Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe imemuhukumu
mwalimu Focus Mbilinyi kwenda jela
miaka mitatu kwa kosa la kumuadhibu na kumsabishia ulemavu wa uti wa
mgongo Hosea Manga aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya msingi
Madeke,Aidha mahakama imemtaka Focus Mbilinyi
kulipa shilling million 10 ikiwa ni fidia ya gharama za matibabu alizozitumia
mtoto hosea Manga Wa shule ya msingi Madeke iliyopo Wilayani Njombe.

Akisoma hukumu hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa
Njombe Ivan Msaki amesema Mahakama
imemuhukumu mwalimu Focus Mbilinyi
kwa kosa la kujeruhi kinyume na sheria namba
225 kifungu kidogo cha 1 sura ya
16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 baada ya
kupitia hoja za mashahidi watano
wa upande wa jamuhuri na watatu wa upande wa utetezi ,Mahakama imejikita kwenye
sheria ya elimu ya utolewaji wa adhabu
kama ulifuata utaratibu ukiwemo wa kusimamiwa na mkuu wa shule wakati adhabu
inatolewa ambaye angethibitisha idadi ya viboko vilivyotolewa.

Hakimu Ivan
Msaki amesema ushaidi uliotolewa na
shahidi wa kwanza ambae ni Hosea Manga uliieleza mahakama kuwa
alichapwa viboko kumi baada ya kukosa hesabu kumi huku akiwa amening’inizwa
miguu juu kichwa chini ushahidi uliojumlishwa na shahidi mwingine mwanafunzi Given Nyangwine na kuithibitishia mahakama kuwa mshtakiwa ametenda
kosa.

Mahakama imeeleza ushahidi na kielelezo
kilichotolewa kutoka taasisi ya mifupa Muhimbili idara ya upasuaji uliotolewa na Daktari Silvery Mwesige aliyeieleza mahakama kuwa Hosea aliumizwa
sehemu ya uti wa mgongo na kusababisha tatizo kwenye pingiri za mgongo jambo lililopelekea damu kushindwa
kufika sehemu ya chini ya mwili wake.

Hakimu Ivan amesema pamoja na upande wa utetezi uliokuwa na mawakili Innocent Kibadu pamoja
na Octavian Mbugani kuleta mkanganyiko wa ushahidi wa kukataa baadhi ya hoja,
mahakama imeona mkanganyiko huo hauna maana kwenye kesi ya hiyo.

Katika kesi hiyo namba 141 ya mwaka 2019 Wakili wa serikali Radhia Njovu ameiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho
na pia kumtaka mshtakiwa kulipa fidia kulingana na sheria ya fidia namba
348 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria
ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20
kwa kuwa muathirika ametumia gharama kubwa za matibabu kuanzia alipoanza
kutibiwa mpaka hivi sasa.

Mahakama imetoa siku 30 kwa mshtakiwa kukata rufaa
katika Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa mwezi novemba mwaka jana . Mnamo tarehe
21 mwezi
machi mwaka 2017 Mtoto Hosea Manga
mwenye umri wa miaka 12 akiwa darasa la
tatu katika shule ya msingi madeke
anadaiwa kuadhibiwa na mwalimu huyo na kusababishiwa maumivu.Maumivu hayo
yaliwafanya wazazi wake wachukua hatua za kumfikisha kwenye zahanati ya
kijijini hapo na kisha kuhamishiwa kituo
cha afya na baadaye kwenda hospitali ya
misheni ya ikonda kabla ya kufikishwa
hospitali ya kibena iliyokuwa hospitali
teule ya mkoa wa njombe kwa wakati ule.

Hata hivyo Hosea alipewa rufaa na kuhamishiwa Dar es
salaamu katika taasisi ya mifupa Muhibili
ambako aligundulika amevunjika uti wa mgongo na hivyo kupewa matibabu na
kiti cha kutembelea huku akiendelea na matibabu.

Baadaye kesi
namba 83 ya mwaka 2017 ikafunguliwa dhidi ya mwalimu huyo nakisha ikafutwa kutokana na daktari aliyemtibu
kutoka hospitali ya muhimbili kushindwa
kufika mahakamani kutoa ushahidi licha ya kuitwa mara nane kabla ya
kufunguliwa tena kwa mara ya pili novemba
2019 ambayo tamati yake imefikia
na kuamuliwa kwenda jela kutumikia mitatu.

Na,Michael Ngilangwa-Njombe.