washiriki wa
mafunzo hayo pamoja na kuwashukuru wawezeshaji
wa mafunzo chini ya shirika la
unesco wameahidi kwenda kuyafanyia kazi
walichojifunza ikiwa ni pamoja na kuwalea watoto katika mazingira rafiki.

Aidha Jumla ya
wazazi na walezi Hamsini wamepatiwa mafunzo ya siku mbili juu ya makuzi, malezi na maendeleo ya awali
ya mtoto katika kata ya IBISABAGENI Wilayani Sengerema.

Na Deborah Maisa -Mwanza